Thursday, March 28, 2013

TWISTED

Cover la Twiste ndio litakuwa na muenekano huo wadau wa filamu Tanzania.

JOHARI NDANI YA BAD LUCK

Blandina Chagula amaeamua kuja na mzigo wake binafsi unaokwenda kwa jina la Bad Luck, katika mzigo huo yumo Miss Tanzania wa Mwaka 2011&2012 amefanya Vitu Vikubwa sana ndani ya mzigo huo wadau, Johari amesema kuwa  sio mzigo wa kuukosa lini utatoka? bado kidogo mpaka itoke Twisted. ndani ya mzigo huo wa Bud Luck niliamua kupumzika na kuwaachia vijana waweze kufanya kazi bila ya kuwepo mimi maana kuna leo na kesho... hao hapo juu ni staff wa RJ COMPANY..

 Miss Tanzania aliyevua taji lake mwaka jana anakwenda kwa jina Saraha, kama nilivyowaambia wadau huyo mrembo kafanya mambo makubwa katika sinema hiyo ya Bad  Luck..

 Batuli naye yumo ndani ya nyumba ni hatari sana..

 Mautundu ya Light Man wangu Samu Shoo yakiendelea kama kawaida ya RJ

 Camera Man wangu wa kwanza kabisa kuanza kufanya naye kazi Razack Ford wa kushoto pamoja na Camera Man wangu wa sasa Farid Uwezo wakiwa pamoja kuhakikisha mambo yanaenda sawa kabisa .


Batuli akiwa On Set..

 Wadau wa RJ COMPANY wakiwa pamoja na Blandina Chagula (Johari).

 Vijana kazini.

Kazi ni ngumu sana Location wadau nyinyi tizameni tu kwenye tv lakini kunakuwa na kazi ngumu sana maana sio kazi ndogo kabisa tutieni moyo   msituvunje moyo mapambano bado yanaendelea..

Dori likifungwa ili kupata picha inayotembea, kama ulaya bongo sasa hivi vifaa vyote vipo watu washindwe kufanya kazi tu.

SEND OFF

Jana ilikuwa ni Send Off ya mke mtarajiwa wa Idrisa Makupa (Kupa) iliofanyika maeneo ya Mbezi ilikuwa ni shughuli ndogo tu ya kumuaga binti yao anayekwenda kwa jina la Mary wa kushoto pamoja na mpambe wake wakiwa wanameremeta kama nyota harusi yenyewe itafanyika siku ya Jumamosi ijayo katika ukumbi wa new urafiki uliopo maeneo ya Shekilango..

Jimmy Mafufu akiwa pamoja na Mke mtarajiwa wa Kupa, Huyu naye ni bwana harusi mtarajiwa maana hawa mabwana wameamua kufunga ndoa kwa pamoja na ukumbi mmoja. itakuwa hiyo Jumamosi ijayo Hongereni sana vijana wa Bongo Movie Unit.

 Kupa na Mkewe mtarajiwa..

 Muda wa msosi ulifika..

 Cloud 112 wa kushoto,  Msanii mkubwa Nchini Tanzania naye alikuwepo kumpa sapoti kijana wake.

Picha ya pamoja.

Mtitu Mkurugenzi wa kampuni ya 5 Effect akiwa pamoja na mkewe wakipata msosi.

Mambo yakiendeleaaa..

Mwenyekiti wa Kamati wa harusi hizo bwana Mauma akiwa pamoja na katibu wake Mama Loraa Masai..

 Ratiba za chakula zikiendelea.

Kupa Hongera sana kijana kwa kuamua kuvuta jiko la kuliweka ndani si kitu kidogo unastahili sifa kijana Mungu awabariki muishi maisha yenye upendo na amani tele..

Thursday, March 21, 2013

SAMSUNG

Nilipata mwaliko toka kampuni ya Samsung nami sikusita kwenda walikuwa wanazindua Camera yao mpya inayokwenda kwa jina la Samsung Camera yenye ubora mkubwa sana na ina internet ndani yake yani unapiga picha na hapo hapo unaproad jamani kweli Dunia imekuwa kijiji embu tucheki mambo yalivyokuwa..

Hapa tukipata picha na kijana wangu Dulla mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo

Dulla

 Ben Kinyaiya..

 The Greatest nikisalimiana na Raqee Mkurugenzi wa kampuni ya I Vew Media maarufu kwa utengenezaji wa macover ya filamu Tanzania..

 Mboni na Dulla wa Planet Bongo kwenye pozi..

 Dj Mafufu na The Greatest.

 Ratiba zikiendelea.

 Ulifika muda wa droo ya samsung atakaye shinda atapatiwa Samsung camera mpya.

 Dulla akijalibu zali lake.

Mboni Masimba wa kulia akuwa nyuma katika upande wa misosi na vinywaji..

picha ya kumbukumbu, vijana wangu mmependeza sana..

Amani kwa Dj Choka..

