About Us

NIFAHAMU NAMI NITAKUFAHAMU

UTANGULIZI
RJ ni kampuni liliyoanzishwa 2006 kwa madhumuni ya kuendeleza filamu bora nchini Tanzania na nje
ya nchi.Kampuni ya RJ ipo mkoa wa Dar es Salaam maeneo ya Sinza Mori.

WAMILIKI
Kampuni ya RJ inamilikiwa na waaigizaji wa filamu, Vincent Kigosi a.k.a Ray The Greatest na Brandina Chagula a.k.a Johari. Waigizaji hawa waliamua kujiunga na kuanzisha kampuni hii.

Waigizaji hawa wamekubalika na jamii kwa umakini wao na jinsi wanavyowakilisha ujumbe kwa jamii. Watu wengi maisha yao yamebadilika kutoka na filamu zao.

MADHUMUNI
Madhumuni ya kampuni ya RJ ni kuhakikisha filamu za Kitanzania zinakuwa katika viwango vya hali ya juu sana na pia kuhakikisha ujumbe unaotolewa kwa jamii unaadibisha, elimisha, unaonya na kufundisha kwa lika zote.

MAMBO YANAYOZINGATIWA KATIKA KAMPUNI YA RJ
RJ inahakikisha yafuatayo yanafanyika kwa umakini zaidi
-Filamu zinatolewa kwa kiwango cha juu.
-Vifaa vinavyotumika ni vya kisasa na vinauwezo wa kutoa filamu bora
-Watalaamu wa filamu ni wale tu waliosomea na wabunifu
-Tunazingatia kwenda na muda kama ulivyopangwa na mteja wetu