Wednesday, January 11, 2012

 MZEE KIPARA KATUACHA
Mwili wa marehemu Mzee Kipara ukiwa ndani ya gari kuelekea katika chumba cha kuhifadhia maiti Mwananyamala.
Mtoto wa kaka yake aliyejulikana kwa jina la Aisha (kushoto) akisaidiwa na msanii wa maigizo, Zawadi, kuelekea kwenye gari ya maiti.Msanii wa maigizo, Bi Mwenda, akilia kwa uchungu.
Msanii wa maigizo, Mariam Athuman ‘Kalunde’, aliyekuwa anamhudumia Mzee Kipara hadi kumfia mikononi mwake.
Mtoto wa Mzee Kipara, Said Fundi (kushoto), akimsaidia dada yake.
MAJONZI na vilio leo vimetawala katika nyumba aliyokuwa anaishi mwanzilishi wa kundi la maigizo la Kaole, Fundi Said ‘Mzee Kipara’ aliyefariki dunia leo asubuhi maeneo ya Kigogo jijini Dar baada ya kusumbuliwa na maradhi ya miguu kwa muda mrefu.

1 comment:

Anonymous said...

Mungu ailaze roho yake pema peponi!