Pozi la mwaka ilo..

Tukiwa makini kufuatilia mambo ya Samsung yanavyokwenda wadau..

 Vijana wakikandamiza misosi

 Mmoja wa mshiriki katika droo..

The Greatest na Shafii Dauda Mtangazaji wa kipindi maarufu cha michezo toka Clouds Fm

 Izzo Bussines mwanamuziki wa kizazi kipya akiwa pamoja na kaka yake  The Greatest..

 Quick Racka msanii wa kizazi kipya.

Mshindi aliyejishindia Camera mpya ya Samsung.

Tuesday, March 19, 2013

RWANDA MOVIE AWARDS 2013

Wadau kama nilivyowaandikia mwanzo kwamba tulikuwa Rwanda kwa ajili ya kutoa tuzo zinzoitwa Rwanda Movies Awards, hawa jamaa wako makini sana katika swala zima tuzo hii mi kumfanya msanii haweze kutengeneza kazi nzuri ili apate tuzo maana tuzo ndio kipimo cha msanii kujua uwezo wake umefika wapi, tuzo zenyewe ndizo hizo hapo juu kama mnavyoziona wadau wa tasnia ya filamu Afrika wacha tuone mambo yalivyokuwa..

Maandalizi yakifanyika kwa mrembo wetu Dada Irene Uwoya kabla ya kwenda sehemu ya tukio..

Hapa tukiwa Serena Hotel ya Rwanda lilipofanyika tukio ilo la utoaji wa tuzo kubwa zinazofanyika kila mwaka..

JB

JB na Uwoya kwenye pozi..


The Greatest nikiajiandaa kuelekea ukumbini.


Jb akiwa pamoja na Uwoya ndani ya Land Cruser..

The Greatest pamoja na King Majuto pia wakiwa ndani ya Land Cruser hakuna kubanana ni wawili wawili tu, jamaa walitupa eshima kubwa sana ..

Tukiwasili kwenye ukumbi wa SERENA HOTEL..


Tukielekea sehemu ya tukio..

Watu walikuwa ni wengi sana si unacheki mwenyewe bana mimi wala sina la kusema yani watu wa Rwanda wanawapa sapoti kubwa sana wasanii wao wa Nchi yao ili ni lakuigwa na nyinyi ndugu zetu Watanzania..

JB alikuwa wa kwanza kuingia ukumbini..

King Majuto akiingia ndani ya ukumbi.

Wadada wa Kinyarwanda walikuwa ni wakumwaga..

Irene Uwoya naye akiingia kwa mbwembwe nyingi sana

The Greatest nilikuwa wa mwisho kuingia..

Mambo yakiendelea..


Huyu dada wa kulia yeye alichukua tuzo ya msanii anayependwa kuliko wasanii wote Rwanda..

Mmoja wa wasanii wakubwa wa Rwanda ni huyu jamaa mwenye tai nyekundu yeye alichukua tuzo ya msanii anyependwa kwa upande wa wanaume..

Baadhi ya wasanii wa Rwanda..

Anaitwa Jackson ni Mwenyekiti wa tuzo hizo..

Watu walikuwa wengi sana..

Mwenyeji wetu huyo wa Rwanda yeye ni mwanajeshi alipewa jukumu la kutulinda..

Tuko makini..

Kambarage toka kampuni ya Steps pia alikuwepo..

Majuto akiongea machache..

Ratiba zikiendelea..

Ulifika muda wa The Greatest kutoa Tuzo..

Msanii bora wa kike ndiyo huyo hapo wadau..

The Greatetst nikimkabidhi tuzo mwandada huyo aliyeshinda kuwa msanii bora wa kike..

Nikiongea machache..

Jb pia akiongea machache na yeye..

JB akikabidhi tuzo..

ulifika muda wa Uwoya kwenda kutoa tuzo..

Akisubili muhusika kufika...

Akimkabidhi tuzo msanii bora wa kiume..

 Msanii wa kiume anayependwa Rwanda akielekea kuchukua Tuzo yake..

 The Gtreatest nikimpa hongera jamaa..

Akikabidhiwa Tuzo yake..

Akishukuru watu waliompigia kura..

Mmoja wa Warembo wa Rwanda naye akishukuru watu waliompigia kura..

Warembo wa Rwanda..

Hili kombe ni kwa ajili ya Filamu Bora ya Mwaka..

Wakishangilia kwa ushindi walioupata, hawa ni baadhi ya washiriki wa movie hiyo walioshinda.

Picha ya kumbukumbu.

Irene Uwoya akiojiwa mchache na waandishi wa habari..

Huyu Mama alikuwa ananifuta viatu kwa nguo zake uku akilia kwa uchungu baada ya kuniona kwakweli hawa watu wa Rwanda wana upendo mkubwa sana kwa wasanii..

Mdau wangu akilia kwa furaha..

Mambo yalikwisha na watu kuendelea na mambo mengine hivyo ndivyo mambo yalivyokuwa...