Thursday, April 12, 2012

POLE MAMA STEVEN KANUMBA

 Muda ulifika wa Mama Kanumba kuwasili uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere maana wakati mauti yanamfika mwanae alikuwa safarini Bukoba.Mama yangu mzazi(mwenye nguo nyeupe) ndiye aliyeongoza msafara wa kwenda kumpokea Mama Kanumba

 Kamati ya mapokezi ikimsubiri Mama Kanumba kuwasili.

 Muda ulifika na Mama akawasili na majonzi yakatawala.

Kilio na simanzi vilitawala uwanjani hapo(kulia) ndiye Mama yangu mzazi, Mama Mary Kigosi akimsaidia rafiki yake.

 Pole sana Mama kwa msiba mkubwa uliokupata ninakuwaidi nitakuwa pamoja nawe kwenye shida na raha

Mama alishindwa kabisa kuzuia hisia zake mpaka kuzimia.

 Njiani kuelekea msibani.

 Tukimsubiri Mama mzazi wa Marehemu Kanumba.

Baada ya kufika nikaenda kumpa pole,alilia sana aliponiona na kuniambia pacha wako mwanangu yuko wapi umebaki peke yako? Niliumia sana.

 Mazungumzo yakaendelea.

Akiliaa kwa uchungu mkubwa sana. Pole mama.

 Kesho yake nikaenda kutafuta jeneza la kumzikia ndugu yetu mpendwa.

Hili ndilo jeneza aliozikiwa Marehemu Steven Kanumba.

 Baada ya kutoka kwenye majeneza nikaenda kuwachukua maskali kwa ajili ya postmortem

 Tukiendelea kusubiria.

Nikiwa nimeshamaliza hatua zote.

52 comments:

Anonymous said...

RAY POLE DUUU UMEJIKAZA SANA UTAKUWA UNAMLIZA HUYO MAMA KILA SIKU TUOMBA UJITAHIDI KUWEKA PENGO KWA MAMA KIDOGO ITASAIDIA POLE NDUGU YANGU.

Anonymous said...

POLE SANA RAY

Anonymous said...

Ray nimekutumia msg facebook usipublish kwasababu ni personal msg yako na johari plssssss just for the seek of me marry her,nampenda johari ni mke siunaona hawawanawake wengine ni wasumbufu tu plsssss do it fo me as ur big fan u have my facebook name siku ikiwa hivyo pls invite me and i will contribute the little i will manage.nataka ubadilishe maisha kwa mtazamo tofauti ukiwa mume heshima inabadilika na sasa hivi taifa limetambua umuhimu wa wasaniii kwa ndio nchi wanaweza kugeuza nchi kabisa.kanumba wil be so proud of u bro

Anonymous said...

POLE SANA KAKA RAY MUNGU AKUZIDISHIE KWA YOTE ULIO MTENDEA NDUNGU YAKO KANUNUMBA LAKINI NDUNGU YANGU BADILIKA WEWE SIO KAMA MAREHEMU UNAMAJIDAI SANA JAPO TUNAPENDA KAZI ZAKO LAKINI HUNA MAPENZI NA SIE KAMA ALIVYO KANUMBA SIUMEONA JINSI KANUMBA ALIVYO ZIKWA NA WATU NI KWA AJILI YA ROHOYAKE YA KUSAIDIA WATU NA UPENDO ALIOKUWA NAOKWA WATU

Anonymous said...

Pole saana tena saana kaka Ray. Mwenyezi mungu atujalie subira na nguvu ktk kipindi hiki kigumu. Mipangi ya mungu haina makosa muhimu ni kuwa waja wema na tuombeane kwa mungu na kupendana kwa dhati. R.I.P Kanumba.

Anonymous said...

pole sana ray ni hakika hatujui unajisikiaje sasa hivi kwa kanumba kuondoka Mungu yeye anayajua yaliyoko mioyoni mwetu,pole kaka.

Anonymous said...

