Wednesday, April 11, 2012

PUMZIKA KWA AMANI STEVEN KANUMBA THE GREAT Majonzi makubwa kwa Watanznia wote kuondokewa na mwenzetu katika tasnia hii Mungu ailaze roho ya marehemu peponi amina nitakukumbuka sana ndugu yangu kwani tumefanya mengi mimi na wewe mpaka kuifikisha hapa hii tasnia nitakuenzi kwa kufanya kazi nzuri na kuyaendeleza yale uliyoyaacha sisi tulikupenda ila Mungu kampenda zaidi  pia nawaomba radhi wadau kwa kuchelewa kupost nilikuwa nimebanwa sana na msiba maana nilikuwa kwenye kamati ya mazishi

 Viongozi mbalimbali wa serikali waliudhuria Mrema wa kati akiingia ni mbunge wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na alishawahi kuwa waziri wa mambo ya ndani


 Waeshimiwa wakiteta jambo

 Kitabu cha kumbukumbu na picha ya marehemu


 Waziri wa ofisi ya Rais na mausiano Mueshimiwa Steven Wasira akindiaka ujumbe wake kwenye kitabu cha kumbukumbu 

 Waziri Mkuu Peter Kayanza Pinda akiwasili kwenye msibani kwakweli tunawashukuru sana serikali yetu kwa kuweza kutufariji katika kindi kigumu tulichokuwa nacho kwa sasa mmetutia moyo kwakweli

 Mueshimiwa Zito wa kushoto mbunge wa Kigoma mjini naye alikuwepo tunakushukuru sana ndugu yetu


 Waziri Mkuu akiongea na mwenyekiti wa kamati ya mazishi bwana Gabriel Mtitu aliyevalia nguo nyeusi


 wakiendelea kuteta jambo

 Rais wa nchi mueshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete naye akiwasili

 Naye akifikia kwenye kitabu cha kumbukumbu

 Mambo yakiendeleaa.....


 Hapa akiongea jambo na baadhi ya wanakamati ya mazishi

 Mwenyekiti wa Bongo Movie Jb akiteta jambo na Mueshimiwa Rais

 Tunakushukura sana Rais wetu kwa kuja kutufariji

 The Greatest nikimsikiliza Rais

 Hapa akiondoka uku akiwasalimia Wananchi wake

 Poleni sana hayo ni maneno yake Mueshimiwa Rais

 Baada ya kuondoka Rais tukawa tunateta jambo ambalo lilimchekesha sana mtoto wa Rais Riz One Kkikwete

 The Greatest nikiwa katika maojian na mwandishi wa habari

 Mzee Chilo akiongea jambo na Steve Nyerere

Salama Jabir na Madam Ritha wakiwa kwenye majonzi 

Dulla wa Planet Bongo na Salama Jabir

76 comments:

Anonymous said...

Usijali Ray kusemwa kupo lakini ukitetereka utajiumiza mwenyewe chamsingi ni kumuomba Mungu akupe moyo katika kipindi hiki kigumu, yatasemwa mengi lakini kuwa imara. Sidhani kama mlikuwa maadui bali mlihitilafiana hata yeye mwenyewe alisema urafiki wenu si kama wazamani lakini hakusema kuwa ni adui yake. Pole kwa kumpoteza rafiki ila iwe funzo kwa tasnia nzima ya Movie jinsi ya kujipanga na kuchapa kazi bora, mapungufu yaliyojitokeza ni kuhakikisha mnajirekebisha haswa mabinti na nyie kaka zao.Mshike Mungu sana hata kuacha

Anonymous said...

NAPENDA SANA HUYU KAKA NA NITAMMISI MPAKA KIFO CHANGU KITAKAPONIFIKA MUNGU AKUREHEMU BABA NA ATUREHEMU NA SISI SIKU YETU ITAKAPOFIKA AMINA.

Anonymous said...

pole sana kaka yangu ray..yote mipango ya mungu haina makosa...nimeumia sana sana yani sina lakusema..ray nakukumbuka sana baada yakupokea huu msiba najua jins gani unaumia kwa kuondokewa na swahiba wako..lkn sie huku denmark tunawapa pole sana kwa msiba wa steven kanumba..mungu akipenda mtaniona muda si mrefu huko kwa kuwapa pole ya msiba huu..najisikia kama nipae lkn siwez unajua tena miji ya watu..mm sina la zaid kaka yangu nakuombea dua njema uko ulipo mungu akupumzishe kwa amäni.ameen.

DADA SANURA
Denmark.

Anonymous said...

its so sad but we cant cry all da time its time for us to pray and make life go on .but my suggetion jamani msimtupe lulu hata mkifika na kumjulia hali itampa faraja onesheni mshikamano wenu kwa huyu aliyebaki hai its me lisa frm arusha

Anonymous said...

Pole saaaana Ray, kama unavyosema huwezi kujisafisha kwa kila mtu ila nafsi na Mungu wako ndo mnajua..just take it easy na pole kwa kumpoteza rafiki yako na mpendwa wetu. Najua kinapotokea kitu cha namna hiyo unatamani kurudisha japo dk moja tu nyuma mpate nafasi ya kuongea na Kanumba, ila kwa sababu haiwezekani tena basi Mungu anajibu maombi..

