Friday, December 25, 2009

MZIGO MPYA WA RJ COMPANY WAVAMIA KIJIJI

Msafara wa crew nzima wa RJ Company ukiwa umewasili kijijini tayari kwa kuanza kazi ya kukamilisha mzigo mpya wa 2010 ambao wadau wengi wanatabiri ndio mzigo utakaosumbua mwaka mzima wa 2010 kutokana na jinsi unavyotengenezwa kwa kutumia vifaa vya hali ya juu na casting zinazobamba katika tasnia ya filam bongo akiwemo Elizabeth Gupta mshiriki wa BBA 2009

Vijana wakiwa tayari kufanya kazi iliyowatuma kijijini kwa kuweka mambo sawa

Camera man Hamidu'Sikazwe' akiwa makini kutayarisha Camera tayari kwa kazi

Dada mainda Make up&continuity wa RJ Company naye akiwa kazini kwa kumtayarisha THE GREATEST tayari kwa kuingia maporini kufanya kazi

Dr Cheni akifanyiwa make up tayari kwa kuingia mzigoni

Hapa sasa kazi karibia inataka kuanza anaonekana JOHARI akimchungulia mtu fulani nje sijui ni nani

Jamani si kweli ni acting ni mimi THE GREATEST nikiwa nimefunikwa shuka na mganga kwa ajili ya kutibiwa

Mganga akiwa makini na kazi yake, chakufurahisha ukija kuona Movie hii hutaamini kama huyu jamaa si mganga maana kafanya njaa ya kufa mtu

Dr Cheni inasemekana yeye ndiye mtaalam wa mambo haya ndio maana akanipeleka nami nikagangwe si kweli jamani

Dr Cheni akiwa anafanya mazoezi kabla ya kushoot mbele ya camera

THE GREATEST NA DR CHENI on set

Vijana hawa inasemekana ndio watakaofunika katika movie hii lakini mimi siamini baada ya movie kumalizika nitawaletea washiriki wote harafu wadau mtachagua mnahisi nani atafunika

Wakiwa on set mbele ya camera ya ukweli

Hapa kazi imepamba moto maana ilifikia wakati mpaka mtu anadondoka anainuka na kuendelea na kazi ama kweli RJ COMPANY IMEPANIA KUJA KIVINGINE Vijana wa GRM PRODUCTION wakiwa makini na kazi yao ni watu wazuri na wanaojituma sana kwenye kazi

Kama kawa mashoot ya kufa mtu utayapata ndani ya mzigo huu

Kila aina ya shoot tunapiga kuhakikisha mzigo unakuwa wa uhakika,Hapa kamera ikiwa nyuma yetu

Mpaka kijijini CRANE ilitumika, Hapa tukitest kabla ya kuitumia namuona kijana FORD mwenye flana nyekundu

CRANE inakaribia kukamilika,Vijana wanaonekana wakiwa hawana mchezo hata kidogo wako makini kabisa

Kama wanavyoonekana Stamford,Hamidu na Steve shoo wakiwa makini kabisa kuhakikisha kazi inakwenda sawa

Kazi ya hapa nashindwa hata kuisimulia Mdau wewe angalia picha tuu utamu utaupata

Mambo yakiendelea.....

Mmmmm mambo yatakuwa makubwa sana ndni ya mzigo huu

Ebwaaana eeeee mazoezi ni muhimu kama ningekuwa sina mazoezi hii scene ikinishinda maana yake ilkuwa si mchezo....

Watu wakiwa kazini huwa hawana mchezo

Eheeeee hii ni balaaaa sasa

Kijana amepania kufunika mwaka 2010.....

Camera men Farid Uwezo akionyesha picha alizopiga kama zimetoka bomba


Wadau namtambulisha kwenu SCRIP WRITER ALLI YAKUTI huyu ndie anayeandika mizigo yote ya RJ COMPANY BIG UP KAKA kazi yako inakubalika

KANUMBA 'THE GREAT' AJA NA LIBENEKE LAKE

Swahiba anavyoonekana mbele ya blog yake inayokwenda kwa www.kanumbathegreat.blogspot.com
Kanumba amekuja kivingine baada ya kuamua kufungua blog yake inayokwenda kwa jina la
www.kanumbathegreat.blogspot.com swahiba wangu wadau wanakukaribisha katika libeneke kwa kuhabarishana habari

Tuesday, December 22, 2009

MAMBO YANAZIDI KUPAMBA MOTO KUELEKEA 2010 NDANI YA RJ COMPANY

RJ Company tuko makini kabisa kuhakikisha mwaka 2010 mashabiki wetu wanafurahia kazi zetu ndio maana tupo makini kuhakikisha tunazalisha kazi ambazo ziko kwenye kiwangi cha hali ya juu ili mashabiki wetu wafurahi kwa maana nyingine tunapenda chalenge ili tujifunze zaidi.Ndio maana kwenye Movie tunayoandaa sasa tuko makini sana katika vifaa mpaka casting kuhakikisha tunatoa kitu bora zaidi

Hemed Suleiman akiwa na Monica Malaki chipukizi aliyeinuliwa na RJ Company katika filam ya Hot Friday kwa mara nyingine tena ameibukia katika Movie mpya baada ya kutesa vilivyo katika Hot Friday

Tulivamia mpaka Hospitali lakini kilichonishangaza nilimkuta Mzee wa Platinum Hemed akilia sijui kilichomsibu ni nini,Tusubiri

Zena Mashauzi shangingi aliyesumbua kwenye DIVORCE aibuka kama Doctor ,Hapa akiongea na Hemed na Elizabeth Gupta katika chumba cha daktari

Kikao kikali kiliendelea ndani ya ofisi chini ya Hemed Suleiman,Hemed naye bosi haya makubwa sasa

Mzee wa Halmashauri ya kichwa Juma chikoka(CHOPA) naye aibuka kivingine, humu ndani kaharibu kinoma

Elizabeth Gupta ndani ya ofisi za Upelelezi akihojiwa


Elizabeth akiwa makini kabisa kufuata maelekezo kutoka kwa DIRECTOR

Rais wa TAFF naye aonyesha njaa zake,Hapa akikata kiu kidogo baada ya kazi nzito

Ebwanaeeeeeeee Elizabeth uso kwa uso na Johari sijui itakuwaje

Baada ya kutesa na HOT FRIDAY , Monica Malaki kwa mara nyingine tena uso kwa uso na THE GREATEST

THE GRATEST nikiongoza kikao ofisini kwangu

Mzee wa Halmashauri ya kichwa naye akutana na THE GREATEST,Sijui ananiambia nini?

Pastor Myamba akiwa na mtoto pembani,Mafans wake msubiri muone Myamba kaja na style nyingine kabisa sio ile mlioizoea

Mimi nilijua labda JOHARI hatakuwemo lakini jana ameibuka kwa makeke na kudai atafunika vilivyo mafans wake wasubiri waone

Masuperstar wa bongo ndani ya pozi la mwaka kabla hawajaingia on set


Chime Chande akiwa on set na dada Mainda akiwa tayari kumpendezesha kijana mpya katika fani ......

Naona mauzo yamekamilika sasa tayari kuanza kazi mshikaji anaonekana amepania kuja kumfunika mshikaji wake Hemed......

Kama kawaida yangu nikiwa kazini uwa sina utani kabisa kijana wangu Kanumba jipange wanaweza watu wakakusahu 201o natania tu mjomba usije ukakimbia mji....

Ni mapozi tu....

Saturday, December 19, 2009

RJ COMPANY YAPANIA KUFANYA MAAJABU MWAKA 2010 NDANI YA MOVIE IITWAYO.........

RJ Company imepania mwaka 2010 kufanya mapinduzi makubwa katika swala zima la filam Tanzania kwa kutumia vifaa vya hali ya juu na kutumia wahusika wenye kubeba haswa uhalisia unaoweza kuwagusa watazamaji vilevile ikiwa na watu makini katika production wanaoweza kufanya kazi kwa umakini wa hali ya juu hiyo yote inafanyika haswa kwa kuleta mapinduzi makubwa Nchini,RJ Company bado wako location kuandaa Movie itakayogeuza kabisa soko la filam Nchini kama mnavoona baaadhi ya picha.

Elizabeth Gupta akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi sijui kafanya nini mimi sijui

AUNTIE EZECKIEL akiwa pamoja na THE GREATEST on set

Camera Men Farid Uwezo akiwa makini kabisa katika kuchukua picha katika Movie ya 2010

Crew nzima ya Production ikiwa makini kabisa katika kutayarisha Movie inayokwenda kwa jina la ................


THE GREATEST mwenyewe nikiwa serious kazini katika kutayarisha CRANE kwa ajili ya kushoot kama nilivyowaambia wadau kwamba mwaka 2010 ni mwaka wa mabadiliko kwa upande wa production pamoja na uchezaji na utayarishaji kwa ujumla wadau mambo yatakuwa makubwa sana ndani ya movie hii


THE GREATEST mwenyewe nikiwa mbele ya CRANE tayari kabisa kwa shooting

Elizabeth Gupta akiwa na Mzee Katembo wakibadilishana mawazo

Tukiwa mbele ya Camera mimi na Auntie huku mtu wa sound Steven Shoo akiwa makini kabisa kuhakikisha sauti inaingia

CRANE ikiwa juu kabisa kutafuta picha nzuri na yenye kuleta msisimko ama kweli mwaka huu mambo si mchezo

AUNTIE EZECKIEL akiwa katika pozi kali ndani ya movie hiyo
Crew nzima ya production ikiwa makini kabisa katika kuhakikisha CRANE inachukua picha nzuri na zilizo na ubora

Hii Movie si mchezo wewe mwenyewe jifikirie Auntie ndani ya nyumba itakuwa balaaaaaa

Mandhari nzima ya Location inavyoonekana

Kusema ukweli Elizabeth sikumtegemea kama atacheza kama nilivyomfikiria kaonyesha uwezo wa hali ya juu kupita kiasi BIG UP sana dada

Elizabeth akiwa na Hemed Suleimani'MZEE WA DRY CHAMA' on set

Elizabeth akiwa makini kabisa mbele ya kamera,Elizabeth anawapa hii mafans wake kwa kumsapoti akiwa ndani ya nyumba ya BBA vilevile anawapa hii Nigerian people kwa kumsapoti mpaka leo kwa kumtaka akafanye Movie Nollywood baada ya kuona baadhi ya picha zake akiwa on set kwenye BLOG yangu

Gari hiyo inaendeswa na Elizabeth Gupta ikifuatiliwa kwa umakini mkubwa na CRANE
Mauaji haya sijui kafanya nani?Lakini namwona Elizabeth na bastola sijiu ndio yeye kaua

Thursday, December 17, 2009

KANUMBA KUSHUSHA MIZIGO MIWILI KWA MPIGO

Game 1ST QUALITY kwa mara nyingine tena jumatatu ya wiki inayokuja ya tarehe 21/12/2009 wanashusha mzigo miwili kwa pamoja inayokwenda kwa jina la SATURDAY MORNING NA THE HEROES OF CHURCH kwa mujbu wa Kanumba ameniambia mizigo hiyo miwili inakuja kufunga mwaka 2010 kwa kupoteza zaidi katika tasnia ya filam, Filam hizo amewajumuisha baadhi ya ya masuperstar na vipaji vinavyochipukia katika medani ya filam kama vile Shamsa Ford na wengine wanaofahamika kama Cloud ,Magali,Aisha Bui na wengine wengi.PATA NAKALA YAKO HALISI SIKU YA JUMATATU

Cover ya THE HEROES OF CHURCH kama inavyoonekana kwa mbele,NAKUKUMBUSHA TENA NDUGU MDAU NENDA DUKANI UKAPATE NAKALA HALISI

Wednesday, December 16, 2009

RJ WAUPANIA MWAKA 2010 KWA KUPOTEZA NA BONGE LA MOVIE

Ndugu Wadau msione watu wanapendeza kwenye luninga ni kazi ya Dada yetu Mainda,Hapa akimfanyia make up Hemed

THE GREATEST mwenyewe huwa sina masihara kazini hapa nikichota jua kwa kutumia kifaa kiitwacho Reflector ili picha itoke vizuri isihathiriwe na mwanga wa jua

Vijana wako makini katika kuangalia picha na sound vinatoka bomba

Ili kuhakikisha mwaka 2010 napoteza kabisa kama 2009 nahakikisha picha inakuwa na sauti iliyo bora kabisa,Hapa anaonekana Stamford akirekebisha Mixer kwa umakini zaidi

Kuna kipindi unatakiwa uwe makini zaidi na picha unayochukua kwa kuiangalia vizuri na kuihakiki,Kama ninavyoonekana nikiwa na camera man Farid Uwezo na Assistant wangu Junior mwenye kofia

Elizabeth Gupta katika hisia kali

Kazi inaendelea kwa umakini wa hali ya juu

Ilifikia kipindi shoot zilinichosha ikabidi niombe msaada kwa kusaidiwa ili mkono usiyumbe na kupoteza balance

Hemed na Flora katika hisia za Mapenzi huku Gupta akiwaangalia kwa kuwatamani, mambo yote haya tunaandaa kwa umakini zaidi na kwa uhalisia wa hali ya juu

Flora Mvungi na Hemed katika mapozi ya ukweli

Elizabeth na Flora katika action ndani ya bonge la movie litakalosumbua 2010

Ebwanaeeee mpaka Auntie ndani ya nyumba basi mzigo utabamba ile kinoma,Norway mmemwona mwenye shati la kijani?

Scene kama hizi ndugu mdau zinachukua sana muda mpaka kuzikamilisha

Usiniue kaka nisamehe tukae tuyamalize,Ndivyo anavyoonekana kijana Hemed akimwambia kaka yake sijui ni nani na hatujui kamfanya nini tusubiri tuone

Huyo ndio Dr Cheni wadau mliokuwa mnamuulizia kwenye maoni naye kaharibu kabisa kwenye hii movie,ITATISHA SANA

Vipi tena THE GREATEST mbona unalia kwani kuna nini tuambie basi tukusaidie

HUKU THE GREATEST,DK CHENI,ELIZABETH,AUNTIE,HEMED NA.................. KWELI KAZI IPO

Wakati action zinaendelea,AFRICA MAGIC PLUS walikuwa wanaonyesha movie ya BEHIND THE SCENE iliyotengenezwa na RJ COMPANY kama unavyoona ndugu mdau kwenye screen

Chini ya usimamizi wa RJ COMPANY wasanii muda wote wanaonekana Happy

Elizabeth na Hemed on set chini ya usimamizi wa THE GREATEST

Elizabeth na Hemed wakijiandaa kwa Shooting

Elizabeth Gupta akiwa na feeling kali sana,kwa kweli dada angu unawatishia akina Johari na kina Uwoya katika hili game la movie Keep it up

Monday, December 14, 2009

RJ COMPANY WANAMLETA TENA ELIZABETH GUPTA KATIKA BONGE LA MOVIE LIITWALO...........

Tukiwa kazini katika kutayarisha mzigo mpya unaotarajiwa kutikisa anga za filamu nchini na nje ya mipaka yetu ambayo inatarajiwa kufungua mwaka 2010,Ndani ya mzigo huu ambao siutaji jina nauhifadhi utakutana na masuperstar kibao akiwemo Elizabeth mshiriki wa Big Brother 2009

Tukiwa kazini huwa hatuna utani hata kidogo,Elizabeth on set

Safari hii RJ haina utani hata kidogo tunataka kuushika mwaka 2010 kama tulivyopoteza mwaka 2009,Nadhani Wadau mnatambua

THE GREATEST mwenywe nikiwa na mtoto Monica Malaki kabla ya kwenda kwenye set

Nikiwa na Elizabeth on set

Hemed Suleiman na Elizabeth wakiwa makini katika kazi,Hii si Movie ya kuikosa wadau

Mambo yakiendelea kupamba moto

Wadau wa tasnia ya filam tegemeeni mambo makubwa kutoka kwa Elizabeth Gupta ndani ya movie hiyo ya ukweli

Nikiwa on set huwa sinaga masihara

Tukiwa na huzuni chanzo ni nini kaa mkao wa kula mwaka 2010





Kijana Steven Shoo akiwajibika kabla ya mbilinge kuanza

Maandalizi yakiendelea

Kijana Hemed akiingia location........

Friday, December 11, 2009

MZIGO WA KUFUNGA MWAKA KUDONDOKA CHRISTMASS

RJ COMPANY inatambulisha mzigo mpya wa kufunga mwaka 2009 na filamu inayokwenda kwa jina la HOT FRIDAY'Baada ya swala kabla ya sabato' Filam iliyosheeni masuperstar kama JOHARI,RAY ,HEMED, Vilevile RJ imeibua kipaji kipya katika tasnia ya filam msichana anayeenda kwa jina la MONICA, filamu hii ndugu Wadau ndio filam ya mwisho kutengenezwa na kampuni ya RJ mwaka huu na ndio filam ya mwisho katika store ya movie ndani ya kampuni.Ndugu Wadau katika tasnia ya filam sio kwamba kila siku tunatoa filam bali filam zinakuwa zimetayarishwa muda mrefu zinakuwa Store na inapofikia muda kila moja inaanza kutoka,kwa maana nyingine huwa nikiingia Location napiga Movie harafu zinakuwa Studio zikitayarishwa huku nikiandaa nyingine harafu napata muda wa kupumzika huku nikianza kutoa moja baada ya nyingine,Itafikia muda kwa mwaka nitakuwa natoa movie moja au mbili inategemeana na soko litakavyoenda.NAWASHUKURU WADAU KWA MAONI YENU

BAADA YA GRADUATION MYAMBA NDANI YA MJENGO WA RJ

Baada ya kumaliza chuo Myamba alitamani kufika ofisi za RJ COMPANY kujua ni jinsi gani ofisi inafanya kazi na kuona mandhari ya ofisi kwa ujumla kwani alishazoea kuona kwenye Blog tu,Na hapa ndio safari yake ya kutembelea ofisi ilipoanza,Baada ya kuingia ofisini Myamba alipata nafasi ya kuonyeshwa kazi mbalimbali na Johari na jinsi Blog inavyofanya kazi

Myamba inaelekea malecture wako walipata tabu sana wewe unaelekezwa na Johari harafu unaongea na simu acha mambo yako kijana

Ulifikia muda wa kupiga picha na DIRECTOR mwenyewe THE GREATEST

Akiwa pamoja na JOHARI

Akapata muda wa kupumzika na kuishukuru RJ kwa kumkaribisha ofisini na kuitakia kila la kheri katika shughuli zake

Wednesday, December 9, 2009

KANUMBA ATAKA KUZAA MTOTO WA CHUPA(TEST TUBE BABY)

KANUMBA 'THE GREAT' amenifahamisha kuwa anataka kuzaa mtoto wa chupa(Test tube baby) na mwanamke atakayekidhi viwango anavyohitaji,Nilipomdadisi kwanini hasa anafanya hivyo akaniambia kuwa ameamua kufanya hivyo kwani ana maamuzi katika maisha yake kufanya analoona anaweza kufanya ili mradi ana uwezo nalo,Ila kaniambia kuwa muda si mrefu atatangaza ni mwanamke gani atakayekidhi viwango anavyohitaji kupitia kwenye Blog yangu na si kwingine,Haya Wadau huyo ndiye THE GREAT'KANUMBA'


THE GREAT akiwa kwenye pozi katika vakasheni fulani niliyofanya naye wiki tatu zilizopita

NI ZAMU YA RIHAMA ALLY NA THEA NANI ZAIDI

Anaitwa Rihama Ally ni Msanii aliyejizolea umaarufu mkubwa katika tasnia ya filam Nchini,Ameshacheza filam nyingi kama vile Fake Promise,Fungu la kukosa,Wrong Number na nyingine nyingi.Nilivyoongea naye muda mfupi uliopita ameniambia kuwa anatarajia kutoka na filam inayokwenda kwa jina la NUNDA amesema kwenye hii filam ameonyesha simanzi ya kufa mtu, Haya Wadau kazi kwenu huyo ndiyo RIHAMA ALLY

Rihama Ally akiwa katika pozi ndani ya viwanja vya Leaders Club katika Bonanza la wasanii

Huyu ndiye Thea mengi nilishamwelezea huko nyuma alipopambana na Auntie leo anakuja tena akiwa ulingoni akipambana na Rihama,Nilivyomtafuta aniambie ana kipi kipya anachokuja nacho kwenye game hii sijafanikiwa kumpata,Wadau mimi sina mengi kazi kwenu

THEA kama anavyoonekana akiwa maeneo fulani hivi jijini

WADAU KUNA FAIDA KUBWA SANA SISI WASANII KUWA NA BONANZA KILA JUMAMOSI

Hapa nikiwa na swahiba wangu Steven Kanumba pamoja na mwandishi wa Global Publisher kuna wadau wengi wa blog yangu wamekuwa wakiuliza kuwa ili bonanza la wasanii lina faida gani? Nawaeshimu sana wadau wa blog yangu na ndio maana nimeamua kuwajibu, Faida ni kubwa sana kwanza kuwa pamoja waswahili wanasema kuwa umoja ni nguvu utengano ni dhaifu pili nikujenga upendo ni furaha kubwa sana wasanii wa bongo tukipendana na pia kuweza kubadilishana mawazo nini tufanye ili tuweze kuwapelekea jamii kitu kizuri na vile vile pia ni sehemu ambayo tunakutana na wasanii mbalimbali ambao wengi wao ni under ground hivyo basi kupata kuwaona na kuwatumia kwenye movie ili nao waje kuwa mastaa wa baadaye kwa ufupi ni hivyo wadau bila shaka mtakuwa mmenielewa asanteni.....

Kama mnavyoona hapa Richie aliyeweka mkono shavuni akiwa pamoja na Dr Cheni na wadau mbalimbali hii ndio faida bonanza watu wkitaka kuwaona mastaa wa bongo basi tunawakaribisha kwenye viwanja vya Leaders Club........

Bibie Blandina Chagula( JOHARI) akiwa pamoja na Jenifer Kiaka( ODAMA) wakionekana wenye nyuso za furaha hii ni moja ya faida ya bonanza wasanii kukutana na kuwa pamoja......

Hapa nikiwa na kijana wangu Yusuph Mlela akichukua maneno mawili matatu kwa kaka yake njia gani apite ili aweze kukaa kwenye gemu kwa muda mrefu...

Hapa nikiwa na Nice Chande ......

Benny Kinyaia akiwa na Yusuph Mlela wakibadilishana mawazo hii ndio faida yenyewe ya BONANZA.......

Mnakumbuka huyu Dada ni mkongwe katika sanaa anaitwa Madina Khamisi Zawadi naye alikuwepo katika bonanza hii ndio faida ya Bonanza lakini tunasikitika kutangaza kuwa huyu dada yetu amefiwa na Mama yake Mzazi na mazishi yanafanyika mchana wa leo pole sana dada yetu wewe ulimpenda ila Mungu kampenda zaidi...

Zawadi akiwa na mwanae mwenye nguo ya njano na wajukuu zake...