POLE BRO those are challenges that human beings faces bt b storng iknw people will talk more kama u were are a good friend ull alwayas b my brother

Anonymous said...

pole sana Ray, mimi nikiangalia tu hizi picha nalia tu lakini wala simjui kanumba wala sijawahi kuona movie zake ila, ameondoka bado kijana sana na taifa linamwitaji, kama marafiki zake pia msimwache LULU kwa sasa hamjui kilichotokea RIP KANUMBA

Anonymous said...

RAY MBONA SIJAONA NI JINSI GANI UMEUMIA KUHUSU KIFO CHA KANUMBA?KWANZA MUDA WOTE UMEVAA TU MIWANI HATA SIJAKUELEWA, NA JE NI KWELI WE NA KANUMBA MLIKUWA NA UGOMVI?ANYWAY POLE SANA RAFIKI YANGU MIMI BINAFSI NIMEUMIA SANA SANA TULIMPENDA SANA KANUMBA ILA MUNGU KAMPENDA ZAIDI, REST IN PEACE KANUMBA

Anonymous said...

SASA UNA MAMA WAWILI... HAKIKISHA UNAFANYA HIVYO MPAKA MWISHO WA UHAI WAKO NA KAMA AKIRUDI BUKOBA UWE UNAENADA KUMSALIMIA.
nacho kusifu HUJIBISHANI NA MTU KWENYE BLOG WW UNASOMA COMMENT NA KUFANYA KILE UNACHOKIONA NI SAHIHI
huwezi kuridhisha kila mtu..
watu wanaweza kuponda kuwa urifurahi kwenda kununua jeneza ili umtoe haraka dunia.... watu jamani.
ALAFU SAMAHANI RAY,, nimeona picha za mama kanumba alizoenda makaburi leo(millard ayo),, sijamuona mama yako kwani mama yako kaisha ondoka msibani inabidi awem naye karibu maaana inawapasa waitane mtu na dada. ampe kampani yakutosha. wakibaki na wanae du HATARI
emmer matutu

Anonymous said...

Endeleo kuonyesha upendo kwa mama kanumba.na endelea kumuenzi swahiba wako kwa kuhakikisha kazi zake zinatoka alizoanza.na kampuni yake.pia uwe unamtembelea pale makaburin kndoni.

Anonymous said...

kweli msiba huu umetuumiza wote.... sijui sinema zake alizoacha kama watu watamfanyia unyama au watakuwa waukweli....

Pumziko la milele umpe eeeh bwana...

Kanumba the great

Anonymous said...

wewe Ray ni mnafiki,kilichokufanya uwe kimbelembele hivyo ni nini?inajulikana kabisa haukuwa vizuri na marehemu,sasa kilichokuwa kinakushughulisha hivyo ni nini jamani?naomba kama hujausikiliza mwimbo wa marehemu basi nenda kausikilize,ile msg ilikuwa yako na hao wajinga wenzio hukutakiwa hata kusogelea jeneza la marehemu,hivi ingetokea pale aamke na kukuambia usibebe jeneza lake ungesemaje?shame on u you are time is running out so watch out.

Anonymous said...

hata usipoiweka utakuwa umeisoma kimya kimya kauzu wewe.

Anonymous said...

Mungu ndie anajua unachomuwazia swahiba wako ni vema kama mlkuwa mmemalza tofauti zenu!Au lah!!!!!Ila maisha n kama gwaride kaka yangu pambana ila jua kuna leo na kesho ametangulia Kanumba sote tu nyuma ake its better ukajipanga ili kuswe na utata kama uliopo now!!!!!!!!!!!!!!

Anonymous said...

Laiti 2ngekuwa 2meumbwa kwa vioo au sightmirror 2ngeona yale wenzetu wanatuwazia dah niliipenda hii ila ndo hivyo man unajua unachomuwazia Marehemu swahiba wako cha kufanya mkumbuke ktk sala zako uombe msamaha pale mliposhndwana I believe Mungu atakuskia!!!!!!!!!keep it up Ray

Anonymous said...

wanaadamu tuache kuhukumu,pole sana ray

Anonymous said...

RIP Kanumba wl olways remember you!!!!!!Ray please jitahidi katika kazi kazo na umwombe na kumwamini Mungu aliye hai ndo kimbilio letu wanadamu,wengine hao sio kabiiiiiiiisa!!!!!!!

Anonymous said...

Sasa jamani Ray anatukanwa kwanini? Kanumba alisisitiza upendo hivyo basi ingekuwa vyema kama tungemuenzi kwa kuonyesha upendo kati yetu. Just leave Ray alone people, if u dnt have anything nice to say then just dont.

Anonymous said...

Kwa nini ulijiita THE GREATEST baada ya kuona kanumba anajiita THE GREAT.....?

Hilda canada. said...

Nimefurahi kumwona mama yako akimfariji mama wa kanumba huo ni upendo wa dhati.Mi bado sijaelewa kuna watu wanasema huna majonzi eti umevaa vizuri na miwani jamani tuache kumnyima amani huyu kijana ina maana alitakiwa abebwe ndo uchungu uonekane?Kuwa smart siyo dhambi jamani ila uchafu ni dhambi.Wote mlioko huko na sisi tulio mbali wote tulipata huzuni kwa kuondokewa na kijana mwenzetu akiwa bado na ndoto zake nyingi. bado mdogo. Ni vizuri tutiane moyo kwani nani anajua saa yake ya kuondoka?

judy canada said...

Nikupe pole na nikusifu kwa kujikaza na kujishughulisha kwa ajili ya mpendwa wetu Kanumba. Kujitoa kwenye msiba sio ili watu wakuone ila unajikuta unajishughulisha kwa ajili ya mapenzi na upendo kwa aliyeondoka.Siyo kwamba ukishughulika sana huna majonzi la ila kama una nguvu ni vizuri kujitahidi na ndivyo ulivyofanya. Huo ni upendo pia kwa wafiwa najua ukifiwa unakosa nguvu so isingekuwa vizuri wadoge zake wakatafute jeneza na nyie marafiki mpo.Tusiwe wahukumu tukumbuke pamoja na mapenzi makubwa tuliyokuwa nayo kwa kanumba hakuna mtu angekubali azikwe kaburi moja na yeye. Wote tungekimbia kama tulitakiwa kuonyesha huzuni kwa kuzikwa pamoja.Tufarijiane. upendano husitiri wingi wa dhambi.

canada said...

Hili ombi ni kuhusu hao dada zenu wa bongo movie.Wekeni wazi mambo yenu aliye na mchumba amweke wazi kabla haujaja mda yatajianika wazi kwa njia isiyo nzuri. Nyinyi wote ni watu wazima kwa nini mnafichaficha mahusiano yenu kama watoto wa shule ambao wanaogopa baba asijue? Jengeni heshima kwa jamii kwani kuna watu wanawapenda na kufurahia mafanikio yenu. Baadhi ya dada huko bongo movie hata ukiwapa Hi anakausha kisa s tar hao mnaowakaushia mtaani mkipata matatizo makubwa si ndiyo hiyo hiyo jamii mnaiomba msaada??Msichague uso wa kupokea salam Mtu anapokupa salamu hakuombi hela wala hupungukiwi na kitu, heshima haiuzwi.Hujui ni tatizo gani litalokufanya uombe msaada kwa hao hao ambao si star inaweza kuwa ugonjwa au case mbaya unajikuta kuna watu wangeweza kukusaidia ila kwa sababu ulionyesha dharau na kiburi wanauchuna tu.

Anonymous said...

watanzania mna maneno, eti ule wimbo wa KANUMBA ALIMTUNGIA RAY je wasingetofautiana na RAY HUO WIMBO MNGESEMA WA NAN? ME NADHANI HAWAKUWA NA BIFU LA KIHIVYO KM MAELEWANO HAYAKUWEPO BAS N YA KIBINADAMU TU KM MNAKUMBUKA KUNA GAZETI LILITOKA RAY AKIMSHAUR KANUMBA AMALIZE TOFAUT NA BABA YAKE, LIKATOKA TENA GAZETI LIKASEMA KANUMBA AMESEMA "RAY UNANITAFUTA UTANIPATA" LKN BAADA YA HAPO KANUMBA ALICHUKUA LILE GAZETI AKAWEKA KWNYE BLOG YAKE AKASEMA YY KANUMBA HAJASEMA HAYO MANENO SS HAMUON KM HAKUKUWA NA UGOMVI MKUBWA KIIVYO NA NDO MANA KANUMBA ALIKANUSHA YALE MANENOO EM KUWENI NA AKILI BWANA INGIENI KWNY BLOG YA KANUMBA MKAANGALIE KWNY OLDER POST MTAELEWA NNACHOMANISHA, muacheni RAY WA WATU HATA KM HAMUMPEND TUPO TUNAOMPENDA NA BNADAM ALOKAMILIKA HAWEZI KUPENDWA NA WATU WOTE AU KUCHUKIWA NA WATU WOTE.

Anonymous said...

Nimekupenda sana Ray, wewe ni msanii, kwa jinsi ulivyopangilia story ya Kanumba kwenye blog yako inaonyesha ni jinsi gani ulivyo msanii, umeanzia mwisho kuja mwanzo. Waandishi wengi wa vitabu kutoka Nigeria wanapenda kuandika kwa mtindo huo. Nimegundua kitu, kuwa wewe na Kanumba hamkuwa marafiki tu bali ni NDUGU kabisa, kama urafiki wenu ulifikia hata mpaka wazazi nao ni marafiki jamani. Big up sana Ray.Hivi Watanzania mnataka Ray afanye nini ili mjue kuwa aliumia sana na msiba huu?? Vumilia tu kwa sasa kwa kuwa binadamu ndivyo tulivyo, ni wanafki kuliko unavyofikiria, hata kwenye msiba wa Kanumba, najua ni wengi wangeumbuka kama Kanumba angeamka japo kwa dakika 5 tu. Unakumbuka ile redio iliyomtengenezea matangazo ya kumuaibisha kuwa aliongea kingereza kibovu alivyoenda Big Brother? uliona jinsi walivyokuja kuwa wanafki eti siku nzima ya mazishi yake hawakuwa na vipindi vyovyote zaidi ya kutangaza kuhusu Marehemu Kanumba. Kuwa na bidii siku zote na usiwasikilize watu, sisi binadamu ni wanafki sana. Mi napenda kukutia moyo usiangalie nyuma tenda wema uende zako, endeleza tasnia, utafika mbali.
RIP Kanumba.

Ni mimi mpenda maendeleo yako
Mzalendo halisi.

Anonymous said...

kukosolewa kupo tu hakuna mkamilifu ukifanya vibaya hata kama ni kipenzi cha watu unasemwa tu haimaanishi wanakuchukia ni kukurekebisha magazeti ya global publishers yamemsema vibaya sana tu lakini mmiliki alikuwa kwenye mazishi ray ulimsema vibaya na ulikuwepo kwenye mazishi kusemwa haina maana ukifa wasikulilie please

Anonymous said...

Poleni sana kwa msiba wa rafiki yako . Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema Astarehe kwa Amani.
Kifo binadamu tumeandikiwa hatujui siku wala saa ni kujiweka tayari katika muda unaofaa na usiofaa. Kanumba kaenda ni huzuni kumbwa sana kijana mdogo. bado mimi nayeandika hapa na sisi wote tuliobaki duniani hatujui siku wala saa. Na mwenyezi Mungu kapanga kila mtu kifo chake kitakavyokuwepo. Japo mara nyingi vinatokea vifo vingine ambapo kwa binadamu ni utata mkubwa sana. Inabidi tukubali ni Mapenzi ya Mungu.


Kuna jamaa mmoja hapo juu katukana sana

Alichokifanya Ray kushiriki kikamilishi na mazishi ya Rafiki yake ni vizuri sana hata kama walikuwa na utofauti wao. Naamini hata ingekuwa mauti yamekufikia wewe na kanumba yupo hai basi angefanya kama ulivyofanya Ray.

Sawa mlikuwa na tofauti zenu lakini kuna mambo mengi sana sana mazuri mmefanya pamoja. binadamu hatupaswi kupima mzani kwa kuangalia kiwango kidogo cha mabaya na kusahau mazuri.

