Sunday, May 27, 2012

AROBAINI YA THE GREAT


Ni mwezi sasa na siku kazaa baada ya kumpoteza ndugu yangu,jamaa yangu ambaye alikuwa mtu wangu wa karibu Marehemu Steve Kanumba(The Great).Na hivi ndivyo arobaini yake ilivyokuwa watu wengi walikuwepo.Namuombea kwa Mungu amlaze mahali pema peponi na amsamehe makosa yake yote, nitamkumbuka sana ndugu yangu,mdogo wangu na nitaendelea kumkumbuka daima katika maombi yangu ya kila siku mpaka pale nami  nitakapokata pumzi yangu ya mwisho, Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba akifuatilia jambo siku ya arobaini hiyo

Mwandishi aliyevalia shati la silver toka Clouds Tv akipata machache toka kwa Mama mzazi wa The Great

Hawa watoto mara nyingi marehemu alipenda kuwatumia kwenye movie zake nao walikuwepo katika arobaini ya kaka yao

 Baadhi ya watu walijikuta wakiwa na majonzi kila baada ya kukumbuka yaliyopita kuhusu marehemu. Dada huyu anaitwa Sandra ni muigizaji wa Bongo Movie

Mama Asha Baraka 

 Shughuri zikiendelea.

 Mwenyekiti wa Bongo Movie Jacob stevin (JB) na Wema Sepetu.mara nyingi upenda kumuita Jb Baba kwa hiyo hapa ni Baba na Mwana

 The Greatest nikiwa makini kufuatilia jambo lilokuwa linaendelea

 Baada ya yote watu waliweza kupata chakula kwa pamoja. Mzee Chilo akipta msosi

 Wadada wa Bongo Movie

Vijana wangu mtamaliza msosi huo angalieni kuna jela

 Baada ya kupata chakula muongozaji wa shughuri hii aliongea machache(Mr.Dino)

 Mr Chilo.

 JB alizungumza mchache kuhusiana na shughuli kwa ujumla.

Baada ya shughuli yote kwa ujumla baadhi wa ndugu,jamaa na marafiki walipata picha za kumbukumbu wakiwa pamoja.

8 comments:

kay said...

samahani hivi ni shughuri au shughuli,wapembuzi wa lugha tusaidiane

Anonymous said...

pole sana kaza kamba sa ww!

Anonymous said...

Ray pole..... naungana na wewe kumuombea Steven kanumba apumzike kwa Amani.Amina

Anonymous said...

bora ulivyoweka wazi kuhusu wema na jb.maana magazeti ya udaku yalishaanza kuandika habari za uwongo

Anonymous said...

maisha yanaendelea,mtaishia kumsema mwenzio anasonga mbele,ray usiwasikilize watu wanao kuvunja moyo

Anonymous said...

mama Asha baraka huo uso ni umri au mkorogo? mbona unatisha sana jamani mkorogo noma

Anonymous said...

HAYA YA MWENZETU YAMEKWISHA SASA TUJIANDAE NA SISI KWANI HATUJUI NI LINI TUTAMFATA YAWEZA IKIWA DAKIKA HII AU KESHO DUNIA NI MAPITO TU

Anonymous said...

YOU ARE GREATLY MISSED BRO...R.I.P S.C.K