Friday, July 6, 2012

THE GLORY OF RAMADHANI COMING SOON

Wadau na sinema za RJ Company napenda kuwafahamisha kuwa nimeamua kutoa movie hii ya The Glory of Ramadhani kwa ajili ya mwezi mtukufu unaokuja hivi karibuni , lengo ni kufikisha ujumbe kwa ndugu zangu Waislam kwani si waislam wote wanaenda misikitini kusikiliza mawaidha basi kupitia sinema hii watu watajifunza mambo mazuri ya kumpendeza Mungu hii si ya kuikosa, maasusi kwa mwezi mtukufu lini itatoka? ni kabla ya siku tatu kuingia kwa Ramadhani..


 Huu ndio mwanzo wa The Groly of Ramadhani ni filamu ambayo tuliweza kuifanya kwa umakini mkubwa sana ili watu wajifunze kutenda mema kwa miezi yote kumi na mbili na si mwezi mmoja..

 Kazi imeanza..

The Greatest nikiwa na vijana wangu kazini.

Mambo yakiendelea kupamba moto wadau huu ni mzigo hatari wenye mafunzo ya kutosha

 
 Chuchu Hans on set

 Chuchu Hans pamoja na Dura wa kipindi cha Planet Bongo wakiwa on set huku The Greatest nikiwapa maelekezo jinsi scene inavyotakiwa kuchezwa, wadau huyu kijana Dura ni tunda la baadaye litakalokuwa bora kwa miaka ijayo kama unabisha nunua mzigo huu utaamini nachokisema

 
 Angalieni vijana wanavyofanya kazi.

Chuchu Hans akiwa na Dulla kijana huyu anakuja vizuri anaweza kuja kuwa Kanumba wa baadaye

 Kazi ikifanyika.

 Tukiwa nje ya mji.

 Mimi sisemi cheki mwenyewe watu walivyo makini na kazi zao hii ni moja ya scene ambazo watu wengi waliikimbilia kwa ajili ya futari sikupata tabu sana kupata exttra..

 The Greatest nikiwa na Neshi katika The Groly of Ramadhani wadau nimetimiza yale mliokuwa mkiniambia kuhusu huyu dada kuwa mnahitaji nicheze naye sinema haya bila nyinyi mimi nisingefika hapa hivyo sina budi kuwasikiliza katika mambo mazuri mnayoniwazisha

 Neshi na Bachard.

 Neshi akikamua.

The Greatest na Nesh on set tukifanya vitu

Hii ni scene ambayo ilikuwa ngumu sana kuitengeneza..

 
 Kila jambo lina wakati na huu ni wakati wa The Glory of Ramadhani.

 Tuliweza kupata location zenyewe kama mnavyotuona.

Asante Mungu kwa kunitia nguvu kwa kuweza kuendelea kuelimisha jamii kwani Mungu baba hii ni kazi ulionichagulia mwenyewe na ndio maana unabariki kazi ya mikono yangiu.

51 comments:

kay said...

ray r na l pia la kuliangalia,nesh mashaallah shavu lazidi kuwa dodo

Anonymous said...

Johari yuko wapi? Ray u seem to dominate this thing more......

Anonymous said...

Thanks so much Vicent Kigosi siamini kumuona Batuli tena katika ulimwengu wa Film nimesikia raha mpaka machozi yamenitoka, Kiukweli mimi ni mshabiki namba moja wa film zako na hasa hasa Blog yako lakini kiukweli from my heart leo nimekupandisha Grade kumbe wewe ni msikivu kwa Fans wako, I can't wait to see your New Movie with Batuli I live her with all my heart nikija Bongo nitahakikisha nafika RJ and please naomba msaada wa kumuona Batuli face to face I beg you Brother, God bless you hujui ni jinsi gani umenifanya nilie leo kwa furaha, thanks again Ray god protect you. Its me mr_michael@hotmail.com

Anonymous said...