Mfano mzuri sana Ray nje kununua vitu na Kanumba alipita mbele na kumpokelea Tuzo lake japo walikuwa na hitilafu.

Kitu kingine kwa watu wasio jua. Kanumba alitengeneza Cd ambayo alikuwa na nyimbo tofauti pamoja na ule wimbo nainua macho yangu. Zile nyimbo ndugu wa karibu na Kanumba wanazo muda mrefu kabla hata hii Itilafu ndogo imetokea baina ya Ray na Kanumba. Watu wengi sana wanazani ule wimbo ndo kwanza kauimba hivi karibuni jibu lake sio kweli.

Mara zote tusipende kupima mabaya machache tuangalie kwa mema mengi ambayo watu wamefanyiani. jambo moja baya lisifute mema mengi.

Ray ulifanya vizuri sana Mwenyezi Mungu akubaliki akupe nguvu za kuweza kupita hiki kipindi kigumu sana Mengi yatasemwa.

Anonymous said...

PolE saN Ray mimi binafsi nawashangaa watu wanaotoa comments za ajabu nyie hamjui vizuri Ray na Marehemu kanumba walikuwa marafiki sana ila tu sisi binadamu tusiopenda maendeleo ndio tunazusha mambo ya uongo Ray Acha nao songa mbele pole sana mdogo wangu Usikatte tamaa Mungu yupo pamoja nawe

Anonymous said...

Ewe Mwenyewezi Mungu mlaze mahara pema mpendwa wetu Kanumba.

Mwenyezi Mungu ana uwezo mkubwa sana najua wengi wetu tunaona ameonewa hakustahiri kufa mdogo vile. Mwenyezi Mungu ana uweze wa kuepusha baadhi ya vifo ndo maana tunakuta ndege imedondoka watu wote wamekufa lakini mmoja anatoka mzima.Inakuwaje siku yake inakuwa haijafika. Au wachawi wanafanya kila juhudi za kumuua mtu wakati mwingine mwenyezi mungu anawaacha tu wafanya na wakati mwingine anaepusha hata wafanyeje mtu afi kwa maana siku ambaye muumba amemwandikia kiumbe wake haikufika. Katika ndoa kuna maogomvi kila siku kuna baadhi wanapigana lakini hawaishii kwenye mauti. siku yako ambayo muumba amekuandikia ikifika unaweza ukajikwaa ukadondoka na kufa. unaweza ukawa umekaa kwenye kiti na ukafa hapo hapo au usingizini.
na Mtu anakufa . Ebu fikilieni hivi taarifa nyingi ambazo zipo Lulu alimsukuma Kanumba kadondoka kafa. Jamani tukienda kwenye maisha ya kanumba. Kanumba alikuwa ni mtu wa mazoezi mwili wenye maguvu mtoto wa kiume hivi kweli Lulu anaweza akamsukuma Kanumba akadondoka kama haikuandika kwenye kifo chake kwamba Kanumba atakufa kifo cha vile. Jamani watu wanadondoka kutoka ghorofa juu mpaka chini kwenye sakafu ngumu mbona wengi wanapona kwanini siku zao zinakuwa hazijafika. watoto mara nyingi sana wanadondoka kwenye ngazi wanajipigiza kichwa lakini hawafi kwamaana siku zao zinakuwa hazijafika.

Tulimpenda sana na tulipenda awe pale siku zote lakini ndo hivyo Mwenyezi mungu Kampenda zaidi.

Kila binadamu ameandikiwa atakufa kifo cha namna gani tujiweke tu tayari. Kanumba katangulia sisi hatuju lini itatokea. Tunaishi leo hatujui kitu gani kitatokea kwenye maisha yetu dakika zijazo. Ukiamka Asubuhi unamshukuru Mwenyezi Mungu. Ukiipita siku nzima salama unamshukuru Mungu.

Anonymous said...

ki ukweli baada ya kanumbu kufariki... watu wanamchafua RAY kwa kasi sana... hata baadhi ya watangazaji i.e ZAMARADI..
du RAY una kazi ya ziada
msiba.. ngoja msiba uishe afu nitashauri kwa upande wangu nini ufanye... mapema sana kwa sasa.
emmer.