Sunday, December 6, 2009

THE WINNER OF BIG BROTHER AFRICA REVOLUTION 2009 IS..............KELVIN

Winner of BBA REVOLUTION 2009 Kelvin akiwa katika jezi ya TANZANIA,Wadau nazidi kumwelewesha mdau aliyekataa kuwa Kelvin ajavaa jezi ya Tanzania nadhani sasa atakubaliana nasi
Hapa Kelvin alipoitangaza nchi yetu ya Tanzania kwa kuvaa jezi iliyoandikwa Tanzania kuna mdau mmoja alikuwa akibisha kuwa Kelvin akuvaa jezi ya Nchi yetu hiyo hapo kaka nadhani utaamini ambacho nilikiandika mwanzo......

Hapa akiwa haamini kilichotokea kwani alilala chini baada ya kutangazwa kuwa yeye ndiye mshindi wa BBA REVOLUTION na kujinyakulia kitita cha dollar 200,000 na cha kuvutia zaidi Kelvin baada ya kupanda jukwaani alivaa Jezi ya Tanzania na kufanya ashangiliwe zaidi na Umati uliohudhuria sherehe hiyo,Hongera kaka sisi Watanzania tunakupenda kwa kututangazia Nchi yetu Ulimweguni

KELVIN akiwa pamoja jukwaani na mwendesha shughuri nzima ya BBA muda mfupi baada ya kutoka ndani ya Mjengo wa BBA

EMMA kutoka Angola ndiye mshiriki pekee wa kike aliyeingia tatu bora, alishika nafasi ya PILI

Mshiriki aliyeshika nafasi ya Tatu,EDWARD'EDDY' kutoka Namibia akiwa jukwaani muda mfupi baada ya kutoka

Mshiriki aliyeshika nafasi ya NNE NZAMO kutoka Malawi muda mfupi baada ya kutoka ndani ya nyumba

NKENNA mshiriki kutoka Nigeria alishika nafasi ya Tano, yeye ndiye alikuwa wa kwanza kutoka katika washiriki watano walioingia fainali

KAMA KAWAIDA YETU YA JUMAMOSI TULIKUTANA TENA LEADERS CLUB

Show zikiendelea ndani ya Bonanza la wasanii,vikundi mbalimbali vya wasanii hufanyaga show za bure viwanjani hapo

Umati wa Watu uliofurika ndani ya viwanja vya Leaders kuhudhuria Bonanza la Wasanii,Ndugu Mdau unakaribishwa nawe pia uje kupata Burudani ya nguvu

THE GREATEST NA THE GREAT tulimfuma live kijana wa gazeti fulani hivi akitafuta Habari fulani za Wasanii ndani ya viwanja,Leo sikutaji jina kijana wangu nakustiri kama ulivyoniomba

Mzee wa Norway kama kawaida yake huwa hakosekanagi ndani ya viwanja hapa akiwa na THE Director of Director Selles Mapunda na Swahiba wake Richie na Msanii fulani hivi wa Kaole.Ujumbe wenu Ndugu zetu wa Norway nilimwambia Cheni kasema msiwe na wasi atawajibu siku si nyingi

Mtumishi wa Mungu JB akiwa anatoa neno kwa wasanii wenzake Mashaka na Bi Mwenda

Vichekesho huwa havikosekanagi ndani ya Bonanza,Hapa wanaonekana wakiweka pozi niwapige picha na Mashaka akiwapa kampani ya pamoja

Baada ya pilika pilika za shule kwisha Pastor Myamba naye alijumuika na wasanii wenzake kuwapa somo na maarifa aliyoyapata darasani, Hongera kaka kwa kujumuika nasi tena

Saturday, December 5, 2009

KAMA KAWAIDA YA RJ COMPANY KUTEMBELEWA LEO TUNAYE AUNTIE EZECKIEL MJENGONI

Auntie aliingia ofisini kwa mikwara mizito na mapozi kama anavyoonekana

Mwenyewe aliamua kukaa kwenye makochi,lakini mikao yake mwenyewe nilikoma

Akiwa katika pozi la kusimama ndani ya mjengo wa RJ COMPANY

Auntie utaniangusha'' nishakwambia hapa ofisini mapozi gani hayo nitashindwa kufanya kazi miye

Johari na Auntie wakiwa katika mapozi mjengoni

THE GREATEST mwenyewe nikiwa na Auntie sambamba kabla sijaenda kumwonesha ninapofanyaga kazi zangu

Wewe Auntie unashangaa nini hasa,Hapa ndipo ninapotayarishaga mizigo yangu inayosumbua katika tasnia ya filam nchini


Baada ya kumwonyesha ofisi na sehemu ninapofanyia kazi Auntie hakuamini kabisa alijua mizigo inatayarishwa nje ya ofisi za RJ,Hapa akinishukuru kwa kumkaribisha ofisini

Hapa nikimtakia safari njema nami nikimwambia karibu tena RJ COMPANY

Auntie akiondoka ndani ya ofisi za RJ kama anavoonekana

Thursday, December 3, 2009

THE GREAT MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI YA HILTON NUSSERY SCHOOL

The Great akiwa na mtoto katika mahafali ya Hilton Nussery School!!!! ndugu yangu inabidi na wewe upate wa kwako uanze kulea umependeza sana na huyo mtoto kama baba yake vile!

Watoto wa Hilton wakiselebuka na ngoma za kiasili aiseee wamependeza kweli!!! hapa lazima tupate wakina WANNE STAR wabaadae!!!

Karibu Ndugu mgeni rasmi wetu Steven Kanumba hayo ni maneno ya mwenyeji wake kama unavyoona

Hawa ni Best pupils wa mwaka huu!!! hongereni sana taifa linawasubiri mje kulitumikia!!!

Aiseee Miss Tanzania 2020 huyo hapo jamani manamuona pozi la ukweli!!

Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi The Great!!!!!!

Muda wa kutoa risala ulipowadia kama kawaida yake The Great maneno mengiiiiiiii utasema yuko bungeni!!!

Tuesday, December 1, 2009

MZIGO MPYA WA RJ COMPANY WAINGIA MTAANI

RJ COMPANY wameingiza sokoni filamu mpya inayoenda kwa jina la FAIR DECISION 'MAAMUZI SAHIHI' ni Filamu kali sana ndugu Mdau iliyowashirikisha Masuperstar kibao kama JOHARI,MAINDA,IRENE UWOYA NA ODAMA usiikose kuitafuta ila TUNAKUOMBA UNUNUE NAKALA HALISI INAYOPATIKANA MADUKANI KOTE

MSHINDI WETU NI MZEE CHILLO

Mzee Chillo ndio mshindi wetu wa wiki iliyopita kwa kumbwaga Mzee mwenzake Magali.Tunakutakia kila la kheri katika kazi zako za sanaa kaza mwendo Wazee wenzako wanakuja kwa kasi

MSANII EMANUEL MYAMBA AMEPATA DEGREE YA SOCIOLOGY!!!!

Keki ya mzee mzima Myamba kama unavyoiona siku alipopata Degree yake ya Sociology katika chuo kikuu cha Dar es salaam.

Kama kawaida The Greatest nilikuwepo kuumpa support ndugu yangu kwa kazi nzito ya kusoma maana si mchezo kupata Degree kwani hata katika sanaa Myamba ni msanii ninayemkubali sana

Emanuel Mgaya a.ka. Masanja akitoa mawaidha mawili matatu kwa ndugu yetu.

The Great Kanumba nae hakuwa nyumba akitoa kajirisala flani hivi kwa ndugu yetu.
Mzee Myamba mwenyewe baba Mzaa Chema akiwa na nyuso ya Furahaa sana!! Kweli kuzaa raha jamani usomeshe na uone matunda kama haya.

Dada Grace huyu ndio dada Mkubwa wa Emanuel!!! Pole sana dada najua kijana alikuwa anakubom sana kipindi alipokuwa shule

Joyce Kiria Nkongo Staring wa Bongo Movie nae hakuwa nyuma kushow love kwa ndugu yetu!! Ila sijui kama Joyce hakuwa kikazi zaidi maana yeye matukio kama haya hayampiti!! Wadau tusubiri tuone Jumatano hii kama kweli Kiria hakuwa na yake. Dont forget to tune to EA TV Bongo Movie saa TATU na NUSU usiku utaweza pata kuona sherehe hizi kwa kifupi.

