Tuesday, March 12, 2013

RWANDA FILM AWARDS

Wadau wa kiwanda cha filamu Tanzania ningependa kuwafahamisha kuwa tulipata mwaliko Nchini Rwanda kwa ajili ya kuweza kushiriki katika tuzo hizo kwa kweli wasanii wa Rwanda na Ishusho Company waandaji wa Tuzo hizo wamefanya kitu kikubwa sana pamoja na serikali ya Rais Kagame kwa kufanya kitu ambacho hata sisi Watanzania hatujawahi kufanya, pamoja na kazi zetu kukubalika sana lakini hatuna tuzo za aina yoyote ile, hii ni aibu kubwa sana tangu waanze kucheza sinema Wanyarwanda hata miaka mitatu hawana lakini wameshakuwa na tuzo kubwa , huu ni mfano wa kuigwa tufanye kazi na tuache majungu. Hapa nikiwa pamoja na mzee Majuto ndani first class

Hiki ndio kikosi kizima kilichoalikwa na Serikali ya Kagame Jb, Uwoya, Ray pamoja na Mzee Majuto, kwa kweli Wanyarwanda wanaupendo wa dhati kwa wasanii mpaka mtu unajisikia raha kuwa msanii si hapa kwetu, baadhi wa wadau wanakujua kabisa kama wewe ni msanii lakini mtu anjifanya hakujui muwe na upendo na wasanii wenu jamani kwani wanaitangaza Nchi vizuri Kimataifa

 
Hapa tukiingia katika jiji la Rwanda ,The Greatest nikipokewa mizigo na wenyeji wetu..

Furaha zilitawala baada ya kuingia ndani ya Kigali..

Mzee Majuto katika tabasamu mwanana..

Tukielekea Hotelini Five Star Hotel, kweli nabii hakubaliki kwao..

Tukiwa tumefika Hotelini..

Msafala mkubwa ukitusindikiza kuelekea sehemu husika

The Greatest 

Tukiwa na Mzee Majuto sehemu ya mapumziko kabla ya kuonyeshwa vyumba tulivyofikia..

hapa ndipo nilipopumzika kijana wenu The Greatest..

Picha ya pamoja na mdau..

Mapaparazi pia hawakuwa nyuma kumuhoji The Greatest..

Siku tuliofika ilikuwa ni siku ya Wanawake Duniani hivyo tulialikwa Serena Hotel kushuhudia hafla hiyo ambapo mwanamuziki kutoka nchini Uganda Chamelione alifanya show ya kufa mtu,

Jb na Uwoya 

The Greatest nikiingia ukumbini..

Umati mkubwa ulijaa kuja kumuona Chamelione pamoja na wasanii wa filamu kutoka Tanzania..

Mambo yakiendelea kama kwaida yake...

The Greatest nikisalimiana na Waziri wa Michezo Nchini Rwanda..

Tukiwa makini kuangalia show ya Chamilione na mrembo Uwoya akipata picha ya kumbukumbu kupitia cm yake ya kiganjani..Show ikiendelea....

Irene Uwoya...

The Greatest..

Chamilione akifanya show kali ndani ya Serena Hotel.. 

Nikiteta jambo na Dada yangu Uwoya..

King Majuto..

Show ilikwisha na tulielekea hotelini...

10 comments:

emmanuel matutu said...

HONGERA KWA KILA UNALOFANYA ISPOKUWA DHAMBI TU,,(mie nakubali na kutafuta sana)
mwili si ndo huo kaka
bado hujapatia tu mavazi...
inabidi uanze kusearch intertnet uone wakina WALCOTT, CRISTIN RONALDO, NA VANPERSIE... WANAVYOTUPIA SUIT... NOUMER AFU NDANI TISHIRT KALI SANA.. SUIT YENYEWE BROWN AU KAKI WENYE CHUKI WATAKUBALI TU

Unknown said...

Safi sana kweli nabii hasifika kwao, tubadilike watanzania si mmeona wenyewe

Unknown said...

Big up mko juu

Unknown said...

Safi sana mko juu kweli nabii hasifiki kwao

Unknown said...

Safi sana mko juu kweli nabii hasifiki kwao

Anonymous said...

Word mdau yaani nimempendaje The greatest huo ndo mwili sasa wa kiseleb haswaa, hapo ni kuzijulia pamba tu....wakilisheni kwa sana tu

Anonymous said...

Kaka hongera kwa kukata weight, last week nilikuwa holiday inn nilikutana na Zao lako la kwenye waves of sorrow Miriam sikumjua kaka amekata weight kama wewe kapendeza mpaka nikabaki mdomo wazi,hi kwa Rj nzima pia mkono wa pongezi kwa Miriam (Batuli)

Anonymous said...

Hongera huo ndo mwili mana nilihisi ule unene utakusababishia maradhi........soon utakuwa model pia..
(ney-Kilimanjaro)

Anonymous said...

mbona haulink kwa fb na twitter

Anonymous said...

Irene kazeeka jamani, ama kweli wanaume wa bongo wafujaji wamemtumia weeeeeeee sasa huyo Kawa kama kazaa watoto 6 daaaah talk to her amrudie mumewe uzuri wote umekimbia, Zai wa Canada