Anonymous said...

hata mimi kwa kweli nimempenda sana RAY alivyo handle the whole issue. kutofautiana kupo mtu utatofautiana na mzazi wako sembuse rafiki?? hata kama kulikuwa na tofauti haimainishi ndo alimwombea kifo. nyie waleta chuki zenu hapa hebu acheni yenu majungu, hata shetani anayewasukuma ataona kabisa mna over do...let it go. halafu ni wazi always media ndo wanakuza mambo. kama kweli kungekuwa na bifu la kutoana roho mama yake marehemu asingemfurahia Ray..na wala mama Ray asingekubali kumpokea mwenzie na kumfariji..so mshindwe na mlegee..ndo nyie mnapenda kuendeleza mabifu hata kama wahusika wameshamaliza tofauti zao. ushabiki wenu leteni kwenye mambo ya kheri. RIP Steven, and Ray hongera kwa ujasiri. Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigum na njia pekee ni kufuata nyayo zake na zaidi, si umeona alivyozikwa? he was man of the people, fanyeni kazi ili Tanzania isipotee katika ramani ya movie, kwani kanumba alijitahidi na kazi alishaanza, inabidi muendeleze..ni hayo tu. DOREEN.

LEONA said...

HATA UNGETANGULIA WEWE PIA WATU WANGEMSAKAMA KANUMBA,LKN USIJALI WANADAMU KUONGEA NI KAZI YETU,MUNGU ATAKUPA WEPESI KTK KIPINDI HIKI,JIPE MOYO RAY UTASHINDA NA KUWASHIKA,MANENO NI KM NGUVU YA SODA UIFUNGUAPO,POLE RAY

Anonymous said...

mh jamani yameongelewa mengi ila tu kk yng ray km alivosema mmjaalopita so kwamba wanakuchukia ila huna mapenzi na mashabiki wako km aluvokuwa marehem, hupendi kuwaendeleza au kuwaibua wengine km yy,hujitumi kisanii,hupendi kujiendeleza kielimu, ss km mlobaki mkiishia hapa bongo nani atatutangaza nje huko. hivihamuoni wivu kanumba alivopendwa na kujulikana? inabidi ubadilike la sivyo hautafika popote. itabaki story ya kanumba tu mpaka kesho. by the way thanks for everthing kwa kanumba wetu alokuwa mpenda watu aso na makuu na majivuno. hakuna atakaye liziba pengo lake labda miaka mingine ijayo.

Anonymous said...

RIP KANUMBA.Ray,kama kweli kanumba alikuwa swahiba wako,tutayaona hayo kwa jinsi utakavyomjali na kumthamini mama yake.Mpe faraja mama huyo na mungu atkuzidishia.Punguza mashauzi na uwajali watu kama alivyofanya kanumba na mabadiliko utayaona.Mungu akutangulie.
Mrs.Temba

Anonymous said...

Ray hujajibu kwa nini ulijiita The Greatest baada ya Kanumba kujiita The Great????!

Anonymous said...

ray alikua anashindana na kanumba.alitaka aonekane yuko juu zaid ya kanumba kitu ambacho kisingekae kiwezekane.ndo nini sasa kujiita the greatest baada ya kanumba kujiita the great?

Anonymous said...

jamani awe na mapenzi na mashabiki wake awabebe mgongoni ama?? heeeeeeeeeeish achani mambo ya uongo jamani. hebu tuwe na mawazo chanya. haya mara ana chuki, mara anajigonga kwenye msiba, mlitaka afanye nini?? mbona mnamjazia chuki za uongo watanzania?? tujaribu kuwa wakweli hata mara moja. Ray kaza buti haya ni maneno ya wakosaji tu. wanaokuponda wasamehe kwa kuwa hawajui watendalo.

Ni mimi Mzalendo Halisi

Latifa said...