Hapa kama kawaida mambo ya MSOSI ndugu yangu uko serious na MENU hutaki utani!!!!
Kwa wale mnaomfahamu ndugu huyu MAARUFU PASTOR MYAMBA siku ya Jumapili Tarehe 29/11/2009 ni siku ambayo hataisahau katika maisha yake ya KIELIMU kwa kupata DEGREE YA SOCIOLOGY mimi kama THE GREATEST na BLOG YANGU kwa Ujumla tunampa Hongera
kwa kufikia hatua hii muhimu katika miisha!!!! kwa ufupi Myamba alipata mafunzo ya elimu ya Awali katika Shule ya Msingi MDETE baada ya hapo akajiunga na SEKONDARI MARANGU MOSHI na A LEVEL alisoma JITEGEMEE na kujiunga na CHUO KIKUU MLIMANI mnamo mwaka 2006 mpaka alipohitumu Shahada yake ya kwanza ya Elimu Ya SAYANSI YA JAMII.Kiusanii Myamba kwa mara ya kwanza nilicheza nae katika FILAMU ya JOHARI ambayo alionyesha umahiri mkubwa mpaka kubatizwa jina la PASTOR filamu nyingine ambazo ameshacheza ni FAKE PASTOR,PENINA, DAR TO LAGOS na nyeginezo nyingi. nimeongea ameniambia kwa sasa Atajikita zaidi katika kiwanda hiki cha filamu na anatarajia kuja na SERIES zake ambazo zitapatikana muda si mrefu zitakwenda kwa jina la PASTOR MYAMBA TEMPTATION ambapo mpaka sasa RJ Company iko katika mazungumzo nae.

DR Cheni kwa mbali namchek akiwa anajaribu kupata mawasiliano.

Maya,Myamba,Wolper na Joyce Kiria wakishow love.

Jamani wadau karibuni muda huu watu wanakuwaga hawataki mchezo mambo ya maakuli yalikuwa si mchezo.

Sunday, November 29, 2009

MASUPERSTAR WA BONGO WAKUTANA KWENYE BONANZA LA WASANII

Hapa ni baada ya mechi kuisha kati ya wasanii wa filam na wasanii wa maigizo matokeo yalikuwa ni 3-1 wasanii wa maigizo kwa kuwashinda wasanii wa filam.

Unajua nyie Vijana wa siku hizi hamfanyi mazoezi mimi mngenipanga ningewashona tu hawa,Mzee Chillo akimwambia Chiki baada ya mechi kuisha.

Hapa nikipasha kabla sijaingia uwanjani kuwaonyesha vitu vyangu hakika kama Maximo angeniona angenipeleka challenge kuchukua nafasi ya Boban

Mashabiki waliofurika kuja kuangalia mechi ya kukata na shoka iliyofanyika viwanja vya Leaders.

Ahaaa muda unayoyoma halafu tushalala harafu Maximo sijamwona sijui kamtuma mwakilishi wake lakini poa tuu......

Wee Johari hawa Watoto wako au umewaazima uje kutuonyesha tu huku.

Mdau wa Tasnia ya filam za kibongo Chime akiwa na swahiba wangu THE GREAT

THE GREATEST nikiwa na Ben Kinyaiya tukijadili jambo fulani hivi.

Kumbe mpaka misosi inapatikana,Dr Cheni,Auntie Ezeckiel na Nice Chande wakionekana wakiongeza afya.....

Dr cheni kwa mapozi bwana au unataka Norway wakuone maana wamekumisi sana huko waambie basi utaenda lini Ahaaaaa......

Dr Cheni inatosha washakuona huko Norway ukiwa na watoto halafu lazima uende na mmoja wapo huko Norway.

Interview mbalimbali huwa zinafanyika ndani ya viwanja vya Leaders hapa anaonekana Yusuph Mlela akihojiwa na Ben kinyaiya

THE GREATEST nikihojiwa na Sauda Mwilima

Mjomba Mpoto akiwa pamoja na Band yake wakiburudisha wasanii na watu mbalimbali waliohudhuria ndani ya Bonanza, huyo msichana unayemwona pembeni ya Mjomba ni Mary Lucas alikuwa mshiriki wa BSS 2009

THE GREATEST NA THE GREAT pamoja na mtayarishaji wa kipindi cha Bongo Movie Sterling Joyce Kiria

Hapa nikiwa na mtoto wa nguvu Nice Chande...

Riyma Ally akiwa katika pozi la nguvu...

Friday, November 27, 2009

WADAU LEO JIONI TULIKUWA MATEMBEZENI MAENEO YA VISIWA VYA BONGOYO

The Great Steven Kanumba tukiwa njiani kuelekea visiwa vya Bongoyo, Wadau tulikuwa katika matembezi ya kawaida tu lengo na nia ni kupumzika na kubadilishana mawazo nini tufanye ili tuwapelekee mashabiki vitu vizuri katika tasnia ya filam nchini Tanzania....

Hii ndio boti tuliokuwa nayo katika mapumziko yetu mafupi jioni ya leo katika visiwa vya Bongoyo...

Hiki ni chumba cha kulala cha boti hiyo ......

Hapa tukiwa katika kiboti kidogo kuelekea katika boti kubwa ili tuanze msafara.....

Hapa tukiwa na Muheshimiwa Alan Kalinga ni mtayarishaji wa movie toka nchini Uingereza....

Mambo yakiendelea katika mapumnziko yetu mafupi katika visiwa hivyo

Ndani ya boti......

Dada Asha Baraka Mkurugenzi wa kampuni ya Aset Club naye alikuwepo katika msafara huo

Hapa tukiwa na ndugu Alan Kalinga producer toka nchini UK.....

Thursday, November 26, 2009

TOT BAND YATAMBULISHA NYIMBO ZAO MPYA NDANI YA HOTEL YA WHITE SAND

Vijana wa TOT BAND wakitambulisha nyimbo zao mpya kwa wadau mbalimbali wa muziki

Waheshimiwa wakifuatilia utambulisho wa nyimbo mpya za TOT BAND,Uliofanyika jana usiku katika Hotel ya White Sand.....

Mc wetu alikuwa ni Maimatha wa Jesse akitangaza jambo fulani hivi ili mambo yaweze kwenda sawa.....

Dr Cheni aliyevalia shati jekundu akiwa pamoja na msanii mwenzake Mayasa Mrisho......

Muheshimiwa Capten Komba aliyevalia suti ya nguvu akiwa pamoja na muweka fedha wa chama cha CCM ndugu Amosi Makala mwenye shati la bluu lenye mistali wakifuatilia uzinduzi huo kwa umakini wa hali ya juu...

Ahaaa mwenyewe The Greatest mtu mzima nilikuwepo ndani ya nyumba nikiwa pamoja na Steven Kanumba,tulialikwa na Muheshimiwa mbunge bwana Capten Komba ili tuweze kusikia nyimbo mpya za TOT BAND na tuweze kutoa maoni mawili matatu hivi ili band yake iweze kusonga mbele. Ilikuwa ni burudani ya kutosha toka kwa vijana wapya wa TOT BAND chini ya kiongozi mpya bwana Bad Bakule jogoo la mjini......

Warembo mbalimbali walikuwepo nao katika uzinduzi wa kutambulisha nyimbo mpya za TOT BAND huyu dada aliyevalia miwani ni mtangazaji wa TBC 1 anaitwa dada Lisa.....

Banza Stone mwanamziki wa zamani wa TOT BAND naye alikuwepo katika uzinduzi huo.....

Mamaaa Dotinata akiwa sambamba na Mumewe Mohamed Posh pamoja na mzee Chilo aliyevalia shati la kitenge.....

Mambo yakiendelea....

