Tuesday, December 4, 2012

ARUSHA AFRICAN FILM FESTIVAL..

 Wadau kama nilivyowaambia hapo mwanzo kuwa nilipata mwaliko Arusha kwenye tamasha linalokwenda kwa jina la ARUSHA AFRICAN FESTIVAL na hapo niliweza kukutana na wasanii mbalimbali wa Afrika, siku hiyo kulionyeshwa sinema yangu ya Sobbingi Sound  watu wengi waliokuwepo hapo waliipenda sana..hapa nikiwa na msanii mkubwa toka Nigeria anaitwa Clario tuliongea mengi sana na nimejifunza vitu vingi sana toka kwake.. 

 The Greatest nikiwa najibu maswali baada ya Movie yangu ya Sobbing kuisha

 Maswali yalikuwa ni mengi sana na naamini nilayajibu kwa ufasaha sana.

Ulifika muda wa  Clario Chukwurah(msanii kutoka Nigeria) kuonyeshwa kwa sinema yake inayokwenda kwa jina la Danger Signal, hapa nikiifuatilia kwa makini sana..

 baada ya Movie kuisha nami niliuliza ya kwangu na Dada yangu Clario alinijibu vizuri tu.

 Baada ya matukio yote tuliweza kubadilishana mawazo na msanii mwenzangu.

Hapa nilkuwa naelezea jinsi gurudumu la filamu linavyokwenda kwa sasa mapungufu yake na mazuri yake wadau hivyo ndivyo mambo yalivyokuwa nawashukuru Watanzania wote mnaonisapoti kwa kununua kazi zangu 

4 comments:

Imami8 said...

Keep it up bro. Your the best

Anonymous said...

cong.kaka!endelea like that nawewe ujulikane foreign like those actors from nigeria.

Anonymous said...

after good network n relations,,,
am expecting collaborations(joint venture)between two companies..
emmer matutu
stay longer...and do good things

Anonymous said...

vaa viatu vya the great (kanumba) kaka, inawezekana kama tu utaamua kujituma kama yeye alivyokuwa anajituma bila kukatishwa tamaa. hapa nchini jina lako tayari limeshakuwa inavyohitajika, make sure sasa unapasua anga la kimataifa ambapo utakuza jina lako zaidi na sanaa ya tanzania kwa ujumla
all the best ray.