Saturday, June 30, 2012

UZINDUZI WA SOBBING SOUND NA WATOTO YATIMA

Hatimaye mzigo wa Sobbing Sound umeingia mtaani kwa aina yake baada ya kaumua kwenda kuizindua na watoto yatima wa kituo cha Maunga kilichopo maneno ya Kinondoni studio, Kwanini nimeamua kufanya hivi wadau ni kwa sababu nimeguswa na jinsi wanayoishi watoto yatima katika mazingira magumu ili ni jukumu la Watanzania wote kuanza kuguswa katika hili maana hapa duniani sisi ni wapangaji tu makazi yetu ni kwa Mungu Baba sasa unapopata kidogo jaribu kuwafikiria na wale waliokuwa na maisha magumu, yani tugawane umasikini. wadau sikuwa na kikubwa sana ila nimejitolea pale nilipoweza kubarikiwa na Mungu Baba unaambiwa kuwa kama utoweza kushukuru kwa kidogo basi hata ukipata kikubwa pia utakuwa mgumu kumshukuru yule aliyekuwezesha kukupa kipato hicho...

 
Hivi ni baadhi ya vitu nilivyowapelekea watoto wa kituo hicho wadau kutoa si utajiri bali ni moyo na nimeamua kila sinema yangu inapotoka basi lazima nirudishe shukrani zangu kwa Watanzania wa hali ya chini nitaanzia Dar es salaa na baadaye mikoani wadau ..

Watoto wa kituo hicho wakiwa wametulia kufuatilia kinachoendelea..

Waandishi wa habari kutoka vituo tofauti  walikuwepo kuchukua habari kama kawaida ya wanahabari panapokuwa kuna tukio.

Pritesh toka Steps kampuni ya usambazaji hapa nchini alikuwepo kunipa tafu katika jambo ili la kuwasaidia watoto yatima..The Greatest(Ray) nikiwa nimewasili katika kituo cha watoto yatima cha Maunga nikimsikiliza mama mlezi wa kituo hicho.
                                  
Mama mlezi wa kituo hicho akiongea machache pamoja na kunishukuru. 

Nami nilipata fursa ya kuongea ya kwangu.

Zoezi la makabhiano yalianza kama ifuatavyo, hapa nikimkabidhi Mama mlezi kiroba cha unga..

Mambo yakiendelea...

Nikiendelea na taratibu za kutoa msaada.

 
Niliweza kutembelea maeneo wanapolala ndugu zangu na kama mnavyoona wadau tunahitaji kujitoa kuwasaidia ndugu zetu..


 

Na hichi ndio choo chao embu angalieni jamani hii n hatari sana kama utakuwa na chochote ama umeguswa kusaidia basi tunaweza kuwasiliana.

Baada ya matukio yote nilipewa nafasi nyingine ya kusaini kitabu cha wageni.

Niliweza kupata picha ya pamoja na watoto hao.

Hapa nikiongea na vyombo vya habari..

Nikipokea shukurani yao.


`Nilifurahi sana kwa kupata nafasi kubwa ya kufika katika kituo cha watoto yatima  na hapa wakinisindikiza.

Sunday, June 24, 2012

UZINDUZI WA WEMA SEPETU


 Hongera Wema Sepetu kwa kuandaa shughuli kubwa iliyokusanya mastaa wengi wa tasnia ya movie bongo pamoja na bongo fleva katika uzinduzi wa cinema mpya ya Wema inayokwenda kwa jina la Super Star, nakupa hongera tena kwa kuweza kumleta msanii mkubwa wa kike kutoka Nollywood Omotola kwa ajili ya kuweza kushuhudia uzinduzi wa cinema hiyo ya Super Staar

Hapa tukiingia ndani ya ukumbi wa Kempick ulipofanyika uzinduzi huo wa Super Star...

 
 Irene paul kijana niliyemuibua katika ulimwengu wa movie ni tunda langu ili sasa yupo ndni ya Red Carpet akipiga picha bongo siku hizi kama ulaya tu

The Power naye akiwa ndani ya Red Carpet

 The Greatest.

Pozi la The Greatest

 
 Kupa.

 Hatman Mbilinyi.

 Shilole wa kwanza kushoto  akiwa na Mainda wakihojiwa machache kuhusu uznduzi wa bonge la movie la Super Star.

 Ommy Dimpoz.

Vijana mpendeza saaaaana

 
 Beny Kinyaiya.

 The Greatest nikiwa na Richie na Barnaba.
                                     
Mtitu akiwa na Mwana FA na Dimpoz.

 Ben Kinyaiya,Hartaman pamoja na Chalz Baba mwanamuziki wa Mashujaa Band...

                        
A.Y mwanamuziki wa kizazi kipya

                                              
 Izzo Bizness.

Vijana wa Bongo Movie 

The Power akiwa na Mama Loraa.


 Tht show

Jenifer Kyaka(Odama) akiwa na The Greatest bata likiendelea.
 
Ulifika muda wa kuangalia Movie ya Wema Sepetu(Super Star).


Mambo yakiendelea..

Wema Sepetu akifuatilia cinema yake
 Hatari mchezo umeanza
 

Baada ya watu kuangalia movie burudani ikaendelea, hapa lina akipiga show ya nguvu

Thursday, June 21, 2012

SOBBING SOUNG JUNE 28


Mzigo uliokuwa ukisubiliwa kwa hamu Sobbing Sound sasa unaingia sokoni rasmi tarehe 28, nategemea kwenda kuzindua na na kinanani? nitawajulisha wakati ukifika wadau

The Greatest nikiwa na vijana wangu kazini bila hata kuchoka.

Wanaume kazini

Hiki ni kimojawapo cha kifaa kinachofanya tuweze kufanya kazi kwa ufasaha zaidi.

 Vijana wakiwa kazini.

 kazi ikifanyika.

Irene na Sajent on set

 Jamani wadau wangu ebu angalieni vijana wanavyofanya kazi.

 Nikiwa naangalia picha kwenye monitor yangu ndogo kwa umakini mkubwa

 Sobbing Sound ni movie nzuri sana ambayo crew ya Rj Company waliitendea haki kwa kufanya kazi kubwa sana.