Anonymous said...

pole sana kaka yangu yote mapenzi ya mungu.
KUHUSU WATU KUKUSEMA VIBAYA NI KWELI...........!!
CHA KUFANYA VUMILIA SANA NI KAWAIDA YA WADAMU KILA MTU ANA MTAZAMO WAKE JUU NA MTU MWINGINE.....
MALIZA MATANGA SALAMA, NA BADAE UFANYE MOVIE ZA INTERNATIONAL NJE YA AFRICA MASHARIKI NDO UTAJENGA JINA LAKO MAANA WAMEONGEA MENGI SANA SIO SIRI INANIUMA SANA ITAFIKIRI NI MIMI NINAYESEMWA... I LOVE YOU..
EMMA MATUTU FROM SAUT MWANZA

Anonymous said...

usiwe na wasiwasi kabisa ray hao wanaoongea wanamatatizo yao wewe na kanumba ni watu mlionzia mbali sana katika fani ya filamu na kutoelewana ni jambo la kawaida katika maisha nakumbuka dr dre alikuwa na urafiki mkubwa sana na Eazy E na baadaye kukatokea mtafaruku mkubwa lakini katika msiba wa Eazy E dr dre alikuwapo katika msiba na baadae akatoa mpaka mwimbo wa kumkumbuka rafiki yake kipenzi Eazy E msiba ni kitu kingine katika maisha nakutakia maisha mazuri na achana nao hao wanaoongea mambo yasiyokuwa na maana mimi mdau kutoka London
hapa
Dr suleiman

Anonymous said...

DU JAMANI MBONA IZO PICHA WATU WANA MAMBO....
WATU WANAMTUTAKANA NA KUMSHUTUMU RAY JUWA KATOA PICHA ZA LULU MBONA UKI CLICK KWENYE OLDERPOST UNAZIONA WATU WANAKUWA KAMA HAWAJUI KUTUMIA BLOG.. PILI AHENI JAMANI KUPAKAZA MANENO MSIO KUWA NAYO UHAKIKA HAYO NDO YATAKAYO WAHUKUMU...
RAY BE STRONG , U HAVE GOT A BIG CHALLENGES BEFORE YOU.. AND IT IS DIFFICULT TO HANDLE THEM. NATAMANI KAMA NINGEKUWA KARIBU NA WEWE NINGEKWAMBIA CHA KUFANYA..
emma matutu..

Anonymous said...

Pole kaka kwa kumpoteza rafiki,Its real pain.Rest in Peace Kanumba.Okhaaaa!

Anonymous said...

wangu yani miaka yote ya kumjua mwenzio ndio hapa umeandika yote?, kweli yasemwayo yapo, usidhani kama ndio utachukua nafasi yake..........

Anonymous said...

jamani watu mnanongwa sasa ulitaka ray aandike nn ?Ray poleni sana na msiba tulimpenda kanumba ila mungu kampenda zaidi nakuombea upate nguvu zaidi iliuweze kufanya kazi zako vizuri na usijali watu watasema ila yataisha tu binadam hawana jema

Anonymous said...

YU WILL BE FOREVER LOVED....REST IN PEACE THE GREAT STEVEN KANUMBA....GONE TOO SOON SO SAD!!

Anonymous said...

Ray mdogo wangu watasema sana ila wewe endelea na kazi yako Muombe sana Mungu akupe nguvu ili uendelee na Maisha yako. mengi yalisema hata kabla ya Kanumba hajafa sembuse sasa ila kuwa na moyo mgumu ndugu yangu. inasikitisha sana tumempoteza ndugu yetu ila kila mtu atapitia njia hiyo hiyo. unakumbuka marehemu walivyosema na alivyosikitika sna. ila alivyotutoka hata wale walimsema walimsifia. wote tuliobado hai yatasema mazuri na mabaya ila tukishatoweka hapa dunia ndipo mengi mazuri yatasemwa. kama marehemu alivyosema tupendane lets do that. your on my prayes. God bless and keep you the way he wishes.

Anonymous said...

pole sana ray najua kwa kisi gani umeumia hata kama mlikaruzana kidogo lazima itakuuma maana kifo kitu kingine kabisa wachana na hawo wanaokunanga haswa huyu changiaji aliyesema namnukuu ktk miaka yote ya kumjua mwenzio ndio hapa umendika yote?mwisho wa kumnukuu yaani minadamu kazi hapa Ray angeandika kwa jinsi gani msiba huu umemgusa wangesema anajikosha kwa ujumla siko ktk Roho ya Ray lakini najua kabisa ameumia sana sana kwa hiyo hata angejieleza naman gani baadhi ya watu ambao hawaachi kupayuka kwa kila jambo kwakuwa mdomo haulipiwi Fat basi mtu anajisemee pasipo kufikiri hamjui mnawaumiza watu wengine miyoyo yao kwa kisi gani Ray najua umeumia sana kwa kumpoteza pacha lako wala mimi sisemi rafiki yako maana alikuwa zaidi ya rafiki na alikuwa zaidi ya ndungu pole sana najuahukufurahia hichi kifo kabisa hata kama mlikaruzana ni kawaida na laiti binadamu ungejua siku mauti yanakuja hakuna mtu anataka kuondoka na kinyongo wala kuwachwa na kinyongo mtu angejua mwenzie anaondoka nafikiri kilammoja angefanya bidii kuelewana na mwenzake lakini kifo ni fumbo kwa kila mwanadamu hakuna ajua zaidi ya Mola wetu Ray usijali piga moyo kondo haya yatapita tu na watu watasahau Mungu akutie nguvu ktk kipindi hichi kigumu kwako

Anonymous said...

Ray una roho mbaya sana, lakini ujuwe wazi kwamba wewe umtoto sana kwenye uigizaji kwa Marehemu Kanumba. Yaani na uswahiba wenu wote mlokuwa nao kabla ya mfarakano, hayo ndo unayoweza kusema tu? We ulijiita the greatest baada ya Kanumba kujiita the great...lakini kamwe hutamfikia hata nusu ya mafanikio yake, nyota yake ilikuwa juu, na itaendelea kuwa juu daiama. We mnafiki sana SIKUPENDI..kwanini hukufa wewe akabaki Kanumba wetu? Lakini wazuri hawadubu, mijitu yenye roho mbaya (kama wewe) ndo inabaki duniani! Hata kanumba asipokuwepo wewe huwezi ku lead film industry ya bongo, sasa nizamu ya JB kung'aa lakini si wewe

Anonymous said...

asante kwa kuwa muelewa kuhusu picha

judy canada said...

yeyote asiye na dhambi na awe wa kwanza kuhukumu. Sidhani kama mlikuwa maadui ila ninachokiona ni ushindani. Na ushindani ni mzuri. Kumbuka ukiwa hai sikuzote siyo wote watakaokupongeza . Kumbuka hao hao wanaokuhukumu ndo walewale walikuwaga wanamsengenya Kanumba kwamba kaliaibisha taifa kwa kutoongea kingereza kizuri. Mara ni bishoo mara malaya.Haohao ndo watakubadilikia wew kwa sababu Kanumba hayupo tena. be strong, there's people care about you so usituangushe tunakuombea

hilda canada said...

The temptation in your life are no different from what others experience. But God will not allow the temptation to be more than you can stand. Trust in God with all your heart . Without God's direction unaweza kukosa hekima katika maamuzi yako.Kubali ushauri,kubali kukosolewa mwambie Mungu kusudi lake litimie ndani ya maisha yako. Mi hunijui ila ninaona mafanikio makubwa ndani ya maisha yako. Usiogope kusemwa walitaka usiende msibani si wangekuita mchawi?? Binadamu sisi hatumsifii mtu wala kumtia moyo hadi aondoke.Take care

Anonymous said...

Binadamu tumeumbwa na vidole vitano unaponyooshea mwenzako kidole kimoja jiangalie vilivyobaki vyote vinamnyooshea nani? Wapendwa tusihukumu kwani sisi hatuna mamlaka hiyo tumwachie mungu na tumwombee mwenzetu Ray aupunake na maneno haya.

Anonymous said...

wwewe unapenda sifa sasa katika picha zoooooote we uliona hizi ndio za maaana, una hulka ya kujigongagonga wewe, umeweka wanasiasa na watu maarufu, eti umemfurahisha sana mtoto wa raisi, hovyooooo, haya mwenzio kafa sijui sasa utamuiga nani, anzisha vya kwako sasa na ubongo wako wa samaki

Anonymous said...

huna lolote mnafki tu,, shame on you na bongo movie wanzako mfyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

kay said...

kila binadam ataonja mauti,na tutaondoka kwa njia aijuae allah,kilichobaki kwa sisi tumrudie muumba wetu.tusitazame ya nyuma,mtasema ukweli aujua muumba,tusahamiane binaadam hatujui ni lini safari zetu.

Anonymous said...

pole sana Ray usikilize ya watu midomo ni mali yao cha muhimu muombe mungu akupe ujasiri ufanye kazi nzuri na kumuenzi rafiki yako. yote nana mwisho binadamu tuliumbiwa kusahau japo jina na sura ya The Great pamoja na kazi zake hatuta sahau.Mungu akupe uvumilivu na moyo wa subira kwa yote yatakayosemwa.

Anonymous said...

Kanumba The Great 4 sure he deserve that name, he was so handsome, charming, kindly so intelligent, we loved u but God has loved u more no way out we gonna miss u man and no one can cover u a place man, we real love u and we will always love u Kanumba!
MAY GOD REST U IN PEACE

Anonymous said...

pole za nini mnazompa huyo ray kwani kafanya nini mpaka mnampa pole acheni unafiki bwana luv u kanumba forever.

Anonymous said...

Poleni sana watanzania wenzangu.Hasa wewe Ray ingawa siwafahamu.Nimepokea kwa mshtuko sana habari hizi.Nilianza kufurahi kuona Tanzania inavyoendelea kisanaa nje na ndani na kuna siku niliona movie ya watanzania kupitia OBE channel.Ray jipe moyo haya yote ni mipango ya mungu.kitu kikubwa muweke mungu mbele kwa kila jambo.Mwangalie mungu maadui ni wengi.Mungu ibariki Africa.

Anonymous said...

RAY,kama wadau waliopita walivyosema.. u just be strong man usisikilize maneno ya watu utapata pressure ni kweli kanumba alisema kua hamkua marafiki kama mwanzo lakini yameshapita so jipe moyo sana sana sana...

Anonymous said...

Ray poleni sana na msiba, ila usijali maneno ya watu, watasema sana lakini badae watakusifia wakati ukiwa kwenye jeneza, haitakuwa na tofauti kama Marehemu Kanumba kipindi cha BBA, so songa mbele na mambo yako. Mungu akuongoze!

