Thursday, January 12, 2012

MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 48 YA MAPINDUZI ZANZIBAR LEO
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, akikagua gwaride maalum wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika leo Uwanja wa Aman mjini Zanzibar .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Aman mjini humo.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, akipunga mkono kwa waandamanaji waliokuwa wakipita mbele ya jukwaa kuu wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika leo Uwanja wa Aman mjini Zanzibar .
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar leo Januari 12, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar leo Januari 12, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Msafara wa Rais wa Zanzibar ukiingia Uwanjani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Shariff Hamad.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar leo Januari 12, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar leo Januari 12, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwa jukwaani wakati ukipigwa wimbo maalum wa Taifa wa Zanzibar.


SOURCE: MICHUZI

No comments: