Monday, May 7, 2012

HAPPY BIRTHDAY MAMA LORAA


 Mdau mkubwa sana wa Bongo Movie Club Mama Loraa alifanya party ya nguvu ndani ya mjengo wake uliopo maeneo ya Mbezi Tang Bovu, Birthday hiyo ya Mama Loraa iliudhuriwa na mastaa kibao wa hapa Tanzania twende mwenyewe ukajionee

 Davina na Wema wakiwa wamewasili katika sherehe hiyo

Wema na Cloud

 Mahsein Hawazi (Dr.Cheni) akiwa amepiga suti matata sana umependeza kaka

 Jack Wolper niliipenda sana hili vazi lake ni hatari sana aliniambia kanunua dola alfu mbili

Mwenyekiti wa Bongo Movie (JB) akiwa na Hatman Mbilinyi wa katikati na wa Wema Sepetu wakifuraia sherehe hiyo.


 Mama Loraa mwenyewe ndiyo huyo hapo wa katikati mama ongera san kutimiza miaka kapuni hata mimi mwenyewe sijui

 Mama Loraa akiwa kwenye red capet kwa ajili ya kuwakalibisha wageni waalikwa na kupiga nao picha.

 Jenifer Kiyaka (Odama).

 Shilole na Irene Uwoya.

 Mc. Chiki Mchoma

 Muda wa kufungua Shampeni ulifika Jb na Wema ndio waliotufungulia shampeni hizo

 Mainda.

Muda wa keki nao ukafika

 Mr na Mrs Loraa na Baby Madaha(wa  kulia).

 Zoezi la kulishana keki liliaza Mume wa Mama Loraa akimlisha keki mke wake

 Mama Loraa

 Uwoya na Wema wakiteta jambo.

Single  Mtambalike.

 Steve Mengele (The Power).

 Tino wa kwanza akiwa na Juma Chikoka(wa kati) na Jimy Mafufu

 Party ikiendelea.

 The Greatest(Ray).

 The Greatest nikiwa na Baadhi ya wanachama wenzangu wa Bongo Movie.

 Msosi time Loraa alifungua njia ya kwenda kuchukua chakula

Shilole utamaliza msosi huo

 Mtitu na mkewe mtarajiwa

 JB na Dr.Cheni wakipata msosi wa nguvu hiki ni kipenfele muhimu sana kwa ndugu yangu Jb

 Baada ya matukio yote watu walikunywa,walicheza na kufurahi kwa pamoja. 

34 comments:

j can said...

Mmependeza sana sana .Simpangii mtu style ya maisha lakini msisahau maisha ya kesho jamani. Siombei mabaya ila mkumbuke kuwekeza huwezi jua ya kesho. Wolper gauni ya elfu mbili?
Kweli sanaa inalipa Tanzania. Mnapofurahi kumbukeni kulia na maisha ya mwenzenu SAJUKI pia mmchangie mwenzetu kwani hakuna anayejua kesho ataamkaje. Hapo bongo movie mkiamua tu 25 dola hiyo itapatikana fasta.
Mungu awabariki kwa kujitolea kwenu.

Sister canada said...

Ray Najua unafanya mazoezi lakini bado mwili wako ni mnene . Zidisha mazoezi unene sana unakaribisha magojwa japo kibongo kunenepa tunaona eti ni kupatia maisha.
Kama unafanya mazoezi lakini mwili unazidi angalia diet yako labda utakuwa unakula sana. Nakupenda kama mdogo wangu ndo maana nakushauri hili na ninaelewa unene sana sio afya. Kama hicho chakula amepakua JB hapo ni kingi sana kwani naye ana mwili mkubwa jamani. Punguzeni kulakula, Pendeni miili yenu.

Anonymous said...

Nic pics
ila jamani tuseme na ukweli kuna baadhi ya vitu huwa mastaa mnajitakia wenyewe, hiyo gauni ya wolper anasema kanunua dola 2000 (million 3 za tz) hapo lazima sisi walala hoi tutaona mnaishi maisha mazuri, lkn mkipata matatizo mnaomba michango, hapo mlalahoi ataelewa akisoma hii habari??
but big up wazee

big sister said...

Nimependa walivyovaa wenye ndoa nguo za heshima. Ila IRENE UWOYA nguo yako ni kweli inaonyesha huna ndoa na kinyonyo nje.
Wema kapendezaaaaa na wengineo sijui Mainda nk. Hata nguo ya wolper ni nzuri ila si tulisikia kawa mtoto wa KISLAM??? Anyway hata watoto wa KIKIRSTO hawaruhusiwi kutembea mapaja nje.
Hasa cos ilikuwa ni nyumbani kwa watu siyo Pub au beach. Usibanie tafadhali

Bi kidude said...

Davina, Mainda Shilole,Wamependeza sana halafu wanaonekana wako smart pia. Wanaume wote mmeonekana smart pia.
Irene please sitaki kuona hicho kinyonyo nje we si tulikukaribisha kundini??

Anonymous said...

Sorry, kwani huyu Mama Loraa ni nani katika Bongo Movie?

Anonymous said...

wote mmetokelezeyaaaaaaaaaaaa.

Anonymous said...

wote mmetokelezeyaaaaaaaaaaaa.

Anonymous said...

Nanyie kwa kujifedhehesha sasa huyo Owoya ndiyo nini kuacha maziwa nje wakati yameshalala

Tajibeba said...

Anza mazoez ndugu yangu Ray..huo unene haukupwendezii kabisa..those days ulivyokuwa unaigioza Kaole ulikuwa na mvutoooo saiv mvuto wote kwishney!!

Anonymous said...

jamani hawa wanawake wanatabu, sasa huyu Wolper si amesema kawa muislam sasa hayo mavazi gani mchezeeni tu mungu, Irene mpka chuchu zinaonekana jamani kwanini mnakuwa hivyo kwani ukivaa vizuri huwezi kuwa mrembo? hongera Wema uko juu mpenzi

Bi kidude said...

Unabana comment hizo ili uzile? Toa tamko kwamba mtu asicomment.
Unafikiri ujumbe utawafikia vipi wengine hujui comment zinakuonyesha uko vipi kijamii??Kama zingekuwa za matusi yes unatakiwa kubana lakini hata za ushauri hutaki. Ok uzimeze vizuri basi .

Anonymous said...

hata mi pia sipingi ww kuitwa mr.bongo movie, coz i believe ww pia ni mpiganaji na pia innovator wa vitu vingu ww mwenyewe ni shahd wa hili!

WAPENZ WENG WA TASNI WA FILAMU KWA SASA AKILI ZAO NA MAOMB NI JUU YA SAJUKI ANAYESUMBULIWA NA MARADHI..,
Uhusiki wako kwa namna yyte ya msaada unayoijua i.e kama walivyofanya wakina william mtitu..
UJUE INANIUMA SANA UNAFAIL KUJENGA REPUTATION KWENYE JAMII YAKO ilyo na negative perception kwako kwa vitu vidogo tu!

Sijisifu lakini naamin nina mawazo mapana na marefu kuliko hata uliyepost na kupongeza bathday yake!

I.e(mfano wa pili)
Wakt mzee kipara anaumwa kanumba alienda kumchek na kutoa alichoweza na kupost baadh ya ishu kuhusu mzee kipara..

Msani nayekupenda(ray)
Ww hukupost chochote kuhusu kifo cha mzee kipara!

FUNDISHO LANGU
You shud knw the appropriate information to post and at right time even though its ur blogspot, hv ni vtu vidogo sana lakin vina faida kubwa sana katika REPUTATION!
tumia media vizur ww ni prominance personal, iwe electronc, printing, au internet, brain storm your heard bro!

Hivi vtu naviandika pia ndo navyovisomea hapa chuon kwetu!

Kiufup mi nakupenda sana ndo maana nafanya kaz isiyonisaidia
Contact me!
b52emmer@gmail.com
Naitwa emmer matutu

Anonymous said...

jamani raymfanya mazoezi.kulingana na kazi zenu,unene haufai.mnawaona ma actor wa ki negeria wa kiume walivyo fit?muone mwenzako single mtambalike na dokta cheni.wana miili mizuri sana.uso umekuvimba,haipendezi.jackline wolper nae amependeza.lakini hio bei ya nguo aliotaja mmh

Anonymous said...

nesh mamaa umependeza lakini umenenepa sana pungua kidogo na urudi katika rangi yako ya asili.

Anonymous said...

ray unabania comment kwa nini?

kay said...

shilole unapendeza sana ukiwa hujavaa wigi,angalia picha yako chini ukiwa ndani ya gari umependeza sana tu,na angalia picha ya hapo juu ukiwa umevaa wigi halijakutoa kabisa shosti,ushauri tu dada

Anonymous said...

WEMA MTAMU JAMANI.KAPENDEZAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA KUPITA KIASI

Anonymous said...

wema sikuhizi anapendeza jamani uliempata usimwachie, tulia heshima yako irudi wema, of-course wote mko pouw

Anonymous said...

Unahitaji mtu akupe darasa kuhusu utumiaji wa media. Nakubaliana na mdau hapo juu aliyeongelea kuhusu mwenzenu Sajuki anayeumwa. Ungetakiwa hiyo ndio kitu cha kwanza kupost na sio kushadadia birthday na nguo za dola 2000 wakati mwenzenu anahitaji msaada. Kweli Kanumba was a different person ndio maana hatotomsahau daima hadi na sisi tufe.

