Tuesday, January 10, 2012

BILION (214.6), KUKAMILISHA UJENZI WA DARAJA KIGAMBONI

Na Emmanuel Kimweri
Serikali kupitia Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), leo imetia saini na Kampuni ya Kichina, China Railway Jiangchang Engeneering CO. Ltd kama ishara ya kutekeleza ujenzi wa mradi wa daraja liakalo unganisha wakazi wa Kigamboni na Dar es Salaam utakaogharimu zaidi ya Shilingi bilion 214.6 kwa muda wa miezi 36.


Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt. Ramadhani Dau akitia saini ili kuruhusu Mradi wa Daraja la Kigamboni kuanza.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dkt. Ramadhani Dau, alisema Shirika la NSSF itachangia asilimia 60, wakati serikali itachangia asilimia 40.

“Kunakila sababu ya kukamilisha mradi wa daraja kwa wakati hii nikutokana na kuwepo tayari kwa pesa za mradi, ni matumaini yangu mradi utafanikiwa kwa wakati na watanzania kushuhudia ndoto ya ujenzi wa daraja imekamilika” alisema
Alisema licha ya kusaini mkataba huu kama ishara ya kuanza kwa mradi zipo changamoto nyingi lakini baadhi ya changamoto ni kwa upande wa kurasini kuna kiwanja kinjamatatizo, vile vile baadhi ya makutano ya barabara ya Chang’ombe , Kamta na Tazara ktuokana na foleni kubwa lakini haya yote tunaimani serikali itayapatia ufumbuzi wa haraka.


Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt. Ramadani Dau akifafanua mambo juu ya utekelezaji wa Mradi wa Daraja la Kigamboni

Naye Waziri wa Ujenzi, Dkt. Magufuli amewataka wahandisi ambao wamechukuwa tenda hiyo kufanyakazi kwa kiwango kinacho kubalika na kwa wakati,
“Kutimia kwa mradi ni miezi 36, hii ni kwa makadirio ya juu lakini mradi unaweza kukamilika chini ya miezi 36, hivyo hakuna haja ya kusubiri muda wote ikiwa pesa ya maradi ipo” alisema
Kwa upande wake Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka, almetoa rai kwa watanzania kutumia fulsa ya ajira itakayo jitokeza kwa kwa kipindi hicho chote cha utekelezaji wa mradi,
“Kwa taarifa zilizonifikia kutoka kwa wataalamu wa mradi kuwa kutakuwa na ajira za kudumu 1000, na za muda mfupi 2000, hivyo watanzania tutumie hizo fulsa za ajira kufanya kazi kwa ufanisi na uaminifu kwa maslahi ya Taifa” alisema Kabaka


Wadau na wataalamu mbalimbali wakifuatilia kwa karibu maelezo ya utiaji wa saini kwa Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni

No comments: