Tuesday, June 19, 2012

UZINDUZI WA FILAMU YA RICHIE

Kama kawaida ya Bongo Movie utengano kwao ni dhaifu na umoja kwao ni nguvu hii ni kauli mbiu ya Club ya Bongo Movie Unit waliongozana na mmoja wa wanachama wa Bongo Movie bwana Richie msanii nguli wa tasnia ya filamu bongo kwenda kuzindua sinema yake inayokwenda kwa jina la Chaguo Langu ndani ya merarani..

Wasani wa bongo movie wakiwa ndo wamewasili katika Air port ya Moshi wakitokea Dar es salaam wakijiandaa kwenda Mererani ambao ni Irene Uwoya wa kwanza kushoto,Shilole wa kati na Hatman Mbilinyi wa kulia.

 JB mwenyekiti wa Bongo movie.

 Steve Nyerere.

Single Mtambarike alikuwa mwenyeji wetu kwenye safari hiyo. 

Vile vile tuliweza kukutana na washiliki wa Miss Kilimanjalo wa mwaka 2012.

Wasanii pamoja na mamiss
walipata mualiko wa kupata kifungua kinywa katika mgahawa flani hivi na hapa mmiliki wa mgahawa huyo akitoa shukrani zake kwa wasanii na mamiss kwa kukubali kuitikia wito wake

Sasa ulifika muda wa kuelekea Mererani kulikuwa kuna watu wengi sana wakitusubili kwa hamu kubwa.

 Jb akisalimiana na wananchi wa Merarani

 Watu wa Mererani walifurahi sana walipotuona na walitupoke vizuri.
 Hapa ni machimbo ya Merarani na hao watu mnaowaona ni wachimbaji wa madini ya Tanzanite maarufu kama (Wanaapolo)

 Tuliweza kutembelea baadhi ya maeneo ya migodi iliyoko maeneo hayo.

 Tukiwa ndani kwenye shimo mojawapo.

 Matembezi yaliendelea.

Tukiwa na wanaapolo machimboni..

 Tukipata chakula pamoja na wenyeji wetu.

Misosi ya kumwaga.

 Ulifika mda wa kwenda kuzindua filamu yetu ya Chaguo Langu tukiwa na Bongo Movie, The Greatest nikiongoza Jahazi hilo katika ukumbi wa songa mbele ulioko Maeneo ya Mererani.

 Ratiba zikiendelea.

 Wana Bongo movie wakisalimia mashabiki waliofika ukumbini hapo

 The Greatest.

 Mda wa show ulifika Richie aliweza kutufungulia show yetu.

 Jb bonge la bwana akipiga mastaili ya kufa mtu

 Ulifika muda wangu wa kufanya mambo niliwainua mashabiki wengi kwenye viti kwani mimi ni mkali sana kwenye mziki wa mayenu

 Nikifanya mambo na Steve Nyerere

 Mamiss wa Kilimanajaro mwaka 2012 nao walipata muda wa kusalimia wananchi wa Merarani pia nitawaletea matukio ya Miss Kilimanjaro kwani tulialikwa katika mpambano huo wa kumtafuta mlimbwende wa miss Kilimanjaro 2012

8 comments:

Unknown said...

hahahahaa nimechekaaa...mlipendeza hongereni na mzidi kudumisha umoja wenu

Anonymous said...

aiseee kama ndo mapinduzi nayoyategemea toka kwako umeniangusha yaaani kifupi nioga bila kuvua nguo... salama alikwa#bia fanya kai watu waappriciaate na ndo watastop kuchonga....sasa broo harakati ndo hizo dah plzhuna hta marafiki kwenye industry film nigeria ufanye connection ufanye mwendelezo wa kanumba na ile ishu ya kufanya movie china vp tena hizo ndo habari tunataka kuziona sio hizo japo ni vizuri kushirikiana nao lakini unatakiwa uendeleee kuwa kwenye ile ile level ya kanumba m ya kuwaza hollwood na nolly wood jamani ww ni msann mwenye phisical apperance ya kucheza movie kali na za aina yote this you time take it and shine.. in short i sid all this becoz i love you z
sa hii siandiki tena jina nishaona hunisomi vizuri wala kukosinder

Anonymous said...

Woooow I like it. I really like it but hatujawaona wasanii wa kike Where is Batuli? Sisi Mkija huku muje nae we love her saaaaana! Mupe salamu. Its me Mrs,Kyamba

Anonymous said...

Hongereni saaaana kwa kuwa na ushirikiano mzuri, umoja ni nguvu msitupane ipo siku mtafika pale mnapopakusudia, hongera sana Ray kwa kutupa matukio mbalimbali ya shughuli mzifanyazo sisi watanzania wa UK tupo pamoja nanyi My contact is Mr_ Chief2006@hotmail.co.uk karibuni mfanye movie huku tutawaunga mkono lakini katika picha zako hatujamuona Batuli wa Kanumba where is she?

Anonymous said...

Nice pic kigosi ila mbona mlienda kidogo? Wengine wapo wapi? Salam nyiiingi kwa wasanii wote wa bong movie Tz especially Batuli.

Anonymous said...

mambo ray habari za kazi nimependa sna kaka kwa sas unajichanganya kila sehemu naona kwa sasa umeelimika zaidi ila nakuomba jaribu kukaa na wadada zako wa bongo movi kwakweli ayo mavazi ya irene uwoya sio mazuri uku moshi ni gumzo kwa kila mtu kwanini uyu dada awezi kujiheshimu jamn si bora atembee uchi tujue moja ndo ayo

Anonymous said...

mwambie4 steve nyerere aache kupaka hayo mafuta amekua mbaya yanamcream..

Anonymous said...

Irene kama changudoa jamani au ndio anatafuta pesa kwa style ya kuvaa nusu uchi? Mwambie amechuja akamuangukie Ndikumana amepoteza nuru kwa majanaba ya wanaume wa Tz