Tuesday, November 24, 2009

ELIZABETH GUPTA NDANI YA MJENGO WA RJ COMPANY MIDA HII

Hapa nikimuonyesha Dada Elizabeth baadhi ya kazi za RJ Company Tz Ltd.....

The Greatest mwenyewe nikimpa Elizabeth Gupta zawadi ya movie ya( DIVORCE) talaka tatu

Hapa nikimpa tangazo la movie ya Divorce, Pembeni yake na Elizabeth ni manager wake kwa jina anaitwa Julio....

Mambo yakiendelea ndani ya mjengo wa RJ Company TZ LTD

Wadau kama mnavyoona niko na Elizabeth Wa BBA Revolution ametembelea sasa hivi. RJ Company inampa pongezi kwa kutuwakilisha katika jumba la BBA kwa hatua aliyofikia Tanzania tunatisha,Wadau mtakuwa manajiuliza ujio huu ni vipi? tupo katika mazungumzo na Elizabeth ya kufanya nae kazi kama mambo yakienda vizuri dada huyu tutapiga nae mzigo wa nguvu! hivyo mkae mkao wa kula

Elizabeth akiwa anacheki kazi mbalimbali zinazofanywa na RJ,Jamaa wa pembeni huyo ni Manager wake anaitwa Julio.

Elizabeth akiwa na Johari ndani ya mjengo sasa hivi,wadau hawa wakicheza pamoja itapendeza eehh?

Bado tupo na elizabeth anapiga tour ndani ya mjengo jamani!!!!

Elizabeth akiwa na Mdau namba moja wa RJ Company!!!

Bado Elizabeth anachek mambo flani flani mapya mapya ya RJ
Pozi la nguvu na Elizabeth na mzee mzima mwenyewe The Greatest

Aise Elizabeth yuko makini hapa namuonyesha jinsi blog yangu ilivyokuwa inampa support ya kutosha wakati yuko ndani ya BBA

Hapa anabadilishana mambo mawili matatu na Johari!!!

Hapa Elizabeth anacheki baadhi ya Script za ukweli za RJ!!! Jamani kama mambo yakienda vizuri mambo yanayokuja ni balaa!!!


Sunday, November 22, 2009

BONANZA LA WASANII LAZIDI KUFANA

The Greatest na swahiba wangu Steven Kanumba( The Great) tulikuwepo katika kubadilishana mawazo na baadhi ya wadau waliofika kwenye bonanza la wasanii

Ebwanaeeeeee jamaa kwenye keyboard yupo si mwingine ni swahiba wangu Kanumba.

Aunt akiwa amepozi na washikaji wake ndani ya viwanja hivyo, Pia nawakumbusha wadau kuwa jumamosi ijayo kutakuwa na mechi kali ya mpira wa miguu, ahaaaaa lazima nizungushe namba tisa na Kanumba yeye kaniambia atacheza namba kumi kama sijakosea Cheni aliniambia kuwa atacheza namba nane balaaa itakuwa ndani ya viwanja vya Leaders Club....

Wasanii mbalimbali katika pozi la pamoja...

Saturday, November 21, 2009

WADAU WA TASNIA YA FILAM TANZANIA MUDA SI MREFU NILIKUWA NAPIGA PICHA KWA AJILI YA COVER ZA MOVIE MBILI AMBAZO NI .......

Kama unavyoona ni pozi la majonzi The Greatest mwenyewe nikiwa najaribu kutafuta pozi ambalo litaendana na story ya movie husika .......

Sidhani kama unamkumbuka mrembo huyu ni kitambo sana alikuwa anaitwa Rayuu jina lake kamili ni Alice Bagenzi aliyekuwa muigizaji wa kundi la Kaole sanaa lakini kwa sasa anarudi ulingoni katika Tasnia ya movie za kibongo chini ya RJ Company Tz Ltd ambayo ndio itakayokudondoshea kitaani mzigo huo muda ukifika....

Pozi mbalimbali katika kutafuta picha itakayofaa kwenye cover muda wa siku mbili tatu hivi nitawadondoshea cover lenyewe mlione wadau....

Pozi ili ni la movie ileeee niliyokuwanikishoot kipindi kile ambacho nilikuwa nawaletea matukio yake inaitwa HOT FRIDAY inatoka baada ya FAIR DECISION kuingia mtaani mwisho wa mwezi huu......

Muendelezo wa picha hizo kijana huyu anaitwa Hemed Suleiman....

Bibie Blandina Chagula (Johari) naye yupo kwenye movie hiyo kama mnakumbuka, Mzigo utakuwa wa maana si mchezo mastaa wote wa movie za kibongo wapo ndani ya HOT FRIDAY.....

Mtoto wa kike huyoooo anaitwa Monica Malaki yeye naye yupo ndani ya HOT FRIDAY ni msanii mpya wa RJ Tanzania Ltd...

Wednesday, November 18, 2009

WANAMUZIKI NA WAIGIZAJI WA TANZANIA WAFANYA KIKAO CHA PAMOJA

Bwana Benny Sitta naye alijumuika na sisi kama mdau ndani ya kikao hicho

Dada Luiza Mbutu mwanamziki wa bendi ya Twanga Pepeta naye alikuwepo kwenye kikao cha kujadili jinsi wanavyoibiwa kazi zao..

Ambwene Yesaya (AY) mwanamziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva )naye alikuwepo katika kikao hicho

Mzee Kasimu Mapili mzee wa enzi zileee ni mwanamziki wa zamani sana huyu naye alikuwepo kutoa busara na hekima zake, Waswahili wanasema utu uzima dawa....

Tuesday, November 17, 2009

Wadau wa TASNIA ya filam Tanzania walikusanyika pamoja na wanamuziki kujadili jinsi wanavyozidi kuibiwa kazi zao...

Jackob Stephen( JB) wakiteta kitu na Kulwa Kikumba( DUDE) katika kikao hicho kilichofanyika jana majira ya saa 9 za mchana katika ofisi za Mkuu wa mkoa wa Dar-es-salaam.......

Rais wa wa shirikisho la wasanii Tanzania nzima ndugu Salum Mchoma akimwaga sera katika mkutano huo...

Baada ya kikao kuisha wadau walitawanyika Lakini kikubwa wadau ni hiki tunaibiwa sana kazi zetu sasa tumechoka ndio maana tunakuwa na vikao vya mara kwa mara ili kuweza kufanikisha kilio chetu ca muda mrefu. Tusaidieni wadau kwa kutokununua kazi zilizo feki au kukodisha kwenye library na tunawaonya wale wanaohonyesha filam zetu kwenye cable tunataharifa ya baadhi ya mikoa kama TABORA, SHINYANGA,SONGEA nk tunaomba muache mara moja kabla hatua za kisheria kuchukuliwa....

MAPACHA WANNE WAJA NA MAMBO MAPYA YA KUKATA NA SHOKA

Hawa ndio mapacha wanne, Kalala Jnr,Chaz Baba,Khalid Chokoraa pamoja na Jose Mara. Vijana machachali wa muziki wa dance nchini Tanzania wanazindua albam yao mpya mwisho wa mwezi huu tarehe 30-11-09 ndani ya ukumbi wa Kinondoni Stereo. Mnakaribishwa wote kuwaunga mkono vijana hawa wanaojituma sana kupitia fani yao ya muziki tuwapeni sapoti vijana wetu ili wafikie malengo yao ya kutoa burudani kabambe..

Na bila kusahau watakuwa wanatoa burudani kila Jumatatu ndani ya ukumbi wa Kinondoni Stereo

Sunday, November 15, 2009

BONANZA LA WASANII NCHINI TANZANIA LAZIDI KUNOGA MNAKARIBISHWA WADAU WOTE

Rais wa Taff bwana Salum Mchoma pamoja na Joyce Kiria Nkon"go muendeshaji wa kipindi cha Bongo movie wakiwa makini kuzungumzia jambo flani hivi ..

Mama yake na Monalisa Suzan Lewis (Natasha ) naye alikuwepo.....

Jini Kabula ndani ya pozi na mtoto wa ukwelI, sijui ni wa kwake?

Yusuph Mlela kijana wa (Milionea Club)

Wacha maneno yako weeeeee, Mzee Magari akiwa na mrembo ndani ya viwanja vya Leaders Club katika bonanza la wasanii lifanyikalo kila jumamosi. Nyote mnakaribishwa..
Monalisa,Teha akiwa pamoja na mzee wa dry chama,katika pozi la ukweli katika viwanja vya Leaders Club ndani ya bonanza la wasanii....

Washikaji kibao walikuwepo ndani ya viwanja hivyo....

Eheee Aunt naye alikuwepo yupo biiiiize na simu yake sijui alikuwa anaongea na nani?

Bibie Rose Ndauka akiwa pamoja na Baba Haji ndani ya viwanja vya Leaders, Dada ulipotelea wapi naona sasa umeanza kuonekana ongera karibu bwana umoja ni nguvu utengano ni dhaifu...

Hemed Suleiman kwenye pozi la ukweli na mzee Chime, ahaaa inapendeza washikaji mmefanana kama ndugu au tabia zenu zafanana za dry chama?

Friday, November 13, 2009

KANUMBA NA IRENE UWOYA WAIVAMIA RWANDA

The Great Steven Kanumba jana mida ya saa nane mchana alipanda ndege kuelekea nchini Ruwanda kwa ajili ya kwenda kwasalimia mashabiki wake wa Rwanda na kufanya show mbili tatu kwa kipindi atachokuwepo nchini humo. Kwa taharifa aliyonipa mwenyewe kwa njia simu kuwa atarejea nyumbani siku ya jumapili...

Irene Uwoya Ndikumana yeye anaondoka mchana wa leo kuelekea nchini Rwanda kwa Mumewe nadhani watakutana na Swahiba wangu Kanumba na watafanya show kwa pamoja nchini humo.

MR CHUZI AVAMIA MJENGO WA RJ COMPANY LTD

Msanii na mtengenezaji wa vipindi vya tamthilia na filam nchini Tanzania ndugu Chuzi kihan"gala alikuja kuzitembelea ofisi za RJ COMPANY Tz LTD, Sasa tumekuwa na umoja wa ukweli kabisa tofauti na zamani kulikuwa amna mambo ya kutembeleana lkn kwa sasa tunashukuru Mungu tumekuwa na upendo dhati....

Katika pozi ndani ya mjengo wa RJ COMPANY Tz LTD, Ukitaka kuijua RJ kwa undani zaidi tembelea website yetu amayo ni www.rjtanzania.com

Wednesday, November 11, 2009

KARIBU DADA ELIZABETH UMEFIKA NYUMBANI KWENU TANZANIA POLE NA KIBARUA KIZITO CHA KUIWAKILISHA NCHI YETU

Elizabeth akwapungia mashabiki

Hapa akiwa amewekwa mtu kati na maparazi wetu, Wakimuhoji maswali mawili matatu hivi baada ya muda mfupi kuwasili akitokea South Afrika ...

Hatimaye muwakilishi wetu wa BBA 4 Elzabeth Gupta arejea nyumbani, Karibu dada sio mbaya umejitahidi sana tunakukaribisha kwenye ulimwengu wa filam Tanzania....

Hapa Dada yetu akijaribu kuonyesha mbembwe za hapa na pale karibu bongo

Mashabiki nao hawakuwa nyuma kupata japo kumbukumbu kuwa walimpokea super star Elizabeth..

Sina uhakika bila shaka huyu ni ndugu yake wakikumbatiana kwa furaha kubwa sana, Tulikukumbuka sana dada yetu tunakupenda sana karibu kwa mara nyingine tena

FAMILIA YA MZEE UWOYA YAMFANYIA PARTY YA KUMPONGEZA MTOTO WAO IRENE UWOYA KWA KUPATA MUME HONGERA DADA

Masuperstar wakusanyika kumpongeza super star mwenzao kwa kupata Mume, Hapa watu wakikandamiza misosi ya nguvu Wolper, Aunt,na Mayasa Mrisho...

Wanamziki nao walikuwepo kwenye party hiyo, Khalid Chokoraa mwanamziki wa Twanga Pepeta aliyevalia miwani meusi .....

Irene Uwoya mlengwa wa party hiyo ......

Richard naye kwa msosi, mmmmmmmm,,,,


The Greatest nikiwa na mdogo wangu Hemed Suleiman ....
Mmmmm kijana wangu Mchopanga ana mwenyewe huyo;;;;

Richard wakiselebuka na Dada Johari katika party ya kumpongeza Irene kwa kupata Mume,Ni party iliyoandaliwa na familia ya Mzee Uwoya...

Wasanii walitoa burudani mbalimbali

Eheeee,,,,, Mama yake Irene Uwoya naye yumo jamani hapa akikumbuka enzi zake za mwaka 47

Wadau huyu ndiye Mama mzaa chema, Mama yake na Irene Uwoya .....

The Great Steven Kanumba akiwa katika pozi na Aunt Ezeckiel katika party ya kufa mtu...

Vijana watanashati Richard wa( BBA 2 winner ) akiwa na mwakilishi wetu wa mwaka jana wa (PROJECT FAME) ndugu Hemed Suleiman, wakiwa wamepozi kiana hivi heti waliniuliza nani ana sura ya mvuto kuliko mwenzake? mimi sijui kazi kenu wadau......

The Great akiwa na pacha wa Uwoya, Jackline Wolper...


Mama Ndikumana akiwa amejichanganya na wadau wa Tasnia ya Filam Tanzania,Huyu kijana aliyvalia shati la mistali meusi anaitwa Inno Bachard

Sunday, November 8, 2009

WATANZANIA WOTE TUMEUMIA JAMANI LAKINI SIO MBAYA UMEJITAHIDI DADA YETU ELIZABETH HONGERAAA

Huyu ndie dada yetu Elizabeth,Wiki hii ametolewa ndani ya jumba la BBA 4 sio mbaya WATANZANIA wenzangu, mpaka hapo alipofikia Elizabeth anastshili pongezi hongera dada umefika mbali asiye kubali kushindwa basi si mshindani

MAISHA CLUB YATEKETEA KWA MOTO

Huu ndio ukumbi maarufu jijini Dar-es-salaam, Maisha club leo mida ya mchana umeteketea kwa moto chanzo bado akijajulikana ...

Mkurugenzi wa Aset Club Dada Asha Baraka alikuwepo sehemu ya tukio.

Mama Sweya mmiliki wa Maisha Club akiwa katika dimbwi la mawazo baada ya mali kuteketea kwa moto...

Duhuuuuuu moto umepamba moto...


Saturday, November 7, 2009

ILIKUWA KAMA KAWAIDA WASANII KU SHOW LOVE NDANI YA VIWANJA VYA LEADERS CLUB.

Kama Victor Mkambi vile akikamua keyboard kwa makini si mwingine ni Hisani Muya a.k.a Tino.

Kama kawaida Ali Choki akifanya mambo yake akikamua demokrasia ndani ya viwanja vya Leaders; The Great mwenyewe si mwingine...

The Greatest nikiwa na mdau kutoka South Africa katika pozi la ukweli..

Watu wakiselebuka ndani ya Leaders Club.

Fatuma Makongoro( BI MWENDA) alikuwepo pia kama unavyomcheki akiwa na wajukuu zake,Wanajivunia kuwa na Bibi super star au sio jamani, Mnakaribishwa jamani katika viwanja vya Leaders Club kila Jumamosi ktk bonanza la wasanii..