Anonymous said...

embu nyie mnaomtukana RAY acheni ujinga wenu ss km HAMUMPENDI HUMU MMEINGIA KUFANYA NINI? KWANI RAY NDO KAMUUA KANUMBA ANAESHUKIWA YUPO HUKO SEGEREA RAY KOSA LAKE LIKO WAP? AU USHINDANI ULOKUWEPO KATI YAKE NA KANUMBA? ME NAWAPENDA WOTE RAY NA KANUMBA NA HATA KPND TUNACKIA WANAZOZANA NLICOMMENT HUMU KUWA WAJTAHD WAPATANE KWAN WALIKUWA WAKPENDEZA SN KUWA PAMOJA KLA SHM PIA HAMNA HAJA YA KUONEANA WIVU KWAN KLA M2 ANA RIZIKI YAKE, RAY WALA USIWASIKILIZE TUPA KULEEEEE, NA WALA SIO LAZIMA AKA ACT NA WATU WA NJE ILI IWEJE??? WHATS MATTER N KWAMBA ANAFANYA KAZI ZAKE HAPA HAPA TZ NA WATZ WANANUNUA NAE ANAENDESHA MAISHA YAKE ANAPATA MKATE WA KLA CK NYIE AMBAO HAMUMPEND MMEKAZANA KUPGA MAKELELE HUKU DVD ZAKE ZIKITOKA MNANUNUA KM KAWA

Anonymous said...

jamani watu mna majungu mpaka kwenye misiba? kwakweli watanzania sijawahi kuwaelewa. Ray, poleni sana na matatizo. Chukulia hili kama challenge, usijiskie vibaya baba.

Anonymous said...

Jamani na shangaa watu wengine,kwanini kuzunguza hovyo hovyo bila akili,plz Ray be strong na kaa kimya acha waongee tu yata pita.

Anonymous said...

sasa mlitaka ray afanye nini? amefanya shughuli kubwa sana katika kumlilia swahiba wake, sasa mnaanza kumsimanga anaroho mbaya, sijui mlitakaje?Ray just be stong na wewe mungu atakulipa fungu lako, huwezi kuwa mzuri kwa kila mtu, waswahili kusema ndio zao! hata marehemu walimnanga hivyohivyo amekuwa mzuri baada ya kifo.
mdau
sweden.

Anonymous said...

Ray ndugu unatakiwa ujiulize mara mia mia why watu wanakuonyesha vidole???? najua kwenye nafs yako unaujua ukwel kwamba ulikuwa hauna mawasiliano mazur na kanumba mpaka anakufa,, sis tuliokuwa pemben hatujui kisa na mkasa wew na marehem kanumba ndo mnajua,, jifunze kitu katika maisha yako na huu msiba uwe ndo funzo kuu kwako kwamba unatakiwa kusamehe binadam mwenzako hata kama mmekwazana,, nafkir ulikuwa unataman hata kanumba aamke japo kwa sekunde moja ili umwambie samahan,, binadam tujenge iman ya kujishusha hata kama unaona hujatenda kosa,,, samehe saba mara sabin ili na wew ukasamehe na muumba wako.

Uster said...

yaami kweli binadamu sisi , yaani mnamhukumu huyu Ray as if nyie ni Mungu. mnajua kilichotokea mpaka wao wakashindwa kuelewana???? kila mtu aliyechini mbingu ameshagombana kwa namana moja au nyingine. Muache kaka watu kwanza yuko kwenye majonzi sana he needs support and prayes from us. Ray wewe muogope Mungu sisi binadamu hatuna jema kwa kweli. mimi binafsi nawapenda wote si Kanumba wala Ray .

Anonymous said...

Ray nakulaumu kwakitu kimoja tu wewe na hao bongo movies woote na hiko kitu ni hiki: Mlijua "watu" ndani ya bongo movie wanamu-abused Lulu mkawamnaficha siri. Ona sasa mtoto wa watu alivyoharibu maisha yake na ya wengine. Nyie bongo movie mnajua kabisa ni wapi mlishiriki au mliona kitendo kiovu anachofanyiwa Lulu hamkukemea, kumbukeni Lulu angeweza kuwa dada, mdogo etc wa any of you. Nachukia na ninalaani mafataki wote, mtu mzima yeyote anayetembea na mtoto mdogo na alaaniwe kabisa. Malipo ni hapa hapa duniani. Rest in Peace K and all the best Lulu!

Esther kanda ya ziwa. said...

Sasa jamani hapo kosa la Ray ni lipi? au mna yenu mlikosa pa kusemea msiba umetokea ndo mmepata pa kutolea sumu zenu? na kama kweli nyie si wanafiki kwa nini hamjaweka wazi majina yenu? kila kitu kinakuwa mikononi mwa Mungu, ni kweli tulimpenda sana Kanumba lakini hapo Ray kakosea wapi? je ni nani kati yenu ambae hajawahi kuwa na tofauti au kutofautiana na mwenzie? au kwa kuwa hao mliyotofautiana nao wapo hai ndo maana mnaongea? hivi angefariki mtu ambae ulitofautiana nae tena kwa bahati mbaya na ukaambiwa haya unayomwambia Ray ungejisikiaje? au nyie ni malaika wa nuru? jamani badilikeni sisi wote ni binaadamu na hakuna ajuae baada ya sekunde 1 nini kitatokea mbele yake, na Mungu tu ndiye hakimu wa kweli.

Anonymous said...

duh watu wansema bora angekufa ray,, kweli BINADAMU amefikia hatua ya kumpangia mungu afanye nini? POLE SANA RAY,
matutu

Anonymous said...

Tupunguze ukali wa maneno yaarabbii! Tupunguze chuki, kwani hamna alie mkamilifu, tusiwaombee mabaya wenzetu, na tusiongelee nafsi za wenzetu. Kila mwanadamu ataonja umauti, huu sio muda wakuanza kutoa hadithi nyiingi kuhusu marehemu, huu ni muda wa kumuombea marehemu, aepushie na adhabu za qabri, apokelewe na malaika wema, kwani, maneno maneno yanamkwaza pia huko alipo. Lamsingi ni kumuombea. Tusipende kumhukumu mtu bila sababu jamani, its not fair mnavyomhukumu ray, ni mungu pekee ndio wakuhukumu. TUWE NA UPENDO WA DHATI NA TUJUE KUSAMEHEANA BINAADAMU, KWANI SAFARI YETU NI MOJA, NA TUMUOGOPE M.MUNGU KWA KAULI ZETU NA MATENDO YETU KWA UJUMLA

Anonymous said...

POLE SANA RAY, THIS TOO SHALL COME TO PASS, VUMILIA YATASEMWA MENGI NA TUNAOMBA UTUSAMEHE KWA MANENO YETU MAKALI YENYE SHUTMA....WE ULIESEMA BORA RAY NDO ANGEONDOKA UMEKOSEA SANAAAAAAAA, UMEMKOSEA RAY NA MUNGU PIA... HATA MIE NAMPENDA SANA KANUMBA KULIKO RAY LAKINI SIO VEMA KUMUOMBEA MAUTI MWENZIO.....RIP KANUMBA YOU WILL ALWAYS BE IN OUR HEARTS AND MEMORIES, YOU WERE THE GREAT INSPIRATION TO MANY.

Anonymous said...

Nimesoma comments zote za wadau wanao mponda Ray kuhusu kifo cha Kanumba, lkn SIJAONA hata mdau mmoja ambaye ametoa point ya msingi ya kumponda Ray. Mtu anaponda tu bila vigezo.

Binadamu wote huwa tonatofautiana, sasa kutofautiana kikazi kati ya Kanumba na Ray ni ajabu sana? Na kwa nini lawama ziwe kwa Ray na siyo Kanumba? Kwani mnajua nani alimkosea mwenzake kati yao?

Nimeona facebook watu wanaponda hiyo picha ya Ray akiwa anacheka na mtoto wa Rais, inamaana kwenye msiba watu huwa hawacheki?? Kama kuna kitu kimechekesha lazima watu watacheka, hasa kama mpo sehemu ya nje. Ladba iwe sehemu muhimu sana ambayo haitakiwi kabisa mtu kucheka, hapo itabidi msicheke.

Acheni kukosesha raha Ray.Hata kama amekosea bado ana haki ya kusamehewa.

Tambueni kila mtu ana makosa yake jamani.

Dismas
www.tulonge.com administrator
+255 713 520 629

Anonymous said...

kwanini umevaa sun google mbele ya Mh.Rais we limbukeni kweli huoni wenzako ameipandisha kichwani tunajua hujui itifaki siku nyengine jifunze

Anonymous said...

Kweli nimeamini siye wabongo wengi ni malofa, na hakuna kitu kibaya kama lofa kujifanya anajua, watu wanamfakamia Ray huku hata hawajui chanzo cha ugomvi wao ilikuwa nini! Ray kafanya shughuli nzito sana tokea siku ya kwanza ya matatizo hadi mazishi, lakini leo wajinga wanamlalamikia Ray hata sielewi wanacho mlalamikia ni nini! Kama alivyo sema mdau hapo juu kwanini Kanumba asilalamikiwe kwa kutoomba msamaha ona sasa kafariki na hasira zake badala yake watu wameweka lawama zote kwa Kigosi. Sijui ni umasikini wa mawazo, sijui wa hela au ushirikina ndio unawasumbua watu hata sijui. Ray u did the best u could, n I wish u all that you are wishing yourself in this industry. God bless u na pole sana. Ila ongezeni heshima kwa watanzania tunawapenda.
MDAU
KASUSULA

Anonymous said...

ONENI KAMA HILI LOFA LILILOANDIKA KWANINI UMEVAA SUN GOOGLE MBELE YA RAIS, sasa coment gani hii Ujue Ray watu wengine ubongo zao ni misiba usione wanauwezo wa kuandika ukajua ni wazima, ukiwafuatilia utaishia kuwa msiba wa ubongo vilevile. Siku zote jua hili mwehu ni mwehu tu hata akiwa professor. keep going Ray kwani sote tuna mapungufu, kikubwa ni kuyatambua na kuyafanyia kazi kwa faida ya siku za usoni.
Kasusula

Anonymous said...

Pole ray najua uliiumia , binadamu jamani kwanini tukohivyo mtu namume wake wanaweza kupishana kwa muda sembuse marafiki , hata ray alishasema anajua wangekuja kuyamaliza tu , ila tu bahati mbaya haijatokea lakini sikubaliani na na watu wanaomshambulia ray kwamba mnafiki si kweli ray jipe moyo we chapa kazi. yani binadamu najua ukifa kama leo utaona misifa watakayo kupa ilaukiwa hai ni kukuvunja moya kama walivyofanya kwa swahiba yako

THE GREATEST FUTURE WIFE said...

KILA MTU ANA HAKI YA KUANDIKA COMMENT APENDAYO ILA CHA MUHIMU NI KUFIKIRIA KWA UNDANI KABLA YA KUTUMA COMMENT KUWA ITAMFIKIAJE BABE WANGU, HAKUNA TATIZO ASANTENI SANA KWA MLIOTUMA COMMENTS NZURI NA WALE MLIOTUMA COMMENTS MBAYA HADI MWINGINE AMEFIKIA HATUA YA KUSEMA BABE WANGU NDIO ANGEKUFA MUNGU AKUSAMEHE SANA. BABE WANGU YUKO KWENYE MAJONZI MAZITO SANA SEMA HAMPO KWENYE UPEO WA MACHO YENU MIMI NILIYEKARIBU NAE NDIO MWENYE JUKUMU LA KUMFUTA MACHOZI YANAYOMTIRIRIKA NA KUMPA MOYO, KWA WALE MNAOANDIKA COMMENTS NZURI NAOMBA MUENDELEE KUMPA MOYO MPENZI WANGU ILA KWA WALE MNAOTUMA COMMENTS MBAYA KAMA INAWEZEKANA NAWAOMBA MUACHE KUTUMA COMMENTS KWA SASA MAANA CHOCOLATE WANGU ANAZIDI KUSIKIA UCHUNGU KWA MANENO YENU. ASANTENI SANA NA SAMAHANINI KAMA NIMEANDIKA HUU WARAKA VIBAYA

Anonymous said...

KWENDA ZAKO HUKO BABY BONGO MFYUUUUUUUUUUUUUU

Anonymous said...

pole sana bro ray usijali na coment za wanafiki umewajibika ipasavyo kwenye msiba wa best yako ziba pengo aloliacha steven namungu atakusaidia

Anonymous said...

future wife wishing you all the best ! life is too short.. as you can see.. tell your future hubby to get married soon there is nothing to keep wait okey baby girl??? Back to Ray.... very sorry to loose your twin we both love him as we love you.. Forget about what people talking about bad side of you and Kanumba... thats life baby you can't play smooth game there are up and down in any kind of relationship so don't be annoyed with the comments but make them as motivators in your work and life in general, where you went wrong make corrections okey home boy ... you will be fine don't bother. I appreciate the great job your doing. Keep it up and make market penetration by working beyond the country you have a portential of doing that so boy you can do it! work hard young man. Once again we are all human being and all shall die.xoxomayaxoxo

Anonymous said...

ha ha ha ha the greatest future wife tushachoka kuona na kusikia watu wenyewe kuoa ni ndoto nakuonea huruma ww unaejiita future wife utajiita future wife na kamwe hutakuwa wife pole

Anonymous said...

Hii ni Blog ya Ray itapaswa sie kumtia moyo na kumpa pole kwa msiba wa swahiba wake na sio kumshushia matusi as if ashiriki katika kifo hiki. Aliyehusishwa yuko segerea

Anonymous said...

usemi aliosema kanumba kwenye wimbo wake hata wabaya wake watabeba jeneza lake ndio huo umedhihirisha nawaona wako mbele mbele kwa kila kitu wanajifanya ndio wazuri kumbe moyoni wamefurahi sana kanumba kufa ili............pumzika kwa amani steven

Anonymous said...

MIMI NI MMOJA WA WALE AMBAO WANASEMA KWANINI HAKUFA RAY????????

Anonymous said...

THE GREATEST FUTURE WIFE INDEED! AHAHAHA WACHA NCHEKE MIE NANI KAKWAMBIA TAKUONA HUYO RAY? JINSI MIOYO YA WATU INAYVOMCHUKIA AAKUFA SIKU SI ZAKE

Anonymous said...

Ray pole sana mdogo wangu, hayo ndio majungu ya wa bongo hawana jema, wao nani kawaambia wewe na Kanumba mligombana au ni haya magazeti ya rangirangi ndio yamewamisslead? Achana nao na hao wanaosema bora ungekufa wewe hawamjui Mungu hao, wangekuwa wanamjua Mungu wasingesema yote hayo. Pole sana nakuombea kwa Mungu akupe nguvu upate kuendeleza pale alipoachia ndugu yako.Usimuache mamayako (mama Kanumba) nadhani anakutegemea sana na Inshallah M'Mungu atakuongoza. R.I.P KANUMBA.

Anonymous said...

Watanzania/Wachangiaji wezangu nimeguswa kutoa mawazo yangu /Mtazamo wangu kwa yaliyoandikwa humu, Mawazo ya mtu mara zote hueshimika ( maana ni mtazamo binafsi huwezi lazimisha mtu aone/awaze/aamue kama wewe utakavyo) kwahiyo kila aliyecomment humu yuko sahihi kwa mtizamo wake binafsi na sababu zake zilizomsukuma kuandika alichoandika (UHURU WA MAWAZO) Ila tusisahau kuwa sisi sote ni binadamu hatutofautiani (maana yangu ni mimi nikikatwa na panga na wewe ukikatwa na kisu wote tutasikia maumivu. Ukubwa wa kidonda, Uponaji wa kidonda utategema baadae kwa kila mmoja lakini huwezi mwambia mwenzako asilie maumivu kisa amekatwa na kisu) kwanini nasema hivi Tumejisahau sana katika yale tunayoyaandika humu na kuyaelekeza kwa mlengwa (matusi ,dharau, lawama, kashfa n.k) Tafakari moyoni mwako je ulichokiandika wewe ukiambiwa ni sawa? Kitakusaidia? Kitakujenga? Kitakubadilisha? Utakipenda?
Je tunayaandika haya tu kwasababu tumeamua au ktumejisikia tu au tunahitaji kumsaidia mlengwa?
Je unaweza kumwambia haya ndugu yako, motto wako, mdogo wako? (hata kama unaweza mwambia yatamsaidia kwa kile unachotaka mfano abadilike)
Kwanini tumekuwa na Roho kuliko za wanyama? (ni vizuri kumwambia mtu umekosea hapa, rekebisha hapa hapa hufanyi sahihi au vizuri na saa ingine kusifia pale unapoona kunajitihada mahali si vizuri kukejeli, kutukana kukashfu na maneno mabaya haisaidii
Ushauri wangu TUPENDE KUSIFIA NA KUJIVUNIA vya kwetu zaidi ya vya watu (Huwezi kuishi kwenye nyumba ya udongo halafu ukawa unaidharau wakati ni yakwako ya jirani yako ni block ukawa unaisifia hata hujui uzuri wa ndani au anapata usingizi au laa!) Tusipende kukashfu wasanii wetu. Tuwakosoe kwa hekima ili waweze kurekebisha mapungufu na kupeperusha bendera yetu ya Tanzania pia inapobidi kusifia tusifie.
Si maanishi kuwa hawakosei laa hasha, ila nimeona busara haitumiki katika ufikishaji wa ujumbe.
Tujifunze kitu – Marehemu aliwahi kukashifiwa sana kukejeliwa lakini tuliposikia leo hatuko naye tena hata wale waliokuwa hawamtambui umuhimu wake wameumia na kusikitishwa ila tumeshindwa kujifunza . tunaendelea kuwafanyia waliobaki yale yale.
Wezangu tuwe na Roho ya Ubinadamu hata Chembe.

Anonymous said...

Watanzania/Wachangiaji wezangu nimeguswa kutoa mawazo yangu /Mtazamo wangu kwa yaliyoandikwa humu, Mawazo ya mtu mara zote hueshimika ( maana ni mtazamo binafsi huwezi lazimisha mtu aone/awaze/aamue kama wewe utakavyo) kwahiyo kila aliyecomment humu yuko sahihi kwa mtizamo wake binafsi na sababu zake zilizomsukuma kuandika alichoandika (UHURU WA MAWAZO) Ila tusisahau kuwa sisi sote ni binadamu hatutofautiani (maana yangu ni mimi nikikatwa na panga na wewe ukikatwa na kisu wote tutasikia maumivu. Ukubwa wa kidonda, Uponaji wa kidonda utategema baadae kwa kila mmoja lakini huwezi mwambia mwenzako asilie maumivu kisa amekatwa na kisu) kwanini nasema hivi Tumejisahau sana katika yale tunayoyaandika humu na kuyaelekeza kwa mlengwa (matusi ,dharau, lawama, kashfa n.k) Tafakari moyoni mwako je ulichokiandika wewe ukiambiwa ni sawa? Kitakusaidia? Kitakujenga? Kitakubadilisha? Utakipenda?
Je tunayaandika haya tu kwasababu tumeamua au ktumejisikia tu au tunahitaji kumsaidia mlengwa?
Je unaweza kumwambia haya ndugu yako, motto wako, mdogo wako? (hata kama unaweza mwambia yatamsaidia kwa kile unachotaka mfano abadilike)
Kwanini tumekuwa na Roho kuliko za wanyama? (ni vizuri kumwambia mtu umekosea hapa, rekebisha hapa hapa hufanyi sahihi au vizuri na saa ingine kusifia pale unapoona kunajitihada mahali si vizuri kukejeli, kutukana kukashfu na maneno mabaya haisaidii
Ushauri wangu TUPENDE KUSIFIA NA KUJIVUNIA vya kwetu zaidi ya vya watu (Huwezi kuishi kwenye nyumba ya udongo halafu ukawa unaidharau wakati ni yakwako ya jirani yako ni block ukawa unaisifia hata hujui uzuri wa ndani au anapata usingizi au laa!) Tusipende kukashfu wasanii wetu. Tuwakosoe kwa hekima ili waweze kurekebisha mapungufu na kupeperusha bendera yetu ya Tanzania pia inapobidi kusifia tusifie.
Si maanishi kuwa hawakosei laa hasha, ila nimeona busara haitumiki katika ufikishaji wa ujumbe.
Tujifunze kitu – Marehemu aliwahi kukashifiwa sana kukejeliwa lakini tuliposikia leo hatuko naye tena hata wale waliokuwa hawamtambui umuhimu wake wameumia na kusikitishwa ila tumeshindwa kujifunza . tunaendelea kuwafanyia waliobaki yale yale.
Wezangu tuwe na Roho ya Ubinadamu hata Chembe.

Anonymous said...

Ray please take care of Kanumba's mum at least afarijike am sure u will be blessed for this broo

Anonymous said...

umesemwa na uturn blog,katoa sasa udaku wanayokasome.siri zinatoka.

Anonymous said...

NAOMBENI KUULIZA KUVAA MIWANI MISIBANI INAMAANISHA NN UCHUNGU SN AU,NI MTAZAMO TU MAANA 90% WAMEVAA

Lucky Pesa said...

Pole sana Ray.. najua ni kiasi gani umeguswa na msiba wa swaiba yako.. kugombana kupo katika maisha na nikitu cha kawaida. Nimefurahi sana kuckia umefika kwenye msiba. hata mungu amesema kugombana ama kukwaruzana kwa njia nzuri haswa ya mafanikio ni kawaida. pole sana kwa msiba kwa kifupi msiba wa steven kanumba umeniuma sana ila sisi tunampenda ile mungu amempenda zaidi kwani leo yeye kesho sisi. chapa kazi kwa bidii napenda sana movie zako kwahiyo usituangushe.
Lucky from Belgum

Anonymous said...

umeona mange kimambi alivyosema kwenye blog yake uturn blog?sasa katoa lakini udaku wamecopy hiko huko hatari,kunaukweli?watu wengi wamesoma huku uk ndio zungumzo la kuhusu wewe.kumbe wewe ndiye ulikuwa naongea nalulu ule usiku?

Anonymous said...

hta km wanakulaumu jiulize wasanii wangapi wapo kwanini iwe wewe tu huoni kuna ulakini ray???? ujuwe siku zote lisemwalo lipo

priscah said...

Its painful to lose a luvd 1,take heart Ray.Wanafiki watasema tu na usiku watalala.
THEY R THROWING SAND AT U, JST SHAKE IT OFF AND STAND ON IT.What u did as preparation for kanumba's burial is wht a gud friend would have done, ur reward is in heaven.Good things one does will not go unrewarded.
Na aliesema ni heri Ray angekufa na kanumba kubaki SHAME ON U. Kazi ya mungu haina makosa na ulichofanya wewe ni kumkosoa Mola.
We lovd Kanumba bt God luvd him more. En where ever he is , am sure he is thankful to u Ray for wht u did for him, makin sure he rests well. I luv ur movies, go on en on, en on.

emuthree said...

KILA NAFSI ITAUONJA UMAUTI, YEYE KATANGULIA NA SISI NI WATARAJIWA TU!

Anonymous said...

kwanini hamjamshutumu aliefanya mapenzi na under 18 (mwanae aliemlea)?.. mnakomalia asie husika na chochote?..Marehemu aliposemwa vibaya bba ray ndo alimpokea na kumuandalia sherehe km kumpongeza swahiba wake leo hii ndo mbaya..afu yule anaesema et ray anaiga kaiga nn? mbona anapiga muv zake hapahapa bongo hajaiga kwenda nigeria na anapiga mapesa..uliza uambiwe usilopoke unajua nani wakwanza kuanzisha muv company? nani wa kwanza kununua hiace ya compay? nani wa kwanza kununua vx tena new? ndo utajua! nakukubali bro keep it up..achana na hao wanatembelea blog yk afu wanadai hawakupendi wafungue BBC sasa

Anonymous said...

Ray nakupenda sana na ninafagilia sana movie zako jaribu kuangalia maisha yako usiangalie binadamu tunaongea nini siku zote hakuna mtu anapenda maendeleo ya mwenzako akikusema hufi wala hupungui nakuomba uwe mvumilivu na maneno ya watu waliokosa kazi ya kufanya. take care

Anonymous said...

wewe ray safisha jina lako kama kweli hukuusika na kifo cha kanumba,lazima umfikishe mange polisi kwakutangaza nakutoa maelezo aliyoambiwa na polisi,au nyie wabongo munamuogopa sana Mange kimambi.

Anonymous said...

wewe umemuuwa mwenzio lakini kumbuka TUPAC aliuwawa na B.I.G na serikali ikamuachia baadae wapenzi wa TUPAC wakamuuwa B.I.G,sasa subir wewe zamu yako tutahakikisha na wewe unakwenda kwa baba soon,tunasubiria kesi tuone itakavyokwenda..halafu tutajua WHAT NEXT.

Anonymous said...

jamani why ebu muacheni kijana wawatu, yameshatokea bac tumshukuru mungu.

Anonymous said...

msipende kubwatuka vitu ambavyo hamna uhakika

Anonymous said...

huna lolote mnafiki tuuu wewe ulizani kutoa roho yake ndio utashika nafasi yake? NAKUCHUKIA MPAKA BASIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

Anonymous said...

we kunguru hapo juu marehem amefanya mapenz na under 18???? kwa hiyo kanumba ndo wa kwanza kumtoa bikra huyu mtoto malaya???? ndugu uliza upewe list ya huyo unaemuita mtoto kam ckosei kanumba atakuwa wa mia 200

patrick said...

jamani hivi kwa nini kazi ya mungu tunaichukua sisi waja wake?kwa kutoa hukumu kali kwa mwenzetu,tumuogope mungu,kila mja atakufa kwa wkt mungu alioupanga na sio kumhukumu ray.rip kanumba

Anonymous said...

Yaani nakuonea huruma sana Ray,hivi huyu msichana anakitu gani maana ukienda kwenye blog yake anavyokuponda ni hatari,nakujisifu kuwa polisi awawezikumfanya kitu chochote,mimi ningekuomba uende kuonanma na Rais nakumuelezea haya mambo yakutukanana kwenye mablog na vile vile kumuonyesha kwamba tanzania hakuna sheria,yeye si ndiye kiongozi wetu bwana,haya mambo yasingekuwa hivi enzi za nyerere kabisa,huyu msichana ametukana wengi sana na kujisifu hakuna mtu atakaye mfanya chochote,yeye akumbuki baba yake yaliyomtokea,am sure tanzania watu wanaamua kuchukuwa sheria mikononi mwao.

Anonymous said...

HUYU MSICHANA MANGE INABIDI MTU AKAWAAMBIEUBALOZI WA MAREKANI HAYA MAKASHESHE YAKE PIA NA HII KESI YAKO,WASIMPE VISA MPAKA AJIBU KOSA LAKO,YAANI YEYE ANAENDELEA NA MAISHA YAKE KAMA KAWAIDA WEWE UNATUKANWA,WAANDIKIE UBALOZI WAMAREKANI BARUA KAMA UMEMSHITAKI NATUMA PROOF ZOTE SIALIANDIKA KIINGEREZA?WAMAREKANI HAWATA M,PA VISA HUYO.

Anonymous said...

Mshikaji mbona huna jipya? Au unapambana na Mange Kimambi? Tunapenda Blog yako bwana weka mambo