Tuesday, March 19, 2013

TWISTED COMING SOON

Baada ya Waves of Sorrow kutingisha soko la ndani ya Nchi na Nje ya Nchi sasa ni zamu ya bonge la Movie linaenda kwa jina la Twisted ni movie kali sana si ya kuikosa kama kawaida ya Rj Company huwa hatubaatishi  katika swala zima la kazi tucheki jinsi location watu walipokuwa wanauandaa mzigo huo..

Cheki mwenyewe jinsi watu walivyojipanga katika kazi siunaona jinsi mataa yalivyosetiwa huku ni kutafuta ubora wa hali ya juu kama kawaida ya RJ COMPANY..

Mambo yakiendelea kama kawaida yetu hapa nikihakiki picha yangu kabla ya kuingia On Set

Mzee Masinde na Mama Njaidi On Set..


Msanii mpya anaitwa Welu akiwa On Set tunajaribu kuleta sura mpya wadau na tofauti na mlizozizoea..

 The Greatest na Welu msanii wangu mpya tukifanya mazoezi ya mwisho kabla mambo kuanza..

Crane ikifungwa.

Tukifanya majaribio ya crane kabla shughuli kuanza..

Farid Uwezo Cameraman wangu akifanya manjonjo yake akiwa pamoja na Samu Shoo LightMan wa Rj Company na The Greatest nikiwa pembeni yao..

 Vijana wakiwa kazini..

Nikipitia Script kabla ya kuingia On Set..

 Umakini kwenye picha..

Scene ya makaburini..

 The Greatest nikihakiki picha kwenye monita yangu..

Location maeneo ya Mbezi katika Lodge mpya inayokwenda kwa jina la Konfa Lodge

 Kijana Seve Countiunity wa Rj Company..

Scene za vijijini pia zimo safari hii..

Masinde na  Mama Njaidi wakisikiliza maelekezo toka kwa Director..
.
Kwa hiyo wadau wa movie nawaomba msiukose mzigo huu wa Twisted ni hatari sana..

Wednesday, March 13, 2013

KIGALI GENOCIDE MEMORIAL

Wadau tulipata bahati ya kwenda kutembelea Kigali Genocide Memorial katika ziara yetu Nchini Rwanda kwakweli tumejifunza vitu vingi sana Watanzania tupendane na tueshimiane tusiwe na mambo ya udini  wala ukabila maana vita ni kitu kibaya sana usikie tu kwa wenzako na sio nchini kwako tudumishe amani tuliyokuwanayo Watanzania, ukifika hapa ndio utajua ubaya wa vita embu tucheki mambo yalivyokuwa tulipotembelea maeneo haya ya kumbukumbu uliyosababishwa na  vita vya ukabila..

Trafiki aliyekuwa akituongoza kwenye msafara wetu jamani uko tulikuwa kama viongozi wa Nchi niu mwendo wa eskoti ya police yani wanyarwanda wanajua maana ya msanii ni nani maana tulipewa eshima kubwa sana nchini humo

Tukiwasili maeneo ya kumbukumbu na huo ndio msafara wetu wadau..

The Greatest na King Majuto..

 Tukisalimiana na baadhi ya viongozi wa kampuni ya Steps...

Irene Uwoya akisalimiana na Jay toka  kampuni ya Steps...

 The Greatest nikiteta kitu na Irene Uwoya.

Hii ni sinema iliyotengenezwa na Steps iliyofanyika nchini Rwanda ilizinduliwa rasmi nchini humo siku ya Rwanda Film Awards ilikuwa inzungumzia mambo ya Gnocide...

 The Greatest

 Tukielekea kwenye makumbusho..

 Hapa tukipata maelekezo toka kwa wenyeji wetu kabla ya zoezi kuanza..

Baada ya kupata maelekezo hayo tulianza kwenda eneo la kwanza ambalo kuna maiti zilizokaushwa na madawa kwa ajili ya makumbusho ya kuwaambia Wanyarwanda kwamba vita sio kitu kizuri...

Hapa ndio sehemu yenyewe yenye maiti hizo..

Tukipata maelezo toka kwa mtaalam wa sehemu hiyo..

Mambo yakiendelea...

Mwanzo kabisa zilikuwaga zipo wazi lakini baada ya kuwaona Wanyarwanda wengi wakienda kutizama walikuwa wanalia sana na kuzimia wakaamua kuzifunika na mashuka , wadau hizi ni maiti.

Tukiweka mashada kama ishara ya upendo na kuwaombea kwa Mungu wapumzike kwa amani..

Jb akiweka mashada..

King Majuto naye akiweka mashada..

The Greatest pia niliweka mashada

Irene Uwoya..

Tukielekea maeneo mengine ya makumbusho.


Hapa tukipata maelezo jinsi vita vya wenyewe kwa wenyewe vya ukabila jinsi vilivyoanza..

Picha mbalimbali za matukio yaliyotokea..

Vita ni mbaya sana.

Watoto wadogo wengi walikufa kwenye vita hivyo ni simanzi kubwa sana wadau..

Baadhi ya mafuvu binadamu yaliyosababishwa na vita hivyo

Nikisoma baadhi ya kumbukumbu..

Tukijiandaa kuondoka


Mapaparazi hawakuwa nyuma kunioji niliyoyaona katika makumbusho hayo


Tulimaliza na kurrudi hotelini