Brother ray Pole sana kakaangu najua umetenda wema na huwezi kumridhisha kila mtu hapa dunian wapo waliokuona umefanya jambo jema na wapo waliokuona una kimbele mbele ila Munugu ndio anaejua wewe kama wewe unafanya nini jikaze sana na hayo maneno ya watu soma yenye kuzingatiwa zingatia yenye kupuuzia puuzia, ila kwa mimi Latifa nakusifu sana pia naunga mkono haya maneno kuna mtu ametoa comment

SASA UNA MAMA WAWILI... HAKIKISHA UNAFANYA HIVYO MPAKA MWISHO WA UHAI WAKO NA KAMA AKIRUDI BUKOBA UWE UNAENADA KUMSALIMIA.
nacho kusifu HUJIBISHANI NA MTU KWENYE BLOG WW UNASOMA COMMENT NA KUFANYA KILE UNACHOKIONA NI SAHIHI
huwezi kuridhisha kila mtu..
watu wanaweza kuponda kuwa urifurahi kwenda kununua jeneza ili umtoe haraka dunia.... watu jamani.
ALAFU SAMAHANI RAY,, nimeona picha za mama kanumba alizoenda makaburi leo(millard ayo),, sijamuona mama yako kwani mama yako kaisha ondoka msibani inabidi awem naye karibu maaana inawapasa waitane mtu na dada. ampe kampani yakutosha. wakibaki na wanae du HATARI
emmer matutu

Reginald Mwemezi a.ka. Man united. said...

HONGERA RAY KWA NAMNA ULIVYOSHUGHULIKIA MSIBA WA MAREHEMU..................................................MIMI NI SHABIKI NAMBA MOJA WA THE GREAT..... LAKINI WEWE PIA NILIKUWA NAZIKUBALI SANA KAZI ZAKO.......
ILA KWA USHAURI JARIBU KULENGA SOKO LA FILAMU KIMATAIFA HALAFU BADILISHA HATA IDEA ZA MAPENZI UGUSE KILA JAMBO KAMA ALIVYOKUWA MAREHEMU.....NAAMINI MUNGU ATAKUSAIDIA.....KEEP COOL....AND DO YOUR BESTS IN BONGO MOVIES................

Anonymous said...

WE RAY HATA HAYA UNA KTK MSIBA HATA CHOZI HALIJAONEKANA KAZI ILIKUWA KUUZA SURA NA KIMBELEMBELE PINDI ULIPONA WAKUBWA KUJA KUTOA POLE ILI NAWE UWEZE KUONEKANA VIZURI ILA TAMBUA NAFSI YAKO INAKUSUTA KWA KILE KIBAYA ULICHOKUWA UNAMSEMA MAREHEMU SASA UKUMBI NI WAKO NAKUSHAURI UENDE ENGLISH KOZI ILI UPATE WALAU ROBO KUMFIKIA ALIPOACHA MAREHEMU VINGINEVYO UTAENDELEA KURUDIA RUDIA TAMTHILIA ZAKO NA SIYO FILAMU KWANI BADO UWEZO WAKO NI MDOGO KWA SOKO LA KIMATAIFA HUO NI USHAURI WANGU KAMA UNATAKA KUENDELEA KUGOMBANA NA WAHINDI AU KATIKA SOKO LA KIMATAIFA NENDA SHULE UWEZO WAKO NI MDOGO!

Anonymous said...

Pole sana Ray!May Kanumba's soul rest in perfect peace.May God keep u strong throughout this period of agony.

THE GREATEST FUTURE WIFE said...

KWA SASA BABE WANGU HAWEZI KUJIBU COMMENTS ILA NAOMBA NIMJIBIE, ALIJIITA THE GREATEST B'CAUSE HE IS THE GREATEST, NADHANI HUA UNAANGALIA MOVIE ZAKE ZINAONYESHA WHY HE IS THE GREATEST, ANATUNGA ANAACT ANADIRECT, DONT YOU THINK HE DESERVES THAT NAME??? NAOMBA UENDELEE KUANGALIA FILAMU ZAKE, TUNAWAPENDA FANS WOTE WA BABE WANGU. ASANTE

Anonymous said...

