Sunday, January 29, 2012

DSTV SO MUCH MORE

 Nilipotua tu bongo nilipata mualiko toka kampuni ya Dstv so much more,Dhumuni la mualiko huo nikupata mafunzo ya Video Production kwa ujumla wake mimi kama mwakilishi wa wasanii wote waliopata mualiko huo tunasema asante sana kwa kampuni ya Mult choice kutuletea wataalam kutoka South Africa na kupata mafunzo ya kutosha kwa kweli tulipata vitu muhimu sana ambapo awali havikuwa kichwani mwaetu, hatuna cha kuwalipa zaidi ya kumwachia Mungu wa Isack na Yakob kufanya kazi yake.

 Huyu jamaa wa katikati anaitwa Adam Juma ni mkurugenzi wa kampuni ya Visual Label Next Level ni maarufu sana katika swala zima la muziki wa bongo fleva, Yeye ndiye alieleta vifaa vyake kwa ajili ya practical, mara ya kwanza ulipokuja uongozi wa Mult Choice walikuja kutusikiliza sisi wasanii wa Tanzania tuna matatizo gani ndipo tulipowaambia kuwa tunahitaji kupata mafunzo na ndipo wakaamua kutuletea wataalam hao, na sio sisi tu tuliokuwepo katika mafunzo hayo, bali walikuja wasanii na maproducer kutoka Kenya katika mafunzo hayo yani yalikuwa ni muhimu sana kuliko hata pesa kwakweli tumejifunza mengi tegemeeni makubwa sana toka kwetu kwa sasa maana vifaa vya kutosha tunavyo na elimu ya kutosha tunayo sasa wadau mnategemea nini hapo kama si kula chakula bora

Hapa tukipata chakula cha mchana kushoto kwangu ni producer kutoka Kenya

 Mambo yakiendelea huyu dada naye ni producer toka Kenya tukipata misosi na kubadilishana mawazo walijifunza vitu kutoka kwetu nasi tulijifunza kutoka kwao ilikuwa ni semina wa siku tatu

 Pia tulikuwa na wawakilishi toka kampuni ya Pili Pili kulia kwangu

 Kama  kawaida jamani kijana aliomba kupiga picha na kusema akirudi kwao hawataamini kama alikutana na Ray The Greatest na ndio maana akusita kupata picha ya kumbukumbu

 Mama na Mwana Monalisa na Natasha kushoto

 Picha ya pamoja

 Watu wakipta mapumziko kidogo kwa kupata chai na baadaye kurudi katika darasa

 Mambo yakaanza hapa tulikuwa tunafundishwa jinsi ya kushika boom ili kupata sauti nzuri, mwenye flana ya orange ndiye alikuwa mwalimu wetu

 Mambo yakiendelea camera 7D ya ukweli mbele yako

 Safi sana

 Hapa tukipata mafunzo ya taa ili kupata mwanga safi katika sinema zetu

 Hapa tukielekezwa jinsi ya kupata engle nzuri katka uchukuaji wa picha tukiwa location

Hiki ni kibaoa muhimu sana wakati wa shooting

POLE BLANDINA CHAGULA

 Msanii nguli wa filamu Tanzania Blandina Chagula (JOHARI) aliponea chupuchupu kifo katika tundu la sindano baada ya kupata ajali mbaya iliotokea maeneo ya ubungo mataa akielekea ofisini kwake,Lakini yeye anasema gari sikitu kwa kuwa ametoka salama katika ajali hiyo anamshukuru sana Mungu sifa na utukufu zirudi kwake hayo yalikuwa maneno ya Dada Johari, kama unayoiona gari ya mwanadada huyo ilivyoharibika vibaya

 Cheki wewe mwenyewe ni hatari sana

 Kwa karibu sana

wadau hiyo ndio hali halisi 

Mwanadada mwenyewe ndiyo huyu, Dada mashabiki wako wengi wanakupa pole na wamekusii sana uwe makini unapokuwa unaendesha gari bado wanakuhitaji sana katika gurudumu la tasnia ya filamu Tanzania...

Saturday, January 28, 2012

RAY THE GREATEST THAILAND

 Baada ya kufika tu Thailand nikakutana na kituko hiki jamaa yuko juu tax akipanga mizigo ya abiria, Jamana katika nchi zote nilizotembelea hapa Thailand ni hatari kuna vitu vya ajabu sana kwa maadili ya Mtanzania siwezi kutaja ni vitu gani lakini kwa mtu mwenye ufahamu wa kuelewa utakuwa ushanielewa na balaaa sijui hata kama wanajua Mungu yupo Duniani

 Tulikutana na hawa wazungu disco wakaipenda company yetu wanatokea Uingereza ni wanafunzi wanasoma Thailand

 Hapa ni uwanja wa ndege ukiingia unakutana na mambo haya na watu wengi sana wanapiga picha ukitaka kujua ni kwanini endelea kuwa pamoja nami katika kusoma habari hii 

 Inapendeza

 Kwa karibu unaweza kuona hivi

 Hapa ndipo utapata habari zote kuhusu hiyo sehemu niliyowaonyesha hapo juu 

 Nami sikuwa nyuma kukamata picha ya kumbukumbuThursday, January 26, 2012

THE GREATEST NDANI YA HONG KONG

 Kama kawaida watu wangu niliwaambia kuwa nilienda nchi tatu hapa sasa nipo  Hong Kong, nikiwa ndani ya treni ya umeme nikielekea matembezini, kuna mdau mmoja alisema China na Hong Kong ni nchi moja  sikweli kaka ni nchi mbili tofauti hata unapotoka Hong Kong kwenda china unaingia kwa viza na hata Muong kong anaingia China kwa viza pia, Mdau kwa hiyo tusiwe wajuaji sana wakati hatujui tujifanye wajinga ili tuweze kuwa welevu

 Kama kawaida tukiendelea na matembezi yetu hapa ni baada ya kushuka kwenye treni 

 Cheki mji huo jamani sijui viongozi wetu wa nchi wanapopata ziara za nje ya nchi hawajifunzi kitu kutoka kwa wenzetu mimi naamini nchi yetu tuna kila kitu kwanini tuashindwa kuijenga nchi yetu inauma sana jamani

 Umati ni mkubwa sana sasa kwanini nchi isiwe ya kitajiri, wewe cheki mwenyewe na hii ni kawaida wala  si kitu cha kushangza kwao yani kupishana ni tabu kweli kweli

 The Greatest katika pozi

 Wacha weeeeeeeee 

 Hapa vijana wakicheki flight yetu ni namba ngapi ili tuweze kujua tunaingia geti namba ngapi kwa kuwa viwanja vyao vya ndege ni vikubwa sana 

 Mambo yenyewe ndio haya mpaka ujue unaingia geti namba ngapi ni hatari lazima macho yako yawe makini sana

 Nikipata picha ya kumbukumbu 

 Kijana kapendeza. lakini nimesikitishwa sana na baadhi ya mashabiki wangu kuniambia heti najichubua jamani ningekuwa nalipwa na kitu nachopaka ningekitaja lakini silipwi kwa hiyo siwezi kutaja. Wakiwa weupe wakina Jay Z wameiva sisi tuanjichubua ahaaa jamani
 ubinadamu kazi .

 Choba na The Greatest

 Ndani ya pipa kuelekea Thailand


TRIP OF THE GREATEST IN CHINA

 Baada ya kazi za mchana kutwa kutafuta mavifaa tukaenda kupata lunch kama kawaida katika kipengele cha misosi sifanyagi makosa

 Cheki misosi ya nguvu hiyo

 Kuna yule jamaa niliyeambiwa kuwa huwa achagui chakula aliagiza matunda akaletewa matunda yanayochemka na kutokota kama unapika makande, hapa alichemka .

 Baada ya hapo tukaenda disco kupata burudani za kutosha, ile njemba ndiyo hiyo hapo ilioagiza hayo matunda

 Ukumbi unavyooneka maridadi kwa kwanja za kutosha

 Bahati nzuri tukapata  mwenyeji wa kibongo anayeishi China, Mwanadada huyu anaitwa Husna ni matata sana

 Mambo yakiendelea kupamba moto cheki mwenyewe mambo hayo

 Mrembo akiteta jambo na The Greatest

 Nikiwa na marafiki zangu tukipoza maumivu ya mchana kutwa na burudani mwanana huyu jamaa wa kati anaitwa Choba ana vituko sana, katika kipengele cha uchezaji muziki ni bingwa wa style za ajabu..

 Balaaaaaaaaa jamani

Upande wa vinywaji ulikuwa hivi.