NANI MKALI KATI YA MZEE CHILLO AU MZEE MAGALI

Anaitwa Hemed Olotu( Mzee Chillo),Msanii anayekubalika katika tasnia ya filam akiwa anaekti kama mzee au Baba au Mwalim utapenda kumuangalia kwani hachoshi hata kidogo, wiki hii anachuana na Mzee wa masauti(Mzee Magali)

Anaitwa Charles Magali(Mzee Magali) au ukipenda Mzee wa masauti anasumbua sana katika tasnia hii ya filam za kibongo akiwa mzigoni huwa hapendi masihala hata kidogo anachuana vikali na Mzee Chillo.Wadau kama mlivyoniomba nami nawaleteni katika mpambano huu kazi kwenu sasa

Friday, November 6, 2009

THE WINNER IS.......................RICHIE

Huyu ndiye mshindi wetu Richie aliyembwaga Dk Cheni kwa kura 52 dhidi ya kura 38 alizopata Dk Cheni, jumla ya kura zilizopigwa ni 95 na kura 5 zimeharibika.Hongera sana kaka Richie ongeza juhudi usibweteke kwa ushindi huu. Vile vile washindi wote watapewa zawadi na wadhamini wa blog hii mtatangaziwa siku maalumu ya kupewa zawadi

Kaka hongera kwani umeonyesha ushindani wa hali ya juu ongeza juhudi katika kazi, kaza buti ndio muda wa kazi huu

RICHARD BBA WINNER 2007 NDANI YA MJENGO WA RJ COMPANY

Richard BBA Winner 2. 2007 akiwa ndani ya ofisi za RJ Company alipokuja kunitembelea mshkaji wake kwa kunipa Hongera kwa kufungua ofisi na yeye kunialika kwenda kumtembelea ofisini kwake.Ndiyo maendeleo hayo ndugu wadau

Tukiwa kwenye pozi ndani ya mjengo wa RJ Company (T) Limited....

Richard BBA Winner 2 akiwa mapokezi ndani za ofisi za RJ Company nyuma yake kukiwa na frem za picha ya Divorce na Fair Decision mzigo unaokaribia kuingia kitaani mwezi huu......

Richard akiwa kwenye pozi tofauti ndani ya mjengo...

Sikusita kumkaribisha sehemu ambako huwa nafanyaga editing na mambo yote kuhusu movie mpaka inakamilika Akhsante Richard kwa kuja kunitembelea nami sitasita kuja mjengoni kwako.

WAKATI WASANII WATANZANIA WAKIWEKA VIKAO VYA MALA KWA MALA KWA AJILI YA KUTETEA HAKI ZAO LAKINI MAMBO YANAZIDI KUWA MAGUMU

Wasanii mbalimbali walikusanyika kwenye kikao kilichofanyika Mango Garden kwa ajili kutetea haki zao lakini mambo yetu yanazidi kuwa mabaya. Huyu ni Fatuma Makongoro (BI MWENDA)

Angalia wasanii walivyokuwa na majonzi. Maisha yao yanazidi kuwa magumu kwa sababu tu ya watu wachache wanaotuibia kazi zetu na kufanya maisha ya wasanii wa Tanzania kuwa magumu....

Colleta Raymond msanii wa kike akisikiliza mada kwa umakini katika kikao kilichofanyika jana Mango Garden ....

Kulwa Kikiumba (Dude) Msanii wa Bongo Dar-es-salaam naye alikuwepo kwenye kikao..

Steven Kanumba nae alikuwepo kwenye kikao hicho.....
Cd feki zinazosambaa mitaani zenye filam kumi kwa moja zimekamatwa Arusha,Mwanza na Dar es Salaam. Vile vile zimetapakaa mpaka Congo na Nchi jirani.Je? Wasanii tutafanikiwa kwa hali hii?Watanzani wenzangu kazi tunazofanya ni ngumu sana lakini wanaofaidika ni watu ambao hawatumii nguvu kubwa.Ombi letu kwa Watanzania wote mlio nje ya nchi na ndani ya nchi msinunue kazi zenye mfano wa macover haya.

Cd feki ya Oprah kama inavyoonekana kwa mbele ya cover. Jamani huu ni unyonyaji mkubwa inauma, Kwenye cd moja zinakaa movie kumi tutafika kweli kwa mtindo huu...

Cd feki ya chanzo ni Mama iliyokusanya na filam nyingine kama inavyoonekana nyuma ya kasha....
Kama inavyoonekana kwa mbele. Je tutafanikiwa kama wenzetu?????

Tuesday, November 3, 2009

GAME 1ST QUALITY YAFANYA PARTY YA KUMALIZA SINEMA ZAO MBILI PAMOJA NA KUTOA SHUKRANI MBELE ZA MUNGU

Maimatha wa Jesse mtangazaji wa Eatv aliyevalia nguo ya blue akiwa pamoja na Sauda Mwilima mtangazaji wa Staa Tv katika party ya nguvu.

Mapaparazi nao hawakuwa nyuma kuchukua matukio mbalimbali bwana Zakayo Maguru Cameraman wa kampuni ya Game 1st Quality
Baadhi ya wadau walioudhuria kwenye party Game 1st Quality

The Great Steven Kanumba akiwa pamoja na Aunt Ezeckiel kama mualikwa katika party hiyo. Hapa Aunt akitoa shukrani zake za dhati kwa watu walimfikisha hapo alipo....

Irene Uwoya hakuwa nyuma ndani ya sherehe. Akiwa katika pozi la upoooole mtoto wa watu jamani sasa ametulia sana nakuombea kwa Mungu akuongoze hivyo ulivyo..

Steven akiwa na wageni waalikwa wakibadilishana mawazo mawili matatu. Nini cha kufanya ili waikuze Tasnia ya filam Tanzania

Cloud akiwa katika pozi la ukweli na mke wake wa ukweli, Kaka niko nyuma yako nakuja Mungu akipenda.
Waswahili wanasema kuwa utu uzima dawa wazee wetu nao walikuwepo kwenye party ya Game 1st Quality ni miongoni mwa washiriki katika sinema hizo mbili, Ambazo ni Saturday Morning na Crazy Love

The Greatest nami nilikuwepo ndani ya party hiyo ya swahiba wangu Steven Kanumba na washikaji wa kutosha kina Mchopanga, Miyamba, Dr Cheni, Maya na wengineo wengi....



Warembo nao walikuwa wa kumwaga

Sunday, November 1, 2009

MAMBO YA SIMBA NA YANGA YALIKUWA NA BURUDANI YA AINA YAKE

Mshabiki wa Yanga akiwaambia mashabiki wa Simba kuwa leo lazima tuwamalize

Hapa mashabiki wa Simba na Yanga walipokutana mitaa ya msimbazi na kutambiana nani zaidi ya mwenzake. Duhuu ilikuwa burudani ya kutosha....

Mashabiki wa Simba wakiwaambia mashabiki waYanga kuwa sisi ndio kiboko yenu....Mlioukuwa nje ya nchi mlikosa mambo jamani....:

Yanga wakisubiri timbwili lianze

Simba nao hawakuwa nyuma kusubiria mpambano kuanza. Huo ndio umati wa mashabiki wa Simba walioudhuria
Nami sikuwa nyuma kushuhudia timbwili kati ya Yanga na Simba nikiwa makini kufuatilia mpambano huo wadau....

Kaka Lundenga naye alikuwepo kufuatilia mpambano huo


Eheeee Mama Ndikuma nilimfuma akiwa na Jackob Stephen( Jb )msanii maarufu nchini Tanzania wakibadilishana mawazo mawili matatu kabla ya mpambano wa watani wa jadi kuanza

Mambo yakiendelea Irene Uwoya akiwa na mlinzi wake anemlinda aliyevalia kofia nyeusi. Wacha weeee siku hizi wasanii wa bongo kama mtoni vile wanalindwa ongera Dada hayo ndio maisha ya kistaa

Ila mwisho wa yote Simba vijana wa msimbazi waliibuka kidedea. Ongereni vijana ila mlishangilia sana kama mmechukua ubingwa au mkutegemea kuifunga Yanga.....''