Monday, January 9, 2012

HENRY MDIMU NA ANGEL PETER WAMELEMETA
Mwandishi wa Habari za Burudani na Michezo wa Mwananchi ambaye pia ni Mtangazaji wa Times FM "Kituo cha Kazi" Henry Mdimu pichani maarufu kama Zee la Nyeti jana aliamua kukubali yaishe pale aliupofunga ndoa yake takatifu na mwanadada Angel Peter. 
Mdau Henry Mdimu akitambulisha ndugu, jamaa na marafiki zake huku ubavu (mkewe) wake ukisikiliza kwa makini wakati wa utambulisho huo. Mdimu aliwavunja watu mbavu wakati wa tafrija hiyo pale wakati wa utambulisho alipomsimammisha mama yake mdogo na kudai kuwa enzi ya utoto wake aliwahi kimbia sindano Hospitali na kumwachia malapa mama yake huyo chumba cha sindano. Pia alipomtambulisha mjomba wake alidai siku moja alikamata vijana walio mtania Mdimu na kuwapa adhabu ya kuosha vyombo nyumbani kwao. 
Hapa akimlisha mamsap wake wa kufa na kuzikana.
Wakati wa maakuli uliwadia na maharusi ndio walioongoza kwa wageni waalikwa katika zoezi hilo.
Mdau Mroki Mroki na mai waifu wake pia walikuwepo katika mnuso huo.

Msanii Bongo Fleva,Barnabas akitumbuiza katika hafla hiyo.
Mzee wa Libeneke,Ankal Michuzi na ubavu wake (kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Maharusi.
Mduara ukisongeshwa.

Ma MC's

2 comments:

Aunt said...

Mbona hakuna surprise ya birthday kwa swahiba mwaka huu ,au kisa ana gari ya bei kubwa ?badilikeni

Anonymous said...

Thanks for one's marvelous posting! I definitely enjoyed reading it, you might be a great author. I will be sure to bookmark your blog and definitely will come back sometime soon. I want to encourage you to definitely continue your great work, have a nice weekend!
my web page: asuntoturkista.net