Ray kuna mdau mmoja amesema maneno mazito plse chukua hatua nawe utazidi barikiwa nanukuu
''SASA UNA MAMA WAWILI... HAKIKISHA UNAFANYA HIVYO MPAKA MWISHO WA UHAI WAKO NA KAMA AKIRUDI BUKOBA UWE UNAENADA KUMSALIMIA.
nacho kusifu HUJIBISHANI NA MTU KWENYE BLOG WW UNASOMA COMMENT NA KUFANYA KILE UNACHOKIONA NI SAHIHI
huwezi kuridhisha kila mtu..
watu wanaweza kuponda kuwa urifurahi kwenda kununua jeneza ili umtoe haraka dunia.... watu jamani.
ALAFU SAMAHANI RAY,, nimeona picha za mama kanumba alizoenda makaburi leo(millard ayo),, sijamuona mama yako kwani mama yako kaisha ondoka msibani inabidi awem naye karibu maaana inawapasa waitane mtu na dada. ampe kampani yakutosha.''

Anonymous said...

Hello Ray, mimi si msanii bali ni mwanasheria, napenda sana kazi zako, nikifika kununua mikanda huwa napenda mikanda yako na ya Kanumba (Mungu amrehemu). Nimekuwa nikiambiwa kuwa tunafanana sana nikiwa hapa Dar hata nikienda Bk likizo, kutokana na hilo nikaona nikuombe tukutane tuwe na kampani maana nafikiri kuna baadhi ya mambo ya kimaisha tunaweza kushare. Email yangu ni katerero73@gmail.com Naomba tuwasililiane.

Anonymous said...

halafu ww unaejiita baby wangu baby wangu nonsense unamuharibia tu bora ukae kimya nyambafu ww unaongea utumbo gani ha umjibie yeye mdomo hana kama huna cha cucoment kaa kimya

Anonymous said...

kuna picha siwezi kuziangalia mara mbili it is so sad kuona THE GREAT ameenda rest in peace Kanumba.

Ray please endelea kushrikana na mama Kanumba nawe utabarkiwa zaidi

Anonymous said...

Kujiita the greatest con kama vbya et 7bu marehm knumbana alikuw anajiita the great,me nahs pia ni7bu ya mapenz tu!hawez ray kufny ushndan nam2 amby ameshafarki,kma 2navyojua ray nakanumba walikuw km kaka na mdgwke so hayo mambo mengne ya bifu cdhn kma yanamaana!ila ushndan wamaendleo nadhan ulikuwepo nahlo nijambo zuri!pia hatuwez kujua hata kma kulikuwa kuna mapungfu madogo madg katka mahusian yao huwenda hata marehemu alikuw anamkwaza sana ray,jambo jema,kuzidi kumwomba mwenyez mungu ampokee marehemu na azd kumpa uwezo ray wakutupa burudan sis watanzania na ujasir kwakufanya kazi yake!tusipende kuwahukumu nakuwatolea wenzetu maneno ya kashfa!huwez jua unavyomsemea ubaya mwenzko unamwngezea baraka ngp!naunajipungzia ngap!hebu watanzani tufunguke!tusipend kuropoka ropoka tu!yan jaman ray kapost vitu vyamaana bdala ya kumsupport mtu anasema alinunua jeneza ili amwahshe kanumba kuzikwa?kwn yey ndo alipanga ratb ya mashz?awe mnafik ili iwaje?ieleweke kanumba na ray nindungu jaman!naunawez kukuta ray ndo kaumia kulik hta ndgu wajiran ukimtoa mamayke!

Anonymous said...

pole sana ray

Anonymous said...

caption zako zimekaa ki SELF PROMO unasahau huwa huo ni msiba. Bado haijaa kaa akilini kama wewe ni mzima kweli kiakili au Kufa Kufaana!! aissssh

Anonymous said...

bwana alimtoa Kanumba na bwana amemtwaa jina lake lihimidiwe...Amina

Anonymous said...

Pumzika kwa amani Kanumba i cant wait to see movies alizoziacha zitatoka liniiiiii

Anonymous said...

Endelea na kazi zako Ray usisikilize ya wanadamu, ni wewe na Mungu wako tu ndio mnaoujua ukweli wote, kazi ya Mungu haina makosa, na malipo ni hapa hapa duniani. Achana na maneno ya wazushi a.k.a wanok nok