Thursday, October 11, 2012

SISTER MARRY Baadhi ya wadau msiwe wajuaji sana kabla ya kitu kukijua kuwa  mjinga ili ujue mengi usijifanye mjuaji wakati ujui chochote, nadhani kwa wahusika ujumbe utakuwa umefika na waswahili wanasema kuwa kukaa kimya ndio jibu la mjinga, hili ndio movie yangu mpya inayokwenda kwa jina la Sister Marry iliyotengenezwa na kampuni yako bora ya Rj Company, si mzigo wa kuukosa maana umejaa mafunzo mengi sana lengo ni kufundisha kama kawaida yangu na sikuikashifu dini wacha tuone mambo yaliyofuata uko chini..

 Watawa wakiwa makini kusikiliza mafunzo.

 Masister wakiwa kwenye Ibada.

 Masister wakipata chai ya pamoja.

On set ofisini kwa Sister Mkuu.

Baada ya Ibada.

a
 On Set.......

 Sister Mkuu na Father Criss wakiwa kazini..

 Majukumu ya kikazi yakiendelea.

 Father Criss na Sister Marry mwenyewe ambaye ni Irene Uwoya..

 Scene za Hospital..

Picha ya pamoja baada ya kazi kumaliza kwa siku hiyo..

21 comments:

Anonymous said...

nimeona trailer ya hiyo muvi naisi lengo lako ni kuonesha jinsi baadhi ya watawa wa kike wasio na wito wa kitawa wanavyo changia kuharibu ukatoliki your idea is good .....ila sasa Ray Askofu mbona hana fimbo ya kiaskofu hiyo kofia kubwa ya kiaskofu ikivaliwa katika ibada lazima askofu awe ameshika fimbo ya kichungaji inakuwaga ya dhahabu au silver next time my dear ukikosa vitendea kazi buni njia mbadala mfano badala ya mchezo kuwa na askofu ungetumia kiongozi mwingine wa juu wa kanisa eg paroko au makamu wa askofu ambao hawashiki fimbo ya kiaskofu wala hawavai kofia ya kiaskofu

MDAU WAKO WA UK said...

TATIZO LAKO HUPENDI KUAMBIWA UKWELI THAT WHAY HATA COMENT YANGU IMEIBINYA JAPO UMESOMA KIMYA KIMYA NA NILIKUSHAURI KWA VIZURI TU NADHANI SASA UNATAKIWA KUINGIA SHULE NDIYO UTAELEWA WADAU HUWA WANAKWAMBIA NINI... KWA UZURI TU

Anonymous said...

eti watu wanadai umechukuwa idea jibao toka kwa sister m,ary ya nigeria aisee kuwa makini na story unapozipata kaka kila la heri
angalia kwenye bible ya kingereza sisi wakatoliki tunaita SISTER MARY NA SIO MARRY HATA NGERIA NA WAO WALIKOSEA KUANDIKA POSTORS ZA ZA SISTER MARY YAO KAANDIKA KAMA ULIVYOANDIKA
ILA HUKO FACEBOOK NA TWITER WAZMEKWISHA KUCHAFUA SANA KUHUSU HII MOVIE

Anonymous said...

duh, we kaka umezidi sana kuigaiga... yani hadi jina umekopy.. inabidi Joti aanze kurekebisha na tabia ya kucopy kama anavyofanya kwenye nyimbo.
tunga ya kwako acha kuigaiga bwana, hadi unakera.. najua utaibinya comment yangu lakini ujumbe utakuwa umeupata.
kwanza me toka kanumba afariki wala sijanunua tena movie, na kama nikinunua basi nitanunua za JB n not u. kwanza siku hizi umekuwa fake sana, from nywele hadi kila kitu ni fake tu.
kila kitu we ni copy n paste hata kuedit hujui.

Debby

Anonymous said...

Wasilize wadau mdogo wangu....
Haina haja ya kubishana na mtu..
Kila mtu anutizamo wake
Mdau germany

Anonymous said...

Movie zako za kidini ni nzuri sana.Big up wacha wenye wivu waendelee kupiga kelele.
Pls waambie hao madada wawe wanajiheshimu after shooting,wanatia kicheu chefu.

Anonymous said...

usiwe unajibizana na watatanzania kuwa mkimya lbda kama umeuliza kitu zeni wakikujibu baaasi na ww unawajibu kama mnachati
but mambo mengine kausha..watu si watu..

Anonymous said...

kaka kam unajiususha na kibifu cha ney wa mitego plz.. jitoe kabisa kitakuja kukuchafulia jina please please please....!!
emmer matutu

Anonymous said...

kaka kam unajiususha na kibifu cha ney wa mitego plz.. jitoe kabisa kitakuja kukuchafulia jina please please please....!!
emmer matutu

Anonymous said...

Hangaika na waogizaji woooote cheza nao ila sie wetu ni 1 tu Batuli hao tumewachoka kazi mbovu na tabia pia.

Anonymous said...

Ray usibishane wajinga pambana kaka maisha yako ni movie so work on it nitanunua kwa sababu wewe upo simpendi huyo Irene Uwoya nikimtizama nasikia kinyaa kwa uchafu wake wa tabia

Anonymous said...

Hivi kwanini huoni aibu kucheza movie ma hawa matakataka tumeshakuambia tumewachoka kwanini huelewi what's wrong on your head tutakukimbia siso ndio mashabiki wako umefungua blig ili kujua tunataka nini au umefungua blog kama fashion? Huyu Irene uwoya ana bad attitude unanunua movie unapeleka nyumbani kwa ajili ya kuelimisha jamii sasa aliyecheza movie ni mpotoshaji wa jamii Ray watch your step, kwani Hakuna wasichana warembo wente kujiheshimu huko mbongo movie? Lucy komba, Johari, Riyama, Batuli huwaoni? Badilika

Anonymous said...

Hayati Kanumba alikuwa akisema kwenye Media kuwa wewe ndie ulikuwa mwalimu wake na ulimshika mikono hadi akasimama, kwa miguu yake brother Vincent nina uhakika hata wewe utakuwa ukifurahi na kujivunia kwa kusikia kuwa msanii aliyeiteka africa alikuwa mwanafunzi wako je huyu uwoya unaweza kujivunia kipi kwake? Kama Hakuna iweje umshike mkono wakati anakutukanisha, sifa ya Rj unaishusha thamani

Anonymous said...

Kuna comment hapa zimenikuna inshort wake wasanii scandal watakupotezea fans wote watanzania wa sasa sio wake wa zamani wakichoka utarudi shamba huyu dada kapoteza heshima yake kuna mdau kaongea point blog umefungua kwa ajili ya kazi sio fashion wenzio huokota almasi wewe unaokota mbao I'm flora from Masaki

Anonymous said...

Yesu na Maria wachangiaji wameua sana ingawa Wapo sawa Irene umekwisha mama acha wachapakazi waendelee hukujua wakati wako ukauchezea sasa utafute Ndikumana umtake radhi kipaji kimeishia kwenye bad Scandals na uchafu wa kubadilisha wanaume mashabiki wako wakiwekewa wewe na kuku naamini watachagua kuku uncle ray huku gumegume la kazi gani

Anonymous said...

Nimefurahishwa na comment zilizoenda shule Rj kama hamtaki kusikiliza watanzania tunataka nini mtatupoteza wote achaneni na hawa makahaba wenye viwango chezeni na filamu na wasanii wenye viwango uwoya umebaki kivuli tafuta kazi nyingine

Anonymous said...

Mamburulaaaa people mmeua sana mpeni moyo Irene anaweza kurudi kwenye chart ingawa mimi mwenyewe salute ni kwa batuli na johari

Anonymous said...

We tabia yko nzuri..mijitu mingine bwanaa toa kwanza boriti kwenye jicho lko ndipo utakapoona kibanzi cha mwenzako...shwain weyt

Anonymous said...

toka nimeanza likizo sijaingia humu nimeanza kazi sasa tutakuwa pamoja, dada irene usipoangalia mwisho wako ndio umefika katika mambo ya kibiashara kuna kitu kinaitwa wakati, kama una duka chunguza mauzo yako yamepanda au yameshuka ukiona umeshuka tizama nyuma ni wapi umekosea comment zote hizi nyingi zinakupinga na wapo waliothubutu kumtukana aliyekuajiri kaka ray. usidharau mashabiki kabisa sisi ndio tunajua tunataka nini mashabikki tunataka kazi nzuri na anaetupa burudani au elimu kupitia filamu awe nae katika maadili sio kazi nzuri tabia mbaya badilika wanaume wana mwisho mbovu daima kazi ndio ngao ya kila mwenye akili nimesikitika kuona hutakiwi na silimia kubwa ya watoa comment jiulize hao unaotajiwa kwenye comment hapo juu wana nini? jibu ni tabia njema hata kama hawana tabia njema uzio waliouwek mbele yaq jamii ndio unaowafanya haweshimike utajuta usipofumbua macho na kukubali wazuri wapo wngi na kila siku wanazaliwa wapya. ni ushauri tu ingawa hata mimi sikukubali kabisa nimekutoa kwenye list ya wasanii wangu niwapendao naitwa Mr Zablon kutoka Arusha

Anonymous said...

hii movie utauza kwa sababu ya johari na wewe mwenyewe huyo aliyebomoa ndoa yake kapoteza muelekeo.

Anonymous said...

nimeitafuta trailer ya hii muvi mpaka nikaiona hii inatokana na jinsi watu alivyoishambulia kimsingi sijaona kosa kuuubwa sema the cover of that muvi liko soooo offensive yaani irene uwoya japo kacheza ndani kama sista aliyelazimishwa usista so akawa anafanya vitu ambavyo ni nje ya utaratibu wa kanisa lakini kwenye kava Ray umevuka mpaka sista hawezi kuvaa kimini ndani ya gauni hata awe amepitiliza ufuska kiasi gani trust me kwanza huruhusiwi kuwa na nguo kama hiyo hata andasket zao huwa ni ndeeefu zinapishana kidogo na gauni nakwambia hivyo coz mimi nawafahamu vizuri nimesoma sekondari shule ya masista tulikuwa mpaka tunakaguliwa hadi andasket ikiwa fupi ni adhabu pia kiatu hamna shirika la kitawa litakaloachia sista avae kiatu kama kile huwezi katisha nacho kokote pia irene anaonekana amechonga nyusi ktk mazingira ya kitawa mtu wa hivyo lazma afukuzwe jamani RAY jiulize kwann watu hata hawajaona muvi lakini wamekujaji vibaya tatizo ni kava kama unataka kava liwe vile basi jina la muvi ungebadili kidogo eg sista mary against the church or au sista mary the wrong nun hayo yangefuta utata woote Ray natumaini uliiona ile muvi ya cross of my sin aliyoicheza swahiba wako ambapo ndani anaonekana padri akilala na sista
muvi ile haikusemwa coz title inaonesha kile kinachoonekana ndani ya muvi ni dhambi nilikusikia kwenye mkasi ukisema umetumia pesa nyingi so nakushauri badili jina la muvi