Anonymous said...

JAMANI WEMA KAPENDEZA SANA TENA ZAIDI YA SANA NAMPENDA WEMA SANA SHE SO BEUTIFULY N INNCENT,,WOLPER MWENYEZI MUNGU AKUZIDISHIE KWAMCHANGO WAKO ULIMTOLEA SAJUKI NAKUPA KISS KUBWA SANA NA OXOXOXOXOXOXOX WOTE MLIOCHA NGIA MUNGU AWABARIKI,,IRENE NAKUPENDA SANA MM NI FANS WAKO MKUBWA ILA PUNGUZA KUVAA UCHI JAMANI HAIPENDEZI KABISA,,RAY PUNGUZA UNENE KAKA YANGU,WEWE N HB UNALIJUA HILO?SASA UKIWA KIBONGE UTAKUA BAYAAAAAAAAAA

Anonymous said...

haya wewe mama Krish ndo nini kuanika chakula cha krish hadharani

Anonymous said...

kaka blog yako iko passive sana kama ulivyo...... lete mijadala tusidianee mfano.. unaweka ovie zako tatu hapa afu unauliza ipi umecheza vizuri na kwa nini watu wanpenda kujua zaid wau wanpenda nn na hawapen nini sio lazima tukio fulan ndo upost
emmer matutu

zajir said...

Ujinga gani huu...!!!! Hivi nyie kazi yenu ni kuelimisha jamii au kupotosha??? Mnakaa uchi, movie zenyewe za sasa hivi kama vile lengo lenu ni kufundisha ufuska kwa wale wasioujua. Serikali wanajitahidi kupiga vita ukumwi, kumbe kuna watu wanajiita wasanii kazi yao ni kuhamasisha ngono... Serikali yetu lazima iliangalie jambo hili kwa umakini, la sivyo ni sawa nakumpigia mbuzi gitaa. Watu wazima ovyooooooooo....

Anonymous said...

mna tabia ya kupenda wapenda fedha hamna lolote mama lolaa ninani kwenu?

Anonymous said...

MI SI SHABIKI WA RAY ILA ANACHOKIFANYA NI SAHIHI COZ HII NI BLOG YAKE....KAMA KUNA MATUKIO MNAONA HAJAYAAPOST NI PREFERENCE YA MTU NA NYIE ANZISHENI BLOG ZENU MPOST MNACHOKIPENDA KAMA YEYE ANAVYOFANYA.....
ILA NA RAY IELEWE MITAA BAADA YA KUIELEWA SANAA........USILEWE SIFA ZA MAPEMA.....FANYA KWELI ENTIRE UNIVERSE YA BONGO MOVIE UONEKANE SHUJAA KAMA ZAMANI.....MI NILIKUSHABIKIA ZAMANI ILA NIMEGUNDUA UMEWEKA HAPPY MBELE SANA KULIKO MATATIZOOO...
SAWA UNA HAKI YA KUHUDHURIA SHEREHE ZAKO.....LAKINI JE UMEMCHANGIA SAJUKI?

Anonymous said...

jamani wema mzuri kapendeza sana lv you wema

Anonymous said...

sawa jeuri ya pesa birthday kama harusi tuachane na hayo ingependeza mama loraa angekuwa amepiga hata picha na watoto au ndugu waliobaki maana mwanae mmoja yupo mbali sawa kama hamumjui ni yule msanii anayejulikana kama stan boy au alishawi kushirikishwa na eastcost enzi hizo ila all in all imependeza

Anonymous said...

kwa kweli Wema sina la kusema juu yako umependeza sana we ni nzuri hata ukitokelezea na kaniki wa2 watakukubali tu umependeza sanaaaaaaaaaa

Anonymous said...

mi sijaone kitu kwa wolper nguo ni nzuri km yeye mwenyewe anavyooina ila haijampendeza kabisa hongera wema

Anonymous said...

KWA UNENE HUO RAYA SIJUI KM UTAPATA MWANAMKE KWELI NANI ANATAKA MATATIZO HUNA PUMZI KAKA

Anonymous said...

HIVI KWANINI WEMA HUTAKI KUTULIA UNAJIJUA WEWE KM NI BINTI MZURI SANA AMA KWELI MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI WEMA UMEPENDEZA SANA

Anonymous said...

MI NATKA KUJUA HIVI UWOYA KWELI BADO YUKO NA MUMEWE KWELI MANAKE..............NAONA ANATAFUTA MUME NYINGINE BIASHARA NJE NJE

Anonymous said...

HIYO NGUO YA MADOLA MBONA PALE KARUME KWENYE MITUMBA ZIPO HIYO YOTE DANGANYA TOTO WOLPER