Saturday, June 30, 2012

UZINDUZI WA SOBBING SOUND NA WATOTO YATIMA

Hatimaye mzigo wa Sobbing Sound umeingia mtaani kwa aina yake baada ya kaumua kwenda kuizindua na watoto yatima wa kituo cha Maunga kilichopo maneno ya Kinondoni studio, Kwanini nimeamua kufanya hivi wadau ni kwa sababu nimeguswa na jinsi wanayoishi watoto yatima katika mazingira magumu ili ni jukumu la Watanzania wote kuanza kuguswa katika hili maana hapa duniani sisi ni wapangaji tu makazi yetu ni kwa Mungu Baba sasa unapopata kidogo jaribu kuwafikiria na wale waliokuwa na maisha magumu, yani tugawane umasikini. wadau sikuwa na kikubwa sana ila nimejitolea pale nilipoweza kubarikiwa na Mungu Baba unaambiwa kuwa kama utoweza kushukuru kwa kidogo basi hata ukipata kikubwa pia utakuwa mgumu kumshukuru yule aliyekuwezesha kukupa kipato hicho...

 
Hivi ni baadhi ya vitu nilivyowapelekea watoto wa kituo hicho wadau kutoa si utajiri bali ni moyo na nimeamua kila sinema yangu inapotoka basi lazima nirudishe shukrani zangu kwa Watanzania wa hali ya chini nitaanzia Dar es salaa na baadaye mikoani wadau ..

Watoto wa kituo hicho wakiwa wametulia kufuatilia kinachoendelea..

Waandishi wa habari kutoka vituo tofauti  walikuwepo kuchukua habari kama kawaida ya wanahabari panapokuwa kuna tukio.

Pritesh toka Steps kampuni ya usambazaji hapa nchini alikuwepo kunipa tafu katika jambo ili la kuwasaidia watoto yatima..The Greatest(Ray) nikiwa nimewasili katika kituo cha watoto yatima cha Maunga nikimsikiliza mama mlezi wa kituo hicho.
                                  
Mama mlezi wa kituo hicho akiongea machache pamoja na kunishukuru. 

Nami nilipata fursa ya kuongea ya kwangu.

Zoezi la makabhiano yalianza kama ifuatavyo, hapa nikimkabidhi Mama mlezi kiroba cha unga..

Mambo yakiendelea...

Nikiendelea na taratibu za kutoa msaada.

 
Niliweza kutembelea maeneo wanapolala ndugu zangu na kama mnavyoona wadau tunahitaji kujitoa kuwasaidia ndugu zetu..


 

Na hichi ndio choo chao embu angalieni jamani hii n hatari sana kama utakuwa na chochote ama umeguswa kusaidia basi tunaweza kuwasiliana.

Baada ya matukio yote nilipewa nafasi nyingine ya kusaini kitabu cha wageni.

Niliweza kupata picha ya pamoja na watoto hao.

Hapa nikiongea na vyombo vya habari..

Nikipokea shukurani yao.


`Nilifurahi sana kwa kupata nafasi kubwa ya kufika katika kituo cha watoto yatima  na hapa wakinisindikiza.

9 comments:

Anonymous said...

MASHAALAH!! umefanya jambo zuri sanaa Alah akuongeze riski yako, uendele na moyo mzuri km huo
hicho kibaby ulichokibeba kimekupendeza km mwanao hahaha

Anonymous said...

HONGERA SANA TENA SAAAAAAAAAAAAAAAANA UBARIKIWE SANA YAANI RAY UNAROHO NZURI SANA NAKUPENDA SANA MDOGO WANGU ENDELEA KWA MOYO HUOHUO,,STAY BLESSED,,MDAU HOLLAND

Anonymous said...

Habari Ray umefanya kitu kizuri sana ila wasi wasi wangu mbona naona kama na Lady jay dee na yeye alipeleka msaada kituo hicho hicho week hii au macho yangu kama ni hivyo basi kutakuwa na kosa kidogo muwaaangalie na wengine kuna kituo kipo boko ccm juu kinahitaji msaada sana

Anonymous said...

hongera sana ray mm nimenguswa sana chuo hicho jamani km kutakuwa na mpango wa matengenezo tupo pamoja mm niko london sina kikumbwa icho kidogo tutashirikiana

Anonymous said...

wabongo wacheni umaskini ndoo ya mafuta,mchele kilo 10,thamani yake hata laki haifiki mkawaite na waandishi wa habari misaada msotoa kimya kimya sio kukaa na kujitangazia kwenye vyombo vya habari au mnataka riziki kupitia hapo?kama mmeguswa kwanini msiwaongezee hv vitanda?na kukarabati choo hicho?acheni hizo mnawadhalilisha hao watoto buree na tena mnajitia mtu akitaka kusaidia awasiliane nanyi wakati kituo kinajulikana kilipo mtu si ataenda kimyakimya sio kama nyie limbukeni wa maisha ht na mungu hapendi namna hiyo misaada gani hv badilikeni!!!!!!!

Anonymous said...

afadhali umeonyesha nia ya kuendeleza yale aliyokuwa akitenda swahiba wako Kanumba, hongera endelea na moyo huo huo leo umeanza na kidogo kesho utaongeza keshokutwa na zaidi na zaidi, ubarikiwe san

muke ya mungoni{ireland} said...

mungu akutangulie kwa kila jambo lako.

Anonymous said...

Ubarikiwe sana kaka yangu uendeleye na moyo uyo uyo kwa sababu ata neno la Mungu linatufundisha ivyo Mungu akubariki sana lea Lila ufanyalo.

Anonymous said...

Nawengine .mjitokeze tujitokeze .silo ray mdogowangu .