Monday, March 19, 2012

HAPPY BIRTHDAY BONGO MOVIE CLUB

 Bongo Movie club yafanya party kubwa ya kutimizwa mwaka mmoja tangu ianzishwe iliyofanyika katika viwanja vya Bussiness iliopo maeneo ya Victoria. Ni vigumu sana kwa wasanii Tanzania kuanzisha kitu chenye umoja na kufikisha mwaka mmoja kwa kweli Bongo Movie club wanastahili sifa kubwa sana. maana kiuhalisia sisi wasanii bongo tuna matatizo sana atuna umoja wala upendo wa dhati toka katika mioyo yetu zaidi ya kuchekeana kichina tu lakini tunaamini kwa nguvu za Mungu wa imani tutabadilika na kuwa wenye upendo wa dhati.

 Viongozi wa Bongo Movie club wakipata picha ya pamoja The Greatest kati Richie Richie na Hartman Mbilinyi vijana wamendeza na suti zao za ukweli.

 Kama kawa mambo yakiwa yanazidi kunoga

 Wazee wa kale hao Mzee Korongo akiwa pamoja na mzee Mbembe kushoto party ilipendeza sana jamani

 Mnakumbuka jamani Bi Kidide enzi za Koale kukundi kilichotoa mastaa wengi mnaowaona sasa wakitesa katika tasnia za filamu 

 Wema Sepetu ndani ya Red Capet akipata interview toka kwa mtangazaji wa Staar tv Dada yetu Sauda Mwilima

 Wema na Ray

 Tino na Sandra

 Viongozi wakiteta jambo

 Wageni waliodhuria sherehe ya Bongo Movie club ya kutimiza mwaka mmoja

 Maya na Recheal picha ya kumbukumbu

 Wema sepetu na rafiki yake

 Johari na Uwoya

 Mwanamuziki wa kizazi kipya Sheta wa kati naye alikuwepo

 Steve Nyerere wa katikati pamoja Iddi aka( Mchongo) wa kulia

 Wolper na Odama kulia

 Amani kwenu warembo wa Bongo Movie club

 Rizi One Kikwete mtoto wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania akifungua rasmi party kwa kuwasha mishumaa kwenye keki rasmi iliyoandaliwa kwa siku hiyo

 Mwenyekiti wa Bongo Movie club JB akiweka mambo sawa katika upande wa keki

Keki yanye mfano wa Camera yani ikiashiria ndio kitendea kazi kukibwa sana katika upande wa kazi zetu, Bongo Movie club 2012 nitwaletea matukio mengine yaliyojiri mambo bado sana kulikuwa na burudani za kutosha

19 comments:

Anonymous said...

Ebana eeh!!! hivi ilikuwa ni kushelekea mwaka mmoja wa bongo movie au kushelekea kuonyesha Nyeti zenu..Muone MAYa mazingira yako wazi kabisa....Ukija KWa UYOYA white Chup** sijui anamuonyesha nani....alafu jamani Mekapu..naona zinawakataa sasa wakina dada..du mnakuwa kama mmepaka vumbi la chaki..usoni..
mdau..Ford Forcus Corsa

Anonymous said...

jamani akina dada mmezidi kuvaa vinguo vivupi.haya angalia hapo uwoya mpaka chupi nyeupe inaonekana katikati.au ndo biashara?

Anonymous said...

Ray picha nzuri sana...jamani tunaomba muwashauri dada wa bongo movie wawe wanavaa kiheshima...yani wamevaa kikahaba sana..watu wanamsemaga wema lakini siku zote kavaa kiheshima..cheki uwoya chupi nyeupe inaonekana..nahuyo jimama rachel rachel paja lote njee..jamani mbona ni warembo sana hata wakivaa kiheshima tunawapenda kwa kazi zao..warekebisheni hao wanaaibisha

Anonymous said...

HONGERENI KWA KUTIMIZA MWAKA MMOJA.MUENDELEE NA UMOJA HUO HUO.

Anonymous said...

Habari Vicent Kigosi, hongera kwa kazi nzuri, sisi ni watanzania tupo UK ingawa tunaishi huku lkn tunafutilia kazi za nyumbani kiukweli mnajitahidi ingawa tumechoka na waigizaji wa kike hawajui wanafanya nn ingawa sio wote, kuna dada mmoja anaitwa (Batuli) we love her hatujawahi kuona ukicheza nae bali tumeona ameact movie na Kanumba (Fake smile) ask anyone atakuambia tunavyompenda huku uingereza sor hatujui anaitwa nani kwa jina lake halisi tafadhali mtafute umpambanishe na johari sisi huku tuna kikundi kinaitwa Tanzania Foundation mpango wetu ni kuanza kuwaalika waigizaji tofauti kutoka bongo ila tutaangalia kazi sio jina lake chukueni ushauri ili mfike mbali tunamkubali johari pia. Godluck naomba email na namba kwa mawasiliano zaidi tupo kwa ajili yenu,karibuni.

Anonymous said...

party ilikuwa nzuri Ray ila shida inakuja kwenye uvaaji wa hao dada zetu/zenu wa bongo movie. wanashindwa kutofautisha nguo ya kuvaa disco na kwenye party ambayo mi nimeona ya umuhimu sana. Jamani wawe wanaangalia basi hata kwenye matukio ya hapa hapa bongo wadada wanavyovaa sio hivo vikaptula vyao. HEbu mchek Jack Wolper jmn so rough wakati angevaa gauni lake zuri la mburuzo angekuwa beauty.Wanaume mmependeza hebu wasaidieni hao dadaz wa bongo movie kuvaa kulingana na tukio dah.. By the way picha ya Johari na Irene Uwoya sijui ni macho yangu tu naona kama "PICHU" nyeupe ya irene inaonekana au ni umakini wa utazamaji wangu umenidangaya!!

Anonymous said...

ray umependeza sn sn suti plain ndo mpango mzima na si zamaua maua au mistari miastari tatizo moja tu.......... umesahau kutoa lebo ya suti hapo mkononi wengi hawajuagi ilo ila juzi anko misupu alitoa clip inayofunza ilo swala. TUNAPASWA KUTOA IYO LEBO

Anonymous said...

Samahani Ray, hiyo picha ya Uwoya hebu iondoe umsitiri tafadhali, naona kufuli yote inje

Anonymous said...

huyo Irene ndo nini kuonyesha mchupi wake?mbona mnajizalilisha sana jamani yani hadi aibu inasikitisha kwa kweli.ffyuuuuuuuuuuuuuuuuuu

Anonymous said...

Kiukweli sina lawama sana na upande wa wanaume haswa katika swala la uvaaji kulinga na tukio siku hiyo.Ila kwakweli dada zetu wa Bongo Movie wametokota vya kutosha yani hi ushamba ulioje hata kuiga kidogo kwa wenzetu.Yani bora wangwevaa sare ya vitenge lakini kuvaa vitu vya ovyo visivyo eleweka utadhani wapo kwenye viduku vya tandale.fikisha ujumbe huu wajifunze kutambua matukio na uvaaji wake.Ovyoooooooooooooooo

Anonymous said...

jamani Irene unavaa nguo fupi mpaka mpaka chupi inaonekana....SHAME ON YUUUUUUUUUUUUUUU

Anonymous said...

RAY WALA USIIONDOE PICHA YA IRENE MUACHE COZ ALIAMUA KUONYESHA ULIMWENGU MZIMA KAMA KAVAA CHUPI NYEUPE WADAU WALA MSIUMIZE VICHWA VYENI KUWAPA USHAURI HAWA MAKAHABA COZ WANAJUA WANACHOFANYA WAACHENI WAKICHOKA WATAACHA WOLPER LINAONEKANA KAMA LISHANGINGI FULANI MFIUUUUUUUUUUUU

Anonymous said...

kama uwoyan maya ndo tatizo sas ile biFU YA KANUMBA ITAHAMIA KWA NAYA NA UWOYA BORA HATA UWOYA UNFANYA NAEKAZI HATOMAINDI ILA MAYA SAFRI YA KANUMBA FULL KUCHEKEANA LAKIN MOYON ANAJUA MWENYEWE,, NOT SURE BROOO dont take serious.. emma matutu saut

Anonymous said...

mdau hapo juu ulosema wangevaa vitenge na kuunga mkono na mguu. mana hizo vyupi vimetuchosha. hao wano jiita ma actres wa bongo jifunzeni kutoka kwa wenzenu mana mawigi imekuwa too much na hamjui kuyavaa make up ndo usiseme ziro kabisa. na we mainda hicho kigauni kama mtoto au unajiona mtoto in short hao wadada style yao ya mavazi ni sifuri nukta.

Anonymous said...

NAOMBA KUJUA ALIPO MDADA MZURIII KULIKO WOTE SIJUI JINA LAKE VEMA ILA ALIWAI KUIGIZA KATIKA MUVI MOJA YA KANIMBA INAITWA'' THE LOST TWINS'' YULE MDADA AMBAYE ALIKUWA KAMA STERING PLEASE NAOMBA MNIJUZE ALIPO I LOVE HER MUCH

Anonymous said...

Jamani hata kama ni ukahaba sasa huo umepitiliza. Kuweka mchupi wako nje wa faida ya nani???????? Inaonyesha jinsi gani akili za wtu wote waliovaa hovyo zilivyo finyu. Shule ndogo nayo ni kikwazo sana. Acha mtu akupende kwa UTU wako si kwa kitu au kujionyesha mapaja yenu. Upumbavu mtupu.

Anonymous said...

I just couldn't go away your site before suggesting that I extremely loved the usual info an individual provide on your visitors? Is gonna be back incessantly in order to investigate cross-check new posts
My page - samson tobacco

Anonymous said...

Fantastic goods from you, man. I've consider your stuff previous to and you are just too great. I really like what you have got right here, certainly like what you're stating and the best way wherein
you are saying it. You are making it enjoyable and you still take care of to stay
it wise. I can't wait to learn far more from you. This is really a wonderful website.
Here is my page : amber leaf

Anonymous said...

That is a great tip especially to those new to the blogosphere.
Short but very precise info… Appreciate your sharing this one.
A must read article!
Take a look at my blog post old holborn tabak