JAMANI NIMEMUONA BATULI (NESHI) NIMEUMIA KANIKUMBUSHA KANUMBA MASKINI. RAY MPE POLE SANA BATULI NA WEWE PIA NAKUPA POLE NIMEGUSWA NA PICHA HIZI I HOPE HII MOVIE ITAKUWA NZURI HONGERA KWA KUCHEZA NA BATULI BINAFSI NAMKUBALI SANA HUYU MREMBO ILA NATAMANI KUMUONA AKIIGIZA KWENYE SEHEMU ZA UTATA MAANA MOVIE ZAKE HUWA ANATIA HURUMA SANA I WISH ACHEZE KAMA MWANAMKE MTUKUTU ANAONEKANA MPOLE SANA SALAM KWA BONGO MOVIE WOTE KARIBUNI MALAYSIA innocent_bahilopa2003@gmail.co.uk

Anonymous said...

Nice job ray unafaa sana katika mafanikio Merci umetupa tukitakacho Batuli wa Bosco huyo nakumbuka mbali itabidi niweke Fake smile niangalie upya kwa furaha ya ujio wake mpya mara ya mwisho nilimuona kafanya kazi na Jb nae mwambie tunaomba kitu kipya kama hiki cha kwako akiwa na Batuli mimi kwa huyu dada nanunua hata copy 10000 na kuzigawa bure kwa jamaa zangu huku Ufaransa am falling in love with her, hata my wife analijua hilo nina picha zake nimezitoa Facebook nimezisafisha na kuziweka kwenye Album na nyingine kwenye frame ili uamini hili nipe email yako napiga picha nyumba yng nakutumia uone, nilikuja February Tanzania lakini sikujua nianzie wapi ili nionane nae bahati nzuri nilionana na Aunt Ezekiel kwa lady jay dee nikamuomba lakini hakuonyesha ushirikiano matokeo yake alinipa namba hii 0787448644 ambayo haipatikani kabisa nisaidie kupata contact zake hii ni mara ya pili nakuomba contact za Batuli namutumia email kwa facebook lakini hajawahi kunijibu

Anonymous said...

I can't believe this is it Batuli? No no no naota or? C'moon Ray mwili umekufa ganzi I don't know how to explain my brother call me and he tells me open Ray the greatest blog for sure umenishtua you know what The great alipokuja US nilimpa maagizo ya Batuli na aliniahidi atayafikisha but nilipojaribu kumsumbua kwa simu aliniambia Batuli kaolewa India so since hapo sijawahi kumuona tena. For real I'm very very happy. Mr,greatest nina dada zangu hapo tafadhali kama hutajali naomba email yako nikutumie namba zao ili wakueleze shida yangu sina nia mbaya kabisa please try to help me nipo chini ya miguu yako please please please usiniangushe kaka nakuomba sana my adress is Bryan2424@yahoo.co.uk or bryan2424@hotmail.co.uk nashindwa kuandika my phone no hapa its very open

Anonymous said...

Yaani huyo mdada Neshi ni mzuri looooh halafu sijui nimewahi kumuona kwenye movie gani? Anatisha nimempa max zote kumbe kuna wanawake warembo zaidi ya akina wema na uwoya? Mpaka namuonea wivu ray kama ni msanii wako mpya umepiga bao hata hao wasanii wenu wa magazeti watajipanga sasa halafu hapo nahisi hata make up hana hivi akilipuka anakuwaje? Mungu anaumba msichana unamwangalia mwenzio bila kuchoka looooh

Anonymous said...

Bonge la suprise big up Ray sikutegemea kukuona na Neshy ila mimi namuita Batuli sipati la kusema nazijua kazi zake 2 au 3 hivi dada anaijua kazi yake vizuri hutenda haki awapo mbele ya Camera msalimie sana mwambie mashabiki wake tupo kumpokea kwa mikono 2 we love her

Anonymous said...

WELCOME BACK BATULI "WELCOME BACK BATULI "WELCOME BACK "BRAVO BRAVO Mr,Greatest Neshi anatisha kwa uzuri kama jini "MR,Greatest nakupa 5 Batuli ni moto wa kuotea mbali hata Chuchu nae mkali ila kwa Batuli bado sana huyo mwingine kama kibibi ni Davina!?! Waambie wamefunikwa na mtoto wa kimanga hapo Batuli sijui mwarabu

Anonymous said...

I'm so proud of you nampenda Batuli sana.

Anonymous said...

Hello Mr,Greatest pole kwa kazi ngumu ya kuelimisha jamii and hongera pia kwa kukubalika maana si kazi ndogo I will try to advice you pale niwezapo by the way pole kwa kumpoteza swahiba wako Steven Kanumba poleni sana bongo movie kwa pigo hilo. Ray maisha anapanga Mola wetu lakini amini ya kuwa yawezekana kesho hawa madada wanaocheza movie ndio wakawa wake wa marais wajao. Hivyo basi fanya nao kazi kwa upendo mkubwa chuki,ubinafsi wekeni pembeni naomba kujua kama Jb,Richie,Cloud nao wana blog kama wanazo tuandikie hapa tuwape ushauri au tusaidiane pale panapobidi kazi mnayofanya ni kazi yenye heshma sana kama mtajitambua na ndio kazi inayoongoza duniani kwa utajiri badilikeni na mrekebishe mapungufu yenu, mimi sipo Tanzania ila nafungua sana blogs za nyumbani kama Michuzi,global publishers na hii ya kwako. Naamini Wema Sepetu, Irene Uwoya,Jackline Wolper na Aunt Ezekiel hawana sanaa yoyote ya kutisha am educated kwa kusoma magazeti tu ya nyumbani nimegundua hawajui walifanyalo na film hawajaiweka kama ndio kazi zao bali wanaishi kutegemea magazeti ili wapate watu fulani hawana umaarufu kupitia kazi zao umaarufu wao unaletwa na magazeti kwa kucreat scandals mbalimbali, kuna msanii anaitwa Johari huyu dada alipata umaarufu kupitia kazi nzuri ya uigizaji badilikeni asiyejua thamani ya afanyacho msimpe kazi, leo nimemuona Neshi ingawa kmy side namuita Batuli nimemfahamu dada huyu kupitia Movie ya Kanumba na pia nimewahi kumuona kupitia Movie ya JB huyu dada anajua afanyalo ogopa mtu aliyefanya kazi 1 au 2 kisha akakubalika ipo siku atasimama na kuwashangaza nyie mliotangulia nyota njema huonekana asubuhi, nilipokuja Tz mwaka jana mwanzoni nilikutana na Batuli Twanga pepeta Billcanas nilijaribu kumsumbua lakini sikuambulia kitu nikajaribu kwa Aunt Ezekiel daaah, sikuamini alivyo cheap. Kiufupi badilikeni Ray wapo wanaoweza kazi bila scandals tumechoka kuwasoma kwenye blogs kila kukicha, tungependa tusome dada flani kaalikwa kucheza moovie Ghana, au katunukiwa tuzo flani kutoka nchi flani au hata kawa balozi wa watoto kupitia makampuni flani au hata kawa mbunge hayo ndio maendeleo sio uchafu kila kukicha. We need changes.

Anonymous said...

Huwa nachungulia humu halafu nafunga sijawahi kutupa comment hata siku moja but today umenikosha now umeamua kufanya kazi mimi na wale wakina Uwoya ni vitu viwili tofauti huyu Neshi namkubali sana na ubarikiwe na Mungu kwa kutuletea tena katika movie huyu ni kipenzi chetu kwa sababu ya tabia zake hatujawahi kumuona kwenye udaku kama hao mnaowaita mastar wa kike kwangu mimi Star ni Johari,Neshi "+Batuli"+ na Riyama hawa ni kiboko ya wote kwa upande wa wanawake. Wasanii hawa niliowataja wanapiga kazi kisawasawa huwa hawafanyi makosa wale micharuko mngewapumzisha kwanza na kuwaonyesha kuwa wapo wengine zaidi yao. Am Rehema I'd: rehema_kawawa@yahoo.com or 022 2770251 karibuni kwangu Mbezi beach kwa location lakini sharti ni moja mkiigiza na Batuli,Johari au Riyama other wise mtanisamehe.

Anonymous said...

Mr,Greates Today's nature but tomorrow's future let's me advice you weka masharti ya kazi au bongo movie club wekeni sheria mpya za kazi kisha inueni vipaji vipya kwa mara ya kwanza leo umenifurahisha kuona sura mpya katika kazi yako tena mrembo kupita hao unaowachagua kila movie can I talk to Mr,Jb? Naomba jina la blog yake and Mr,Cloud + Mr,Richie secondly karibuni Masaki nawezaje kuwapa mualiko? Mnapatikana wapi? Ila sitawahitaji Aunt,Uwoya na Wema. Hawa hapana msije nao.Please Accept my Invitation. Nawapataje?

Anonymous said...

I like da Comments za hapo juu yaonyesha wazi waliochangia wameenda shule na wanapenda film za Tanzania, Mr,Greatest naungana na wadau hapo juu wakina Uwoya wametuchosha tunataka watu wapya kama Neshy ((batuli)) msichana mzuri mpaka raha nawatakia kazi njema na isiwe hii tu tupe na nyingene ya aina tofauti ukiwa na huyu mrembo. La mwisho nyie wadau punguzeni kumlilia huyu msichana woooote mnaonekana mnamtaka ebo si mtamfanya aandamwe na scandal sasa

Anonymous said...

Woooooow! Amazing Ray umependeza sana u look good ndani ya kanzu, na hilo Ua la safari hii ni kiboko Neshi mzuri sana waliotangulia kuweka post zao naona wanagombania nafasi za kuoa wanamwaga contact zao bila woga naweza kutowalaumu maana mwanamke mzuri sana huyu BATULI kama namuona mie Mungu hakosei jamani. Waambie hao wasanii wa magazeti kuna mtu anakuja wakae mkao wa Taharuki. Tunaisubiri kwa hamu THE GLORY OF RAMADHANI. Thanks Mr,Greatest salam nyingi kwa Neshi BATULI

Anonymous said...

Mmmwaaaaaaaaaaaaaaah! Batuli huyoooooo, Ray akhsante saaaaaaaanaaaaaa mtoto tulimmiss huyu mpaka basi lakini hao wadau waliochangia wananifanya nichanganyikiwe naomba kuwafahamisha tu kuwa huyu sio sawa na kina Aunt,Uwoya au Wema huyu anajua atakalo kimtazamo tu maana angetaka umaarufu na mapedeshee angeuza story kama wenzie ili nae awe Star wa magazeti Ray mnyanyue Neshi wetu lakini mpe masharti mapema asije kujisahau kama hao mastar mabongo lala wanaotumia miili yao kujipatia maisha bora badala ya kuchapa kazi kama akina johari,jb na wengineo. Heshma ya pesa uitafute kupitia mikono yako miwili hapa nina maana ya kuchapa kazi na hapo Mwenyezi Mungu hushusha riziki na utajiri uliomwema waambie wakina Uwoya hadithi nzima ya ulipoanza mpaka hapo ulipo ili wajue umetoka wapi hadi leo hii unamiliki vitu mbalimbali vya gharama namuasa Batuli atulie na asiwafuate wakina Wema na Uwoya mwambie afanye kazi kwa bidii na sio scandal kwa bidii.

Anonymous said...

Mh kweli Davina yupo kama kibibi halafu huwa hana mvuto huyu mdada binafsi namuona wakizamani hana jipya wenzie wamebadilika wanaenda na wakati yeye sijui yupoje ngoja niliachie hapo Ray umependeza na Batuli wa Kanumba mmevutia sana hapo nimeikubali casting more than 100% kingine nikushukuru kwa kusikia tutakacho hata mie nilikushauri ucheze na Batuli talk to her mwambie mashabiki wake tupo wengi hatuhesabiki, mpe hongera pia Johari kwa kuwa najua fika nae anahusika kwa hili la kutuletea Batuli katika kazi za Rj mmepiga hatua unajua kumsikiliza mteja ndio mwanzo wa mafanikio ili uthibitishe hili tafuta mgahawa unaosimamiwa na wahindi angalia huduma utakayoipata lazima kesho urudi sasa basi katika kazi binadamu anapaswa kujua wateja wake wanataka nini na sio yeye anapenda nini umetukonga nyoyo zetu.

Anonymous said...

HAYA HAYA MAGAZETI YA UDAKU SURA MPYA YA MAUZO HIYO SOKONI HONGERA RAY KUMRUDISHA BATULI WA KANUMBA ILA SASA HIVI NAONA UZURI WAKE UMEONGEZEKA MWANZO MZURI NA ISIWE HII TU THE GLORY OF RAMADHAN NATEGEMEA NA ZIJAZO NIIONE SURA YA HUYU MALAIKA IKIFANYA MAAJABU RUDISHA VIPAJI NA INUA VIPAJI VIPYA NASISITIZA KUWA KARIBU NA MASHABIKI ILI UJUE TUNATAKA NINI NAITWA FLORA

Anonymous said...

A loving hearts is the beginning of all knowledge nimeipenda hii Ray kusikiliza watu wanataka nini big up Mr,Greatest mwanzo wa fanaka huu natarajia kuna nyingine tutakuona na Batuli baada ya hii THE GLORY OF RAMADHAN Keep it up utatufanya tukupende zaidi kioo cha jamii husikiliza jamii na kutekeleza yale ya jamii.

Anonymous said...

Being a good actor isn't easy kwa wapenzi wa film watakuwa wamenielewa. Nimependa maamuzi yako ya kuweka sura mpya kwenye kazi zako endelea hivi hivi. Global Publishers nao watafurahi maana mauzi yataanza na sura mpya waliopo soko lao limeshuka wamebakiza funny moja tu scandals kazi Kwishney.

Anonymous said...

Shangwe na vigeregere vikufikie ray khaaaaaaa umemtoa wapi Batuli umenipa tabasamu leo

Anonymous said...

Very nice Ray maisha yenye mafanikio yanahitaji usikivu tupe majina ya blog za wenzio tunataka kujua wanafanya nini. Nampenda Batuli msalimie sana bila kumsahau johari natamani wakutanishwe kwenye film.

Anonymous said...

NAMFUNDA BATULI JAMBO MOJA KUBWA NI KUENDELEZA KUJITUNZA NA KUISHI KIMAADILI KAMA ALIVYOIBULIWA NA MAREHEMU STEVEN KANUMBA NA AKAPOA BASI NDIVYO NINAVYOMUASA NA SASA PIA NAMPONGEZA KWA KURUDI KWENYE FILM CHAPA KAZI MREMBO NA MSIKILIZE SANA RAY NA JOHARI. SHABIKI MARY

Anonymous said...

Kuna kupiga hatua na kukimbia Ray leo umekimbia I hate ukicheza movie na wale Scandal girls ingawa mnadai ndio wanauza movie eti kisa mikasa yao ya kwenye magazeti answer my Question Johari hana scandal mbaya je anauza movie au hauzi? Acheni imani potofu kazi nzuri hujiuza yenyewe na sio msanii mwenye bad news always ndio anauza movie wakati wa kuwa wapya ndio huu don't waste your time for bad actresses.

Anonymous said...

Mashallah mnawakawaka Ray kama muislam yaani umependeza mpaka nakosa la kusema na umejua kuchagua msichana mzuuuuuri wa kucheza nae I wish ndio mngekuwa mke na mume USHAURI WANGU KWAKO RAY:MUOE BATULI MTAPENDEZA SANA NA SIJUI MTAZAA MALAIKA? MAANA NYOTE MASHALLAH. Tunaisubiri kwa hamu film hii tuone cheche zako mpya. KARIBUNI DUBAI

Anonymous said...

ray me namkubali sana batuli she is qute, jaman, kweli nakumbuka waliectia movie flan na jb home


ila kunawatu wadogowadogo wanaectijamani, kula yule dada jina nimelisahau movie moja kaect na q chief. ingine na jb mwanamke anakiburi anayad ya magari, yuke anatalent naye jaman mtumie, pia mzuri sana, bado sadabonge lol!

Anonymous said...

Loh! Kuna mdau kaamua kuimba kabisa Welcome back Batuli sasa na mimi sijui niimbe maana nimependezwa na alichokifanya Ray kusikiliza watu wanataka Ray ukiendelea hivi utafika mbali sana I'm a businessman najua wateja wangu wanataka nini kupitia shughuli zangu za Import/Export weka malengo sanaa yako isiishie hapa nyanyua miguu yako uvuke mipaka. Binafsi nimependa kumuona huyo Princess kwenye kazi hii ya GLORY OF RAMADHAN nanukuu hapo juu kwa mdau aliyesema Ogopa sana mtu aliyefanya kazi 2 au 3 kisha akakubalika kuna siku atawashangaza ni kweli hili si jambo la mchezo huyu dada hana kazi nyingi lakini anakubalika jiulize WHY

Anonymous said...

Kazi nzuri RJ Batuli yupo juu kapendeza mpaka raha tunasubiri kazi.

Anonymous said...

Kaka Ray ingekuwa amri yangu ningekuamuru sasa hivi weka ndani huyo Batuli yaani oa kabisa kwa sababu anafaa kuwa muke na sio micharuko hiyo mingine.kama akina Irene Uwoya kamutesa ndugu yetu Ndikumana.Sasa huyo Batuli sijui kweli kaolewa kama walivosema wengine.sijawahi muona movie yoyote ila nilivomtazama yeye kwa picha inaonekana ametulia safi. najua huwa mnasema ndoa za macelebrity hazidumu lakini najua kwa huyu binti ndoa itadumu najua nawewe sio mutu wa kujiachia sana na mademu manake kwa umaarufu wako ungekuwa unachapa sana totoz za bongo. safi sana kaka big up.
Mdau toka Rwanda

Anonymous said...

ray ongera na nimefurahi kumuona batuli tena ila ingekuwa vizuri zaidi kama angekuwepo,riyana ally.lakini sio mbaya,

Anonymous said...

Nyie mnaoomba mawasiliano mnataka nini kwa Neshi ovyo

Anonymous said...

WEWE MDAU ULIYESEMA KWAMBA UNGEPENDA UONE WASANII WAKIKE WAITWE GHANA KWAAJILI YA FILIM SASA HUYO WEMA UNAYEMUONA MCHARKUO HUYO NDIO PEKE YAKE ANAYEWEZA KUACT NA WA GHANA COZ ENGLISH INAPANDA HUYO BATULI UNAYEMFAGILIA AENDE SHULE KINGEREZA ZERO,,APIGE BRUSH YA KINGEREZA,,WEMA ANAKUBALIKA NA WALA WEMA SIO MCHARUKO GLOBAL PUBLISHER NDIO WANAMCHAFUA HATA AUNT EZEKIEL HANA UBAYA WOWOTE MNAPENDA KUAMINI WANAYOANDIKA KWENYE MAGAZETI ILA MKAE MKIJUA SIO YOTE YANAYOANDIKWA YANAUKWELI NDANI YAKE

Anonymous said...

INAELEKEA WEMA ,AUNT,IRENE WANAWAKOSESHA USINGIZI,POLE YENU ILA HAWANA MATATIZI MSIPENDE KUAMINI MAGAZETI IKOSIKU MTAJIONA KWENYE MAUDAKU JE NANYIE NIMICHARUKO?

Anonymous said...

I've always believed that if you put in the work, the result will come

Anonymous said...

The Greatest kanzu imekaa mahala pake badili dini bwana uingie kwa kina yakheeeee. Nice couple Neshi yupo bomba nadhani movie itakuwa tishio.

Anonymous said...

Yeeeeeeaaaaaaa, umeamua Kigosi eeeeeeh, good idea ni mambo mapya haya nakupa mkono wa pongezi Neshi (batuli) mzuri itatikisa hii

kighumi said...

Big up ray, i like haya mageuzi ya karne. kaza buti mdogo wangu. god will bless u! pia wachezeshe na watoto pia. then naomba kupata kopi ya "Second wife" nitaipataje nipo dodoma kila ninapoenda uliza hawana.

Anonymous said...

HONGERA RAY

Anonymous said...

Bora umetubadilishia ladha kila movie za rj humkose yule kicheche uwoya haya tunasubiri mzigo huu

Anonymous said...

Wananchi changieni kilichowekwa mezani na ray sio kuponda madada zetu a.k.a Masupastar wa bongo

Anonymous said...

hongera sana kaka naisubirikwa hamu!!

Anonymous said...

KAKA RAY NILIKUWA NAOMBA SANA KAMA MDAU WAKO MKUBWA WA MOVE ZAKO.CHEZA NA WALE WATOTO WALIOKUWA WAKICHEZA MOVE NA SWAHIBA WAKO.USIWAACHE KUWA NAO KARIBU.HATA KAMPUNI YA KANUMBA THE GREAT JITAHIDI KUIFUTILIA NA KUWATUNGIA MCHEZO WAWEZE KUTOA ALBURM HATA WAKIKUPA NA WEWE PACENT FULANI SIO MBAYA KWANI MAMA YAKO (MAMA WA SWAHIBA WAKO)ATAKUSHUKU LIFANYIE KAZI HILI BROTHER.BIG UP WEWE NI MKALI HAKUNA ANAEKUFIKIA BONGO KIDOGO JB.BY MWANAISHA.

Anonymous said...

Hongera kaka tunasubiri mzigo huo

fetty said...

i love nesh she so beautiful i realy love her

Anonymous said...

jamani huyu neshi mzuri sana.jee ray umebadili dini?najua hapo ni ku act tu,ila napenda kujua.maana nasikia mainda alibadili dini,jee vipi na wewe?angalau hii movie,utaangalia na familia maana mavazi ni ya heshima

khalidi athumani said...

big up kaka ray umefanya kazi nzuri sana mungu akubariki na akumpe umri mrefu uendelee kutuburudisha mi ni moja kati ya fans wako yani filamu zako nazikubali ni za ukweli na zinaelimisha sana. is me khalidi.

Anonymous said...

hee kumbe wanaume sometimes mna macho yalotulia sasa mnavyojitiaga kuendekeza uzinzi ni nini, kama mnampenda batuli hivi mnamsifia kwa adabu mngetulia kusingekuwa natabia za hao mnaowachamba, au sasa hivi mna adabu mkimpata tu adabu yote mfukoni, kwa kweli she is pretty na ana innocent personality, bless her

Anonymous said...

Nimesoma comment nimefurahi watu mnavurugana mpaka nashangaa haya wewe uliyesema wema anajua kiingereza yaonekana huna akili timamu rejea historia ya wema kama kiingereza ni deal ilikuwaje akachemka kwenye miss World??? Nakurudisha ktk historia ya marehenu Steven kanumba alipondwa sana kuwa hajui kiingereza lkn alifanikiwa kuitangaza Tanzania kupitia kazi hiyo hiyo ya film huku akitumia broken English mpaka pale alipokizoea use your brain kutoa mada sifia kazi sio lugha au ngono kiufupi waliotajwa hapo wameshuka kutokana na ulimbukeni wao muache ray awashike mikono wanaojitambua la mwisho jiulize film za India wanatumia lugha gani? Ukipata jibu jicheke.

Anonymous said...

Kwa sauti ya kiafande aarooo ray nimemupenda neshi tacadhali tuma contact kwa simu yangu, ha ha haaaaaaaaaaasssssssh! Dugu hii movie yatoka lini? Ooooooh neshi.

Anonymous said...

jembe kazini batuli wa Kanumba, hongera kwa kurudi kwenye game lakini nakupa pole zng za dhati kwa kumpoteza Kanumba wako.

Anonymous said...

Batuli ni nouma.