Thursday, March 28, 2013

SEND OFF

Jana ilikuwa ni Send Off ya mke mtarajiwa wa Idrisa Makupa (Kupa) iliofanyika maeneo ya Mbezi ilikuwa ni shughuli ndogo tu ya kumuaga binti yao anayekwenda kwa jina la Mary wa kushoto pamoja na mpambe wake wakiwa wanameremeta kama nyota harusi yenyewe itafanyika siku ya Jumamosi ijayo katika ukumbi wa new urafiki uliopo maeneo ya Shekilango..

Jimmy Mafufu akiwa pamoja na Mke mtarajiwa wa Kupa, Huyu naye ni bwana harusi mtarajiwa maana hawa mabwana wameamua kufunga ndoa kwa pamoja na ukumbi mmoja. itakuwa hiyo Jumamosi ijayo Hongereni sana vijana wa Bongo Movie Unit.

 Kupa na Mkewe mtarajiwa..

 Muda wa msosi ulifika..

 Cloud 112 wa kushoto,  Msanii mkubwa Nchini Tanzania naye alikuwepo kumpa sapoti kijana wake.

Picha ya pamoja.

Mtitu Mkurugenzi wa kampuni ya 5 Effect akiwa pamoja na mkewe wakipata msosi.

Mambo yakiendeleaaa..

Mwenyekiti wa Kamati wa harusi hizo bwana Mauma akiwa pamoja na katibu wake Mama Loraa Masai..

 Ratiba za chakula zikiendelea.

Kupa Hongera sana kijana kwa kuamua kuvuta jiko la kuliweka ndani si kitu kidogo unastahili sifa kijana Mungu awabariki muishi maisha yenye upendo na amani tele..

1 comment:

Anonymous said...

hongereni sana nimeipenda hii shughuli simple nawatakia kila la heri