Sunday, January 29, 2012

DSTV SO MUCH MORE

 Nilipotua tu bongo nilipata mualiko toka kampuni ya Dstv so much more,Dhumuni la mualiko huo nikupata mafunzo ya Video Production kwa ujumla wake mimi kama mwakilishi wa wasanii wote waliopata mualiko huo tunasema asante sana kwa kampuni ya Mult choice kutuletea wataalam kutoka South Africa na kupata mafunzo ya kutosha kwa kweli tulipata vitu muhimu sana ambapo awali havikuwa kichwani mwaetu, hatuna cha kuwalipa zaidi ya kumwachia Mungu wa Isack na Yakob kufanya kazi yake.

 Huyu jamaa wa katikati anaitwa Adam Juma ni mkurugenzi wa kampuni ya Visual Label Next Level ni maarufu sana katika swala zima la muziki wa bongo fleva, Yeye ndiye alieleta vifaa vyake kwa ajili ya practical, mara ya kwanza ulipokuja uongozi wa Mult Choice walikuja kutusikiliza sisi wasanii wa Tanzania tuna matatizo gani ndipo tulipowaambia kuwa tunahitaji kupata mafunzo na ndipo wakaamua kutuletea wataalam hao, na sio sisi tu tuliokuwepo katika mafunzo hayo, bali walikuja wasanii na maproducer kutoka Kenya katika mafunzo hayo yani yalikuwa ni muhimu sana kuliko hata pesa kwakweli tumejifunza mengi tegemeeni makubwa sana toka kwetu kwa sasa maana vifaa vya kutosha tunavyo na elimu ya kutosha tunayo sasa wadau mnategemea nini hapo kama si kula chakula bora

Hapa tukipata chakula cha mchana kushoto kwangu ni producer kutoka Kenya

 Mambo yakiendelea huyu dada naye ni producer toka Kenya tukipata misosi na kubadilishana mawazo walijifunza vitu kutoka kwetu nasi tulijifunza kutoka kwao ilikuwa ni semina wa siku tatu

 Pia tulikuwa na wawakilishi toka kampuni ya Pili Pili kulia kwangu

 Kama  kawaida jamani kijana aliomba kupiga picha na kusema akirudi kwao hawataamini kama alikutana na Ray The Greatest na ndio maana akusita kupata picha ya kumbukumbu

 Mama na Mwana Monalisa na Natasha kushoto

 Picha ya pamoja

 Watu wakipta mapumziko kidogo kwa kupata chai na baadaye kurudi katika darasa

 Mambo yakaanza hapa tulikuwa tunafundishwa jinsi ya kushika boom ili kupata sauti nzuri, mwenye flana ya orange ndiye alikuwa mwalimu wetu

 Mambo yakiendelea camera 7D ya ukweli mbele yako

 Safi sana

 Hapa tukipata mafunzo ya taa ili kupata mwanga safi katika sinema zetu

 Hapa tukielekezwa jinsi ya kupata engle nzuri katka uchukuaji wa picha tukiwa location

Hiki ni kibaoa muhimu sana wakati wa shooting

5 comments:

Anonymous said...

Hiyo ni step nzuri namuona kanumba leo kwenye blog yako, hope mtazika kabisa tofauti zenu mrudi kama zamani, jamani kumbukeni mlipotoka kaka zangu

Tony said...

Dalili njema kuona picha ya kanumba bila shaka ule ujinga unaelekea kwisha,wanaume hawanuniani.

Anonymous said...

Ray this wats up boy, nimefurahi sana umeweka picha za swahiba wako, mwenyezi Mungu awazidishie heri.

Anonymous said...

ray naomba tuelimishe kuhusu kuhusu hicho kibao muhimu kaz yake nini hasa maana nakiona sana kwenye cinema za hollywood, tupe darasa..thank you

Anonymous said...

Nimefurahi kweli kuona picha za swahiba wako naomba haya mambo muyamalize kiume bana. Wengi tunajua mlikotoka na mafanikio yenu ila wenye chuki wanataka kuwatenganisha tafadhali malizaneni tofauti zenu hatutaki kuwaona kwenye magazeti ya udaki sisi ni wapenzini wenu na tunawapenda saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana