Saturday, January 28, 2012

RAY THE GREATEST THAILAND

 Baada ya kufika tu Thailand nikakutana na kituko hiki jamaa yuko juu tax akipanga mizigo ya abiria, Jamana katika nchi zote nilizotembelea hapa Thailand ni hatari kuna vitu vya ajabu sana kwa maadili ya Mtanzania siwezi kutaja ni vitu gani lakini kwa mtu mwenye ufahamu wa kuelewa utakuwa ushanielewa na balaaa sijui hata kama wanajua Mungu yupo Duniani

 Tulikutana na hawa wazungu disco wakaipenda company yetu wanatokea Uingereza ni wanafunzi wanasoma Thailand

 Hapa ni uwanja wa ndege ukiingia unakutana na mambo haya na watu wengi sana wanapiga picha ukitaka kujua ni kwanini endelea kuwa pamoja nami katika kusoma habari hii 

 Inapendeza

 Kwa karibu unaweza kuona hivi

 Hapa ndipo utapata habari zote kuhusu hiyo sehemu niliyowaonyesha hapo juu 

 Nami sikuwa nyuma kukamata picha ya kumbukumbu



7 comments:

Anonymous said...

dah Ray naona mkorogo umekubali, mpaka umekutoa streachmark kama wema.hongera bwana unapaka cream gani

Chris Jumanne said...

hayo ambayo hayaandikiki ni yapi kaka???

we sema kama umekuta machangu wanajiuza kwa sana au umekuta mashoga...

sio vigeni hivo kaka tuambie japo tufaham ili tukipata nafasi ya kwenda na sie tuwe tunajua kukoje japo kwa muhtaasari bana

Anonymous said...

unajuwa wewe Ray hata sikuelewi unasema hutumii mkorogo je na kioo hutumii ? hebu jiangalie katika kioo utajuwa tunaongea nini ...

khaaa!!!

muddy washington said...

dogo naona walimpeleka patpong na skumvit ndani ya bangkok ndio maana ana hadithia dunia nzima..pale kama mara yako ya kwanza lazima utakua na hadithi nyiiiiingi,ndio dunia ilivyo bwana kigosi muwe mnatembea tembea sio dubai dar mmemaliza picha nyiiiiiingi kwenye ngazi za umeme,nyie na yule dadaenu dida mnapenda sana kupiga picha kwenye ngazi,nashukuru sasa manji kawaletea pale kwenye kitu chake barabara ya nyerere

Anonymous said...

kah ulivyojichubua???????????? wewe mkareeee unapaka nini karolite nini? au ni cream gani wapaka mwe? naona unashindana na johari hahahahhahaha

muddy washington said...

dogo naona walimpeleka skumvit na patpong hapo bangkok,halafu ray china na hongkong ni nchi moja sema china imeaicha hongkong iwe ni nchi yake ya kibiashara kwa maana china ni wajamaa sasa hongkong ni kama marekani yani ubepari kwa kwenda mbele,lakini ni sehemu ya nchi,ni kama hapa kwetu wewe ukiwa mdogo bado huko mikoani kwenu zamani zanzibar kwenda ilikua lazima uwe na passport japo ni sehemu ya tanzania,wengi passport zetu za kusafiria ulaya n.k. tulizipata kwa kisingizio cha safari ya zanzibar huwezi amini lakini habari ndio hiyo!

Caris said...

Wee Mchizi Mudy washington acha kumfanya kila mtu mshamba kwa kuwa tu labda wewe umepata bahati ya kutembelea nchi kadhaa.Hata wee mwenyewe ulivyofika sehemu kama hizo kwa mara ya kwanza ulishangaa shangaa sembuse Ray, wee nini bana. Acha ushamba wa kutaka kuonekana unajua wakati wee mwenyewe pengine umekariri tu baada ya kusimuliwa. Ulizaliwa ukiwa mshamba,ukakua ukiwa mshamba sasa ni wakati wa kuachana na habari za kishamba, sio kila kitu lazima ukosoe kama huna la kuchangia kaa kimya. Nenda wewe basi Thailand halafu utuwekee picha zako ukiwa unasimulia kila kitu unachokiona kama unadhani ni kazi nyepesi. Acha USHAMBA wa kujifanya unajua miji wakati hujui chochote.