Tuesday, January 17, 2012

SIKU ZA KUISHI DUNIANI MBUNGE WA CHADEMA MAREHEMU REGIA MTEMA ZIMEKWISHA. 

Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Mama Tunu Pinda, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko.

Askari wa Bunge wakishusha Jeneza katikagari kuelekea mahala palipoandaliwa rasmi kwa ajili ya shughuli za kuaga.

Askari wa Bunge wakibeba Jeneza kuelekea mahala palipoandaliwa rasmi kwa ajili ya shughuli za kuaga.

Askari wa Bunge wakibeba Jeneza kuelekea mahala palipoandaliwa rasmi kwa ajili ya shughuli za kuaga.

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Willbload Slaa, akitoa salama za rambirambi.

Mwenyekiti wa CHADEMA, FreemanMbowe, akitoa salama za rambirambi.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akitoa salama za rambirambi kwa niaba ya Serikali.

Spika wa Bunge, Anne Makinda, akitoa wasifu wa mare hemu katika shughuli zake za kibunge na salam za rambirambi kwa niaba ya Bunge.

Katibu Mkuu wa Chadema Dkt. Slaa na mkewe wakiwa bize wakichati na simu 'sare sare' zinazofanana wakati wakiwa katika shuguli hiyo ya kuaga mwili wamarehemu. Haikuweza kufahamika mara mojawalikuwa bize katika suala lipi hasa.
Wengine pia walikuwa bize katika kunasa matukio ya shughuli hiyo, kama anavyoonekan mdada huyu, ambaye kivazi chake tu kilikuwa gumzo katika maaa kama hapo kwenye msiba, "utazani anaenda disco au Beach" walisikika baadhi ya watu wakinong'ona.

Baadhi ya watu waliohudhuria shughuli hiyo.

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, wakiwa katika shughulia ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyeagwa leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Regia anatarajia kuzikwa kesho nyumbani kwao Ifakara.

6 comments:

Anonymous said...

is this real u?vicent kigosi?cz naona kama kuna mtu tofauti anapost,anyway its all gud. i lve ya blog

cute

Anonymous said...

RAY KAAANGU NAKUBALIANA NA WEWE HIZI CM SIKU IZI JAMANI ZINATEKA AKILI ZA WATU MNO HATA KWENYE MATUKIO MUHIMU YAKUITAJI KUCONCENTRATE MBAYA ZAIDI WOTE NA MKEWE WAPO MBELE KBS.JOYCE KIRIA NAE JAMANI GAUNI MTEGO M2PU MPK MISTARI YA NANIHII ALOVAA NDANI UNAIONA

Anonymous said...

KWELI MISIBA ILIKUWA ZAMANI WATU BIZE NA SIMU BILA HOFU HUYU MWINGINE NAE SHUTI KIGAUNI CHA KUBANA AFU ANAPIGA PICHA HAZIDI HAIPUNGUI KIATU CHA KISIGINO JAMANI MSIBANI????? OKEY TUSEME UMETOKEA KAZINI BASI HATA KUFUNGA KANGA????? AMAKWELI WANAWAKE LIVE

Anonymous said...

jamani nimechekaje mie na hizi picha????? yani Slaa na mkewe ndo wamenimaliza afu wapo mbele kbs shuti simu sare sare. mbavu zangu mie lol

Anonymous said...

huyu Joyce jamani kweli hana haya?? au mi ndo mshamba???? msibani kweli kuvaa hivo afu unapita huku na kule cjui kipiga picha au video. Anyway labda mie mshamba mana Bongo ya sasa si ya mwaka 47 km alivosema prof jay

Anonymous said...

RAY ACHA USHAMBA INAJULIKANA KABISA KWENYE TANSIA YA SANAA NINI KIMETOKEA (MZIBA WA MZEE KIPARA) SASA WEWE UNAJIFANYA KAMA HUJUI? HATA KAMA UNABEEF NA WATU AU MZEE MWENYEWE NDIO UMESHINDWA HATA KUONYESHA HISIA ZAKO SHAME OF YOU!