Saturday, February 4, 2012

BONGO MOVIE NDANI YA TMES FM

 Bongo Movie club juzi kati waliivamia Redio ya Time Fm na kufanya shoo ya nguvu sana watangazaji wetu walikuwa Masanja Mkandamizaji pamoja Steve Nyerere,Dhumuni lilikuwa ni kuwachangisha wadau wakubwa wa tasnia ya movie kwa ajili ya wenzetu waliopatwa na mafuriko makubwa pale Jangwani,tuliguswa sana na maafa hayo na ndio maana tukasukumwa kufanya jambo ilo kwani watu wengi wanaonunua kazi zetu ni watu wa hali chini sana kwa asilimia 70 kama sikosei,Sasa ni jukumu letu sisi kwarudisha shukrani zetu dhati kwa kujitolea kufanaya tukio ilo pia leo usikose kuja pale Uwanja mpya wa Taifa kuna mechi kali kati ya Bongo movie na Wanamuziki wa Dance kiingilio ni shilingi alfu mbili tu pesa zote zitazopatikana zitaenda kwa ndugu zetu waliopatwa na maafa hayo

 Masanja akiwa kazini kuendesha zoezi ilo kulia Mkoloni mwanamuziki wa kizazi kipya kma mnakumbuka walikuwa na kundi lililokuwa likiitwa Wagosi wa Kaya

 Mainda na Steve Nyerere

 Mambo yakiendelea.....

 Chopa Mchopanga naye alikuwepo katika zoezi ilo

 Davina mrembo wa Bongo Movie

 Mainda mwanadada machachari katika fani ya uigizizaji, Yeye ni mwanakamati mkuu katika swala zima la ushagiliaji pale Uwanja wa Taifa ni sipakukosa

 Wanabongo Movie wakiwepo ndani ya mjengo wa Times Fm 

 Dada Heriety Chumila mwanabongo movie, Yeye pia alipatwa na mafuriko na kupoteza kila kitu na kuanza upya naye alikuwepo kuwawakilisha wanzake wote waliopatwa na janga ilo

Karibu Uwanja wa Taifa kuona mechi kali .

3 comments:

Anonymous said...

mainda mdogo wangu huo ni mkorogo au ni manake huo uso unavyotisha pole we uzuri hauonekani mpaka ujichubue ona sasa unavyoonekana kam kinyago cha mpapure

Anonymous said...

hongera kaka yake kanumba ila huo mkorogo na kitambi kazi ipo

Anonymous said...

RAY WEWE NI MSANII KIOO CHA CHA JAMII,MNAVYOPARK BARABARANI AU KUKAA,NI KUTAFUTA UMAARUFU AU?BE CAREFUL ONE DAY